FOR IMMEDIATE RELEASE – Saturday April 6th, 2013
-Dar-Es-Salaam - Ziara ya Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya
Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi, imeiweka nchi ya Botswana
mahali pazuri kwa kuiingiza kwenye kundi la nchi nane (8) za Afrika
zitakazofaidika na progra
mu ya “IBF ya Utalii wa Michezo”.
Akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari pamoja na wadau wa
michezo alipokuwa anahitimisha ziara yake iliyomchukua kwenye majiji ya
Francistown na Gaborone, Rais Ngowi aliweka bayana furaha yake kwa jinsi
serikali ya Botswana kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BNSC) ilivyompa
mapokezi mazuri.
Ngowi aliitembelea Botswana kuanzia tarehe 31 Machi mpaka tarehe 5
April ambapo aliweza kutembelea majiji mawili ya Francistown na Gaborone. Aidha,
Ngowi aliitembelea pia miji midogo ya Molopolole,Kanye, Kang, Jwaneng na
Ghanzi.
Katika miji midogo ya Ghanzi na Kanye Ngowi alijionea jinsi
Botswana inavyotunza na kuendeleza vivutio vya kitalii na hivyo kuweza kujipatia
pesa nyingi za kigeni kutoka kwa watalii wanaotembelea nchi
hiyo!
Programu ya “IBF ya Utalii wa Michezo” itaifanya
Botswana kufaidika na ujio wa watalii kutoka nchi zaidi ya 144 ambazo ni
wanachama wa IBF. Pia kutakuwa na wawekezaji watakaowekeza kwenye vivutio
mbalimbali na kuifanya Botswana kuwa moja ya nchi zinazofaidika na
“Utalii wa Michezo”(Sports Tourism).
Rais Ngowi aliishauri serikali ya Botswana umuhimu wa kuwekeza
kwenye sekta ya michezo hususan mchezo wa ngumi na kutoa mfano wa namna nchi
zinavyotumia mabilioni ya dola za Kimarekani kuandaa michezo ya kimataifa kama
vile michezo ya Olimpiki na Kombe la Dunia.
Katika hotuba yake
rasmi (Key Note Speech) aliyoitoa kwenye ukumbi wa Chama Cha Mpira wa Miguu cha
Botswana (BFA), Ngowi alieleza jinsi bondia mmoja anavyoweza kuitangaza nchi kwa
kiasi kikubwa na kumtolea mfano bondia wa Botswana Lesley
Sekotswe ambaye aliiwakilisha nchi vizuri alipopambana na bondia
Immanuel Naidjala wa Namibia hivi karibuni.
Nalo Barala la Michezo la
Botswana BNSC limemhakikishia Ngowi kuwa litafanya kila liwezalo
kuuendeleza mchezo wa ngumi ambao ndio unaoitangaza vyema Botswana kwenye medani
ya kimataifa. Mwenyekiti wa BNSC bwana Solly Reikeletseng
pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa BNSC bwana Perscy
Raditladi walitoa ahadi ya kushirikiana na IBF katika kuuendeleza
mchezo wa ngumi kwa kiwango ha kimataifa.
Ngowi alimaliza ziara yake nchini Botswana jana siku ya Ijumaa na
kuelekea nchini Afrika ya Kusini ambako atakuwa na ziara ya siku nne itakayoisha
tareeh 9 April. Akiwa nchini Afrika ya Kusini Ngowi atafanya
mazungumzo ya serikali ya nchi hiyo hususan serikali ya jimbo la
Mpumalanga ambalo limekuwa likidhamini mapambano mengi ya
ngumi.
Mwishini mwa April Ngowi atafanya ziara nyingine katika nchi za
Ghana, Cameroon, Misri na Tunisia kujenga uwezo wan chi hizo
katika kuitumia programu ya “IBF ya
Utalii wa Michezo” (IBF Sports Tourism)
Picha 1: Ngowi
akihutubia katika ukumbi wa BFA jijini Gaboone, Botswana!
Picha 2: Ngowi akiwa amesimama na wadau mbalimbali
wa Ngumi wakiufurahia mkanda wa IBF wa
Kimataifa.
Picha 3: Ngowi
akiwa amesimama na Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la Almasi la
Botswana DEBTSWANA Bi. Lesedi Rakola katika mkutano huo.
IMETOLEWA
NA:
INTERNATIONAL
BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM,
TANZANIA
Benjamin
William Mkapa Pension Towers
Tower B,
Mezzanine Floor, Azikiwe Street
Dar-Es-Salaam - Tanzania
No comments:
Post a Comment