Tangazo

Pages

Tuesday, December 11, 2012

MBWANA MATUMLA: CHEKA, MIYEYUSHO YAWEZA KUWA WANATUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU



 FRANCIS CHEKA RIGHT AND DANIEL WANYONYI KENYA.

Miyeyusho kulia akimuadhibu Nassib jana


Mbwana
BINGWA wa zamani wa dunia wa WBU, Mbwana Matumla ‘Golden Boy’, amesema ana wasiwasi Francis Miyeyusho na Francis Cheka wanatumia daw za kuongeza nguvu, zinazopigwa marufuku michezoni.
Akizungumza  jana, Golden Boy alisema kwamba umefika wakati Tanzania kuwe na utaratibu wa kuwapima mabondia kabla na baada ya michezo, kwani inawezekana kutokuwa na utaratibu huo kukatoa mwanya kwa mabondia wengine kutumia dawa hizo.
“Mimi nilipigana na Francis, kweli alinipiga, ila nilipata wasiwasi sana juu ya nguzu zake, kwa kweli hazikuwa za kawaida, sisemi kwamba anatumia, inawezekana ni uwezo wake, lakini nasema nina wasiwasi, yeye na Francis Cheka wanatumia hizo dawa,”alisema Mbwana.
Golden Boy alipigwa na Miyeyusho Oktoba 30, mwaka jana ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, kwa pointi, jaji Omari Yazidu akitoa 113-114, Said Chaku 110-117 na Jalus Lugongo 109-118.
Katika pambano hilo, Francis Miyeyusho alienda chini raundi ya pili, wakati Mbwana Matumla alidondoka raundi ya pili na ya nane na hilo ndilo lilikuwa pambano la mwisho la Golden Boy hadi sasa.
Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ jana aliendeleza ubabe wake , baada ya kufanikiwa kutetea taji lake la WBF uzito wa Bantam, kwa kumpiga Nassib Ramadhan kwa Techinical Knockout (TKO) raundi ya 10 kwenye ukumbi wa PTA, Saba Saba, Temeke mjini Dar es Salaam usiku huu.
Nassib alionekana kuishiwa pumzi tangu raundi ya nane, lakini alijikongoja kutaka kumaliza raundi 12 za pambano hilo, ila kwa bahati mbaya, safari ikaishia raundi ya 10.
Hata hivyo, Nassib bondia kutoka Mabibo, Dar es Salaam, alilianza vizuri pambano hilo akimsukumia mpinzani wake makonde mazito yaliyoonekana kumyumbisha.
Naasib aliendelea kutawala pambano hadi raundi ya sita, ila baada ya hapo, mwelekeo wa pambano ulianza kubadilika taratibu, Chichi, Mtoto wa Kinondoni akianza kumuadhibu mpinzani wake kwa makonde yake yaliyoshiba uzito.
Nassib alijitahidi mara moja moja kujibu, lakini zaidi alitumia ujanja wa kumkumbatia Chichi ili kumpunguza kasi.
Hata hivyo, Nassib hakushindwa kwa kupigwa ngumi, bali aliishiwa pumzi jambo ambalo linaashiria kijana huyo ni bondia imara na anaweza kuwa mpinzani wa kweli wa Chichi Mawe.
Kwa ujumla lilikuwa pambano zuri ambalo kwa muda mrefu halijapatikana katika ardhi ya Tanzania- mabondia walikuwa wakipigana, hakukuwa na ujanja ujanja. Wote ni mafundi na mamia waliohudhuria pambano hilo, waliburudika kwa mchezo mzuri.
Katika mapambano ya awali, Deo Samuel alitoka sare na Freddy Sayuni, Mohamed Matumla alimpiga kwa Knockout (KO) raundi ya pili Deo Miyeyusho, Fadhil Majiha alimpiga kwa pointi Juma Fundi na Ibrahim Classic ' King Class Mawe' alimpiga kwa pointi Said Mundi.
Mgeni rasmi, Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara alimvalisha mkanda wa ubingwa Miyeyusho baada ya pambano hilo, lililohudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’

No comments:

Post a Comment