Mabondia
Francis Cheka (kushoto) na Chiokta Chimwemwe wakiwa wameshika mkanda
watakaougombea muda mchache ujao jijini Arusha leo, wakati wa
utambulisho wao na zoezi la kupima uzito.
Bondia Francis Cheka akipima uzito
.
Bondia Chiokta Chimwemwe akipima uzito.
Mabondia Francis Cheka (kushoto) na Chiotcha Chimwemwe, kupigana baada ya kupima uzito na kucheki afya leo asubuhi.
***************************************
Mafahali
mawili wanaotegemea kuzichapa tarehe 26, 2012 kugombea mkanda wa IBF
katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania
Francis Cheka na Mmalawi Chiotcha Chimwemwe nusura wazichape kavukavu
wakati wa upimaji uzito na mkutano wa waandishi wa habari katika hoteli
ya nyota 5 yaNaura Springs, jijini Arusha jana tarehe 25 Desemba 2012.
Hii
ni mara ya kwanza kwa ngumi za kulipwa kupewa hadhi kubwa kama hiyo ya
kuwekwa kwenye hoteli ya nyota tano (5) hapa Tanzania.
Wawili
hao walikuwa katika hoteli hiyo ya kifahari ya Naura Springs
inayomilikiwa na bwana Felix Mrema anayemiliki mahoteli lukuki katika
jiji la Arusha na Moshi ambazo ni Naura Springs Hotel, Impala Hotel,
Ngurudito Hotel, Impala Moshi na Livingstone Hotel za Moshi!
Mpambano huo uliopewa jina la “Vurumaini chini ya Mlima Meru”umekuwa
ni gumzo katika jiji la Arusha, Moshi, Tanga, Dodoma, Manyara pamoja na
nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda na unaandaliwa na
kampuni ya kizalendo ya Green Hills (T) Limited inayomilikiwa na bondia
wa zamani wa taifa katika ngumi za ridhaa na kuloipwa George Andrew na
familia yake.
Aidha,
watalii wengi walioko katika jiji la Arusha wakati huu wa sikukuu ya
Xmas wameonyesha nia zao za kuliangalia pambano hili na wengine
wameshakata tiketi tayari kuingia katika ujwanja wa Sheik Amri Abeid
kuwashughudia mafahali hao wawili wakitoana jasho.
Chiotcha
mwana wa Chimwemwe mwanajeshi wa ngazi ya Luteini Usu katika jeshi la
Malawi amepania kulibeba juu taifa lake lililoko pembezoni mwa ziwa
Nyasa kwa kumwonyesha Francis Cheka kuwa ngumi zinaendana na ushupavu.
Chimwemwe
anadai kuwa hakuja Tanzania kutalii kama walivyo watalii wengine bali
alikuja kuwakilisha nchi yake aipendayo ya Malawi na kurudi kwao na
mshipi wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya
Kati. Alisema kuwa kushinda kwake sio kitu cha kubahatisha ila ni
uhakika.
Naye
Francis mwana wa Cheka, Mtanzania aliyeipeperusha vyama bendera ya
taifa hili katika mapambano mengi bila kuzivunja nyoyo za mashabiki wa
ngumi nchini alisema kuwa “Mwache Mmalawi huyo ajifurahishe tu kwani hajui kinachongojea ulingoni”
Cheka
aliyejizolea sifa kemkem kati ya mabondia wa kitanzania aliendelea
kusema kuwa yeye sio mzungumzaji sana ila ngumi zake ndizo
zitakazozungumza siku ya tareeh 26 Desemba, 2012.
“Asifikirie kuwa ngumi ni kupiga makelele tu na ukashinfa” alisema Chelka akimwangalia Chimwemwe wakati alipokuwa anajigamba kwa sifa kemkem!
Mpambano
huo wa kukata na shoka unakuja wakati ambako Arusha imekuwa ni jiji na
linataka kutumia mapambano mengi ya ngumi ya kimataifa kukuza hadhi ya
jiji hilo kama “Geneva ya Afrika” kutokana na mandari yake na mikutano mingi ya kimataifa inayofanyika katika jiji hili.
Francis
Cheka anakutana na Chimwemwe baada ya kuutema mkanda wake wa IBF wakati
alipokutana na Karama Nyilawila kugombea mkanda mwingine mbali na IBF
hivyo kuupoteza ubingwa wa IBF. Cheka amepania kuuchukua tena mshipi huo
na kuudhihirishia ulimwengu kuwa yeye kweli ni moto wa kuotea mbali!
Mpambano
huo utahudhuriwa na viongozi wengi wakiongozwa na Meya wa jiji la
Arusha Mstahiki Gaudence Lyimo pamoja na wageni wengi wanaofanya kazi
kwenye mashirika kadhaa ya kimataifa ikiwa ni pamoja na mahakama ya
kimataifa ya wahalifu wa kivita wa Rwanda, Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki na Kati, ILO, UNICEF, WFP na nyingine nyingi.
Aidha watalii wengi wameacha kwenda mbugani siku ya pambano ili washughudie wenyewe ni nani zaidi kati ya Cheka na Chimwemwe.,
Pamabano
hilo linaratibiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) chini
ya Rais wake Onesmo Ngowi na kupewa baraka zote na Shirikisho la Ngumi
la Kimataifa (IBF).
Waamuzi wa pambano ni:
Onesmo Ngowi - Kamishna Mkuu, Roman Chuwa ambaye ndiye Kamishna wa TPBC mkoa wa Arusha –(Kamishna Mkuu Msaidizi), Nemes Kavishe (Refarii), Boniface Wambura – (Jaji), Gallous Ligongo –(Jaji), Mark Hatia –(Jaji).