Tangazo

Pages

Thursday, September 29, 2011

KASEBA NA MANENO WATAMBIANA WAKUMBUSHWA SHERIA

Mabondia Japhert Kaseba (kushoto) na Maneno Osward wakitunishiana misuri walipokutana, Dar es salaam leo kukumbushwa sheria mbalimbali zitakazotumika katika mpambano wao utakaofanyika jumamosi hii katikati ni Katibu, wa Chama cha mchezo wa ngumi kinachosimamia mpambano huo. PST. Anton Lutta. (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
 Mabondia wakichangia mada



Mabondia Japhert Kaseba (kushoto) na Maneno Osward wakitunishiana misuri walipokutana, Dar es salaam kukumbushwa sheria mbalimbali zitakazotumika katika mpambano wao utakaofanyika kesho katikati ni Katibu, wa Chama cha mchezo wa ngumi kinachosimamia mpambano huo. PST. Anton Lutta.

Tuesday, September 27, 2011

NANI ZAIDI NGUMI KINONDONI VS TEMEKE

MBWANA MIYAYUSHO WATAMBULISHA MPAMBANO WAO


Bondia Fransic Miyayusho (kushoto) naMbwana Matumla kulia wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa ubingwa wa Mabara (UBO) Dar es Salaam , utakaofanyika mwishoni mwa mezi ujao katikati ni mratibu, Mohamed Bawazir.


MABONDIA WA KINONDONI
MABONDIA WA TEMEKE

Bondia Mbwana Matumla (kushoto) na Fransic Miyayusho kulia wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa ubingwa wa Mabara (UBO) Dar es Salaam , utakaofanyika mwishoni mwa mezi ujao katikati ni mratibu, Mohamed Bawazir.

Monday, September 26, 2011

YOHANA ROBART KUTETEA UBINGWA WAKE



BINGWA wa mkanda wa TPBO Yohana Robert amechezea kichapo kutoka kwa Jonas Godfrey katika pambano lake la maandalizi la kutetea ubingwa huo lililofanyika juzi katika ukumbi wa DDC Magomeni Dar es Salaam.

Kutokana na kichapo hicho Robert atakuwa amejipunguzia heshima ya kutetea ubingwa huo ambao anatarajia kuutetea Septemba 30 mwaka huu jijini Tanga kwa kutwangana na bondia Alan Kamote.

Awali Robert alitakiwa kutwangana na Mohamed Shaaban ambaye hakutokea siku ya kupima uzito hivyo kumfanya Robert kubadilishiwa mpinzani katika dakika za mwisho.

Akizungumzia kichapo hicho Kocha wa Robert, Rajab Mhamila alisema kitendo cha bondia wake kubadilishiwa mpinzani ndicho kilichopelekea kichapo kwa bondia wake.

"Mimi sijafurahishwa kabisa bondia wangu kupigwa kwa sababu imempunguzia heshima ya ubingwa wake pia kitendo cha Shaaban kuingia mitini nacho pia kimenikera kwa kuwa tulitegemea ndiye bondia atakayecheza nae,"alisema Mhamila.

Alisema hata hivyo mapungufu yaliyojitokeza kwa bondia wake atayafanyia kazi ili aweze kufanikiwa kuutetea mkanda huo jijini Tanga.

Bondia Robert alipigwa na Godfrey kwa pointi 40-39 ambapo pambano lao lilikuwa la raundi sita. aliongeza kuwa atatumia nafasi ya kumpereka bondia wake tanga na kuamasisha mchezo wa ngumi kupitia DVD zake za Super D Boxing Coach zinazoelekeza mafunzo ya mchezo huo

Sunday, September 25, 2011

NGUMI, KICK BOXING ZAPINGWA DAR ES SALAAM JANA


Mabondia Deo Samuel (kushoto) na Mohamed Matumla wakipambana wakati wa mpambano wao pambano hilo lilitoka droo baara ya kugongana vichwa raundi ya kwanza
bondia Jonas Godfrey akioneshwa ushindi baada ya kumtwanga mpinzani wake Yohana Robart Dar es salaam jana
Kick Boxing Hamisi Mwakinye kulia akilusha teke dhidi ya mpinzani wake Said Mabunda Dar es salaam jana Mwakinye alishinda kwa KO raundi ya kwanza
Pendo Njau kushoto na kanda Kabongo wakiangalia mipambano
Kick Boxing Khalidi Manje kushoto akipambana na Amosi Mwamakula


mabondia chipukizi wakioneshana umaili wa kutupa masumbwi

Thursday, September 22, 2011

KLABU ZA NGUMI ZATAKIWA KUJIANDAA NA MICHUANO YA KAMANDA KOVA

KLABU za ngumi za mkoa wa Pwani na Dar es Salam zimetakiwa kujiandaa vema kwa ajili ya michuano ya ngumi ya kuwania kombe la Kamanda Kova 'Kova Cup' litakalowaniwa Oktoba 24 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam , Katibu Mkuu wa Shirikisho la ngumi za ridhaa nchini (BFT), Makore Mashaga alisema klabu hizo zitakapojitokeza kwa wingi zitatoa changamoto kwa timu ya Taifa ambayo inajiandaa na mashindano mbalimbali ya Kimataifa.

"Kwa sasa mabondia wetu wanaendelea na mazoezi kama kawaida chini ya kocha mkuu Hurtado Primentel ambapo nao watashiriki michuano ya Kova Cup kwa ajili ya kujiweka sawa,"alisema Mashaga.

Alisema michuano hiyo itatoa mabondia mbalimbali kutoka mikoa ya Pwani na Dar es Salaam ambapo watashiriki kama klabu huku kila moja ikiwania kombe hilo ambalo limeandaliwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Suleiman Kova.

Timu hiyo ya Taifa inafanya mazoezi yake katika uwanja wa ndani wa Tafa Dar es Salaam tangu iliporejea nchini kutokea Maputo Msumbiji ilipokuwa ikishiriki Michuano ya Mataifa ya Afrika.

BFT YASAKA MABONDIA WA KUSHIRIKI MICHUANO YA OLIMPIKI

SHIRIKISHO la ngumi za ridhaa nchini (BFT) limeandaa programu kwa ajili ya timu ya Taifa kufuzu kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika London, Uingereza mwakani.

Programu hiyo ya BFT tayari imeanza kwa mabondia wa timu hiyo kufanya mazoezi huku BFT wakishughulikia udhamini kupitia makampuni pamoja na Serikali.

Akizungumza Dar es Salaam , Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema tayari Shirikisho la Ngumi Afrika (AFBA) limetoa ratiba ya mashindano kwa ajili ya nchi wanachama kushiriki ili ziweze kufuzu kucheza michuano hiyo ya Olimpiki.

Mashaga alisema wanatakiwa kucheza mashindano makubwa matatu yanayoandaliwa na AFBA ili Tanzania iweze kushiriki michuano hiyo ya Olimpiki.

"Endapo tungekuwa tumefanya vizuri katika mashindano ya Mataifa ya Afrika 'All Afrca Games' tungekuwa tumejipunguzia mzigo wa kusaka viwango vya kufuzu,"alisema Mashaga.

Kwa mara ya mwisho Tanzania ilifuzu kushiriki michuano ya Olimpiki kwa upande wa ngumi mwaka 2007 lakini hata hivyo bondia wake Emilian Patrick alizuiwa kushiriki michuano hiyo baada ya Tanzania kukumbwa na kashfa ya dawa za kulevya nchini Mautius.

SUPER D , KINYOGOLI WATAMBA BONDIA WAO KUFANYA VIZURI

KOCHA wa bondia Yohana Robart, Rajabu Mhamila 'Super D' ametamba bondia wake kuibuka na ushindi katika pambano lake dhidi ya bondia Mohamed Ndonga litakalofanyika JUMAMOSI  katika ukumbi wa DDC Magomeni.

Pambano hilo ni la maandalizi kwa bondia huyo kutetea mkanda wake wa Oganaizesheni ya Ngumi za KUlipwa (TPBO) litakalofanyika jijini Tanga Septemba 30 mwaka huu ambapo atapambana na Alan Kamote wa jijini Tanga.

Akizungumzia maandalizi ya bondia huyo Super D alisema maandalizi ya bondia huyo ni mazuri na anafanya mazoezi chini ya kambi ya ngumi ya Kinyogoli Foundation.

"Nategemea bondia wangu kuibuka na ushindi katika pambano lake la Septemba la jumamosi, ambalo kwa kiasi kikubwa litamsaidia katika maandalizi yake katika pambano la Tanga ambalo litakuwa la raundi 10,"alisema Super D.

Alisema bondia huyo atapigania uzito wa kg. 60 light weight ambapo katika pambano lake la kesho atapigana raundi sita.

Seper D alisema mapambano hayo ni moja ya muendelezo wa kuendeleza vipaji vya mabondia mbalimbali ambapo amewaomba wadau kujitokeza ili kusaidia juhudi hizo zinazofanywa na kambi ya ngumi ya Ilala.

Monday, September 19, 2011

KASEBA AJIFUA KUMKABILI MTAMBO WA GONGO


Bondia, Japhet Kaseba akifanya mazoezi ya kukaza misuri ya tumbo, kambini kwake Mwanyamala, Dar es salaam jana, Kaseba anajiandaa na mpambano na Maneno Osward litakalofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao



Bondia, Japhet Kaseba akifanya mazoezi ya kukaza misuri ya tumbo, kambini kwake Mwanyamala, Dar es salaam jana, Kaseba anajiandaa na mpambano na Maneno Osward litakalofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao

NGUMI KULINDIMA SONGEA

Mwakyembe kumkabili Onyango

 Na Addolph Bruno

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Benson Mwakyembe  anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na Mkenya Joseph Onyango kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki ambao kwa sasa unashikiliwa na Mwakyembe.

Pambano hilo la kimataifa litakuwa ni la uzito wa kati (Middle Weight) kilogram 72 itakalofanyika Novemba 20 mwaka huu katika uwanja wa Majimaji Mjini Songea.

Akizungumza  Dar es Salaam jana, Mratibu wa Pambano hilo, litachezwa mjini Songea kupanua wigo wa mchezo huo mikoani ambako tayari umeanza kupokelewa na wadau.

Benjamini Chuma alisema limeandaliwa na Kampuni ya Maguaz Investmemt ya Jijini Dar es Salaam ambapo tayari Onyango amethibitisha kuja nchini kupambana na Mwakyembe.

"Maandalizi yanaendelea kufanyika na tayari Mwakyembe ameanza kujifua kambioni kwake Songea., " alisema Chuma na kuwataka watanzania kumsapoti bondia huyo.

Wakati huo huo Chuma alisema kabla ya pambano hilo, bondia Abdallah Mohamed 'Prince Nasim' wa Tanzania anatarajia kupanda ulingoni na Mkenya James Onmyango Oktoba 8 katika ukumbi wa DDC Keko Dar es Salaam.

Chuma alisema pambano lisilo la ubingwa litatanguliwa na mapambano mengine yenye ushindani mkali ambapo bondia Cosmas Cheka wa Morogoro atazichapa na Pinde Shomari wakati Dotto Mstapha ataoneshana kazi na Manti Abuu wote wa Dar es Salaa,.

Sunday, September 18, 2011

BONDIA ROGERS MTAGWA ADUNDWA KWA MARA NYINGINE


Celebrating his 30th birthday as well as Mexican Independence Day, WBC featherweight champion Jhonny Gonzalez (50-7, 44 KOs) scored an impressive second round TKO over Rogers Mtagwa (27-15-2, 19 KOs) on Thursday night at the County Coliseum in El Paso, Texas. After an even round one, Gonzalez opened up in round two and rocked Mtagwa with a series of big shots. The iron-jawed Tanzanian was definitely hurt, but the bout was waved off by referee Guadalupe Garcia before we could see if Mtagwa would have weathered the storm. Time was 2:15.

After the fight, Gonzalez again called out the best of his division. “I want the best, Elio Rojas, Yuriorkis Gamboa, Juan Manuel Lopez and the others at this weight. Thanks El Paso, Viva Mexico!” said Gonzalez. Manager Oswaldo Kuchle added “Tonight Johnny G has been confirmed as one of the best fighters in the world and one of the biggest punchers today. We are very confident of facing the best and winning those fights.”

BONDIA FLOYD MAYWETHER ATAMBIA UBINGWA ALIO NAO

 AKIWA NA MIKANDA YAKE
 FLOYD MAYWETHER ALIPOAMUA KUCHEZA MIELEKA AKIMSULUBU MTU JUKWAANI
MAYWETHER AKIPAMBANA KWENYE MIELEKA

 MAYWETHE AKIWA KATIKA SURA MBALIMBALI
 AKIWA AMEVAA KAMA ROBORT
 MIELEKA

 NANA ATANIWEZA
 MAYWETHER AKIWA AMEBEBEWA MIKANDA YAKE NA  MSANII 50 CENT

Mayweather amtwanga Ortiz KO raundi ya 4,na kutwaa ubingwa WBC

Mayweather amtwanga Ortiz KO raundi ya 4,na kutwaa ubingwa WBC



LAS VEGAS,Marekani

BONDIA Floyd Mayweather Jr.ameendelea kuwa bondia ambaye hajawahi kupigwa, baada ya kumsimamisha mpinzani wake, Victor Ortiz, katika pambano la kuwania ubingwa wa Welter lililofanyika usiku wa kuamkia jana mjini Las Vegas nchini Marekani. .

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Marekani AP, Mayweather aliibuka na ushindi huo, baada ya kumchapa Ortiz, dakika ya 2:59 ya raundi ya nne kwa kumshindilia makonde mfululizo yaliyomfanya mpinzani wake kwenda chini.



Kwa mujibu wa shirika hilo la habari, kisago hicho kilikuja baada ya mabondia hao kutoka mapumziko ambapo Ortiz alimfuata moja kwa moja Mayweather katikati ya ulingo na baada ya kugonganisha mikono, Mayweather aliachia konde la mkono wa kushoto na kufuatiwa na la mkono wa kulia ambayo yalimfanya Ortiz kuanguka chini.

AP ilieleza kuwa baada ya Ortiz kuanguka chini alijaribu kunyanyuka kwa shida lakini mwamuzi, Joe Cortez, akaamua kumaliza pambano.

“Tuligonganisha glove na tukawa tayari kupambana na baadaye nikaachia konde la mkono wa kushoto na kulia,” alisema Mayweather. “Ulingoni unapaswa kujilinda mwenyewe muda wote,”aliongeza bondia huyo.

Hata hivyo kabla ya pambano hilo kumalizika, raundi hiyo ilionekana kuwa tayari na utata, baada ya Ortiz,kumpiga kichwa makusudi Mayweather jambo ambalo lilimfanya aonywe na mwamuzi Cortez,lakini baada ya hapo Ortiz akaenda kumbusu Mayweather juu ya shavu.

KASEBA KUMVAA MTAMBO WA GONGO



BONDIA Japheth Kaseba anajiandaa kupanda ulingoni dhidi ya Maneno Osward pambano lisilo la ubingwa litakalochezwa Oktoba Mosi Mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana,mmoja wa mabondia hao, Kaseba alisema litachezwa kati ya ukumbi wa Travertine Magomeni au DDC Mlimani ambapo litasimamiwa na Shirikisho la Ngumi za kulipwa Tanzania (PST).

Alisema pambano hilo ni ra raundi 10 uzito wa kati kilogramu 72 ambapo ni mara ya kwanza kwa mabondia hao kutwangana.

"Tupo katika maandalizi na hili limeandaliwa na mdau mmoja wa ngumi anayefahamika kwa jina la Gervas Mganda kwa kushirikiana na PST (Shirikisho la Ngumi za kulipwa Tanzania).," alisema

Alisema "nipo katika mazoezi kama ilivyo kawaida katika kambi yangu, wadau tunawaomba wajiandae kushuhudia pambano hili, lengo kuendeleza rekodi zetu na kuwapa burudani mashabiki.," alisema Kaseba.

Mbali na pambano hilo Kaseba amewahi kupambana na bondia Ernest Bujiku, Fransis Cheka, na Mada Maugo ambapo ameshinda moja kati ya hayo dhidui ya Bujiku.

Thursday, September 15, 2011

Khan aombea Ortiz apigwe



Khan aombea Ortiz apigwe
na Mayweather

LONDON, Uingereza
AMIR Khan hataki rafiki yake Victor Ortiz ampige Floyd Mayweather Junior kesho kwa kuwa anataka kupiga na mbabe huyo.

Ortiz atapiugana na Mayweather mjini Las Vegas keszho na Khan anataka ‘Pretty Boy’ abakie kuwa bondia asiyepigwa hadia yeye atakapopambana naye k0atika mechi ainayotaraj iwa kuchezwa Agosti mwakani.

Victor ni mpiganaji mzuri, lakini sipendi ashinde,” alisema bingwa wa WBA na IBF uzani light-welter n kukaririwa na Daily Mirror.

"Ninataka kwua wa kwanza kupigana naye na kumshinda."

Sioni kama Ortiz atashinda, ingawa ana nguzu zaidi, Mayweather ana uzoefu zaidi na ufundi.”

BONDIA KALAMA NYILAWILA ATAFUTA PROMOTA KWA AJILI YA KUPAMBANA NA CHEKA


BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Kalama Nyilawila amesema kwa sasa ameanza mchakato wa kutafuta promota kwa ajili ya kumuandalia pambano dhidi ya francis Cheka ili aweze kutetea ubiungwa wake wa WBO.

Akizungumza na majira jana, Kalama alisema, kutokana na malengo yake ya kutaka mkanda huo ubaki hapa nchini hivyo alionelea kucheza na Cheka kutokana na kuwa na uwezo mkubwa na hasa mchezo mzuri aliouonyesha katika pambano lao la marudiano dhidi yake na Mada Maugo kwa kumtandika na kumzidi tofauti ya pointi.

Alisema, kwa sasa ameishaanza kusaka promota ambapo bado wapo katika mazungumzo ya awali ambapo watakapoa afikiana ndipo watapanga tarehe halisi ya kufanya pambano hilo ikiwa ni pamoja na mahali.
"Kama nilivyosema sitaki mkanda huu utoke nje hivyo nikifanikiwa kucheza na Cheka itakuwa faraja kwangu kwani najua uwezo wake na hata anatambulika Duniani hivyo haitakuwa vibaya kwani naye alishawahi kucheza mapambano ya Kimataifa," alisema Kalama.
Aliongeza kuwa wakati wa yeye kutetea ubingwa huo umefika ambapo akishindwa kucheza na bondia wa hapa nchini anatakiwa kutafuta pambano la nje ya nchi ili kuweza kutetea ubingwa huo kiyu ambacho yeye hakitaki lakini ikishindikana kupata pambano hilo itabidi atafute pambano la nje.

Wednesday, September 14, 2011

ISSA SEWE AJIFUA KUMKABIRI RAMADHANI SHAULI

 Kocha Mkongwe wa mchezo wa ngumi Nchini Habibu Kinyogoli'Masta' (kushoto) akimwelekeza jinsi ya kutupa masumbwi bondia, Issa Sewe wakati wa maoezi yanayorndelea ya kambi ya Ilala Sewe atapambana na Ramadhani Shauli mwishoni mwa mwezi ujao.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)