Mwakyembe kumkabili Onyango
Na Addolph Bruno
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Benson Mwakyembe anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na Mkenya Joseph Onyango kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki ambao kwa sasa unashikiliwa na Mwakyembe.
Pambano hilo la kimataifa litakuwa ni la uzito wa kati (Middle Weight) kilogram 72 itakalofanyika Novemba 20 mwaka huu katika uwanja wa Majimaji Mjini Songea.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa Pambano hilo, litachezwa mjini Songea kupanua wigo wa mchezo huo mikoani ambako tayari umeanza kupokelewa na wadau.
Benjamini Chuma alisema limeandaliwa na Kampuni ya Maguaz Investmemt ya Jijini Dar es Salaam ambapo tayari Onyango amethibitisha kuja nchini kupambana na Mwakyembe.
"Maandalizi yanaendelea kufanyika na tayari Mwakyembe ameanza kujifua kambioni kwake Songea., " alisema Chuma na kuwataka watanzania kumsapoti bondia huyo.
Wakati huo huo Chuma alisema kabla ya pambano hilo, bondia Abdallah Mohamed 'Prince Nasim' wa Tanzania anatarajia kupanda ulingoni na Mkenya James Onmyango Oktoba 8 katika ukumbi wa DDC Keko Dar es Salaam.
Chuma alisema pambano lisilo la ubingwa litatanguliwa na mapambano mengine yenye ushindani mkali ambapo bondia Cosmas Cheka wa Morogoro atazichapa na Pinde Shomari wakati Dotto Mstapha ataoneshana kazi na Manti Abuu wote wa Dar es Salaa,.
No comments:
Post a Comment