Tangazo

Pages

Wednesday, April 17, 2013

MASHINDANO YA NGUMI TEMEKE YANAENDELEA BILA WADHAMINI

 Na Mwandishi Wetu

Bondia Athumani Yanga wa timu ya Ashanti Boxing ya Ilala
MASHINDANO ya klabu  bingwa ya Mkoa wa Temeke yameanza jana jijini, Dar es Salaam huku
yakishirikisha timu 20 na yanatarajiwa kufikia tamati  Aprili 19 mwaka huu.
 
Lengo la mashindano hayo yaliyoanza jana ni kuinua vipaji vya mabondia chipukizi na kupata vipaji bora watakaokuwa chachu ya maendeleo ya mchezo nchini.
 
Kocha wa kimataifa wa mchezo huo nchini Rajabu Mhamila 'Super D' alisema vijana wanakaoshiriki mashindano hayo walipima uzito katika Ukumbi wa CCM Kata ya 15, Temeke Dar es Salaam.
 
Super D ambaye pia ni kocha wa timu ya Mkoa wa Ilala ambao ni waalikwa katika michuano hiyo alisema vijana wake kutoka klabu ya Amana na Ashanti watafanya vema katika mashindano hayo.
 
Mkoa wangu umetoa vijana sita ambao naamini watafanya vizuri katika mashindano hayo na kutoa upinzania mkubwa ambao utakuwa chachu ya maendeleo ya mchezo huo nchini.
Super D aliwataja baadhi ya mabondia hawo kuwa ni Hussein Mawimbi na Said Hamisi kutoka klabu ya Amana na Athumani Yanga pamoja na Said Mabunda kutoka klabu ya Ashanti.
 
Pia aliwaomba wadau kujitokeza kusaidia mashindano hayo yanayofanyika katika ukumbi wa CCM Kata ya 15, Temeke ili kuhakikisha hamasa ya kuendeleza mchezo huo inapatikana yatakayofanikisha mafanikio ambalo ndilo lengo kubwa. la mashindano hayo

Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa
katika mchezo huo kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis  Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe. na Francis Cheka dhidi ya Japhet Kaseba mapambano yote mawili mbali na hivyo atakuwa akisambaza vifaa vya mchezo wa masumbwi kwa mabondia ambao awana wanaweza kumuona na kujipatia vifaa mbalimbali

No comments:

Post a Comment