Tangazo

Pages

Thursday, September 22, 2011

BFT YASAKA MABONDIA WA KUSHIRIKI MICHUANO YA OLIMPIKI

SHIRIKISHO la ngumi za ridhaa nchini (BFT) limeandaa programu kwa ajili ya timu ya Taifa kufuzu kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika London, Uingereza mwakani.

Programu hiyo ya BFT tayari imeanza kwa mabondia wa timu hiyo kufanya mazoezi huku BFT wakishughulikia udhamini kupitia makampuni pamoja na Serikali.

Akizungumza Dar es Salaam , Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema tayari Shirikisho la Ngumi Afrika (AFBA) limetoa ratiba ya mashindano kwa ajili ya nchi wanachama kushiriki ili ziweze kufuzu kucheza michuano hiyo ya Olimpiki.

Mashaga alisema wanatakiwa kucheza mashindano makubwa matatu yanayoandaliwa na AFBA ili Tanzania iweze kushiriki michuano hiyo ya Olimpiki.

"Endapo tungekuwa tumefanya vizuri katika mashindano ya Mataifa ya Afrika 'All Afrca Games' tungekuwa tumejipunguzia mzigo wa kusaka viwango vya kufuzu,"alisema Mashaga.

Kwa mara ya mwisho Tanzania ilifuzu kushiriki michuano ya Olimpiki kwa upande wa ngumi mwaka 2007 lakini hata hivyo bondia wake Emilian Patrick alizuiwa kushiriki michuano hiyo baada ya Tanzania kukumbwa na kashfa ya dawa za kulevya nchini Mautius.

No comments:

Post a Comment