Tangazo

Pages

Monday, April 1, 2013

MSHINDI KATI YA ISSA OMAR NA MADILU KUCHEZA UFILIPINO

Mshindi  na ambae atakuwa bingwa mpya  wa Universal Boxing Organization uzito wa light fly kati ya Issa omar(peche boy)  na Shaban Madilu amepata shavu la kucheza  may 18  na lienel legada ambae ni bondia bingwa  wa ufilipino.Pambano litakalo fanyaka katika mji wa Dumaguete City, Negros Oriental  nchini philipines . Ofa hiyo imekuja baada ya vyama vya ngumi kupitia record zao na kuwashauri  mabondia hao kucheza ubingwa wa UBO(Universal Boxing Organization) ambao nao pia upo wazi kutokana na bingwa aliepita kutoutetea kwa kipindi kirefu. UBO kupitia mwakilishi wao kanda ya Africa mashariki ndg Emmanuel  Mlundwa  imekubali pia kudhamini pambano hilo kwa kutoa  ubingwa huo kwa mabondia wawili toka nchi moja yaani Tanzania kugombania ubingwa huo. Nafasi ambazo ni chache sana kutokea bahati kama hiyo, pindi itakuwa na  muda mfupi wa kuutete ubingwa huo kwa ofa hiyo ya ufilipino ambayo itakuwa na  ukishirikishwa  wa ubingwa wa PAN PACIFIC lightfly weight title nchini ufilipino mwishoni mwa mwezi ujao kulingana hali ya bondia na matokeo ya mpambano wa tarehe 7 april utakao fanyika katika ukumbi wa  ccm mwinjuma-mwananyamala. Ni mpambano ambao pia utawakutanisha mabondia wengi wakongwe na chipukizi
 

IBRAHIM KAMWE
Director - Bigright promotion 
 owner of bigright boxing Gym

No comments:

Post a Comment