Tangazo

Pages

Monday, July 16, 2012

RASHIDI MATUMLA ASHINDWA KUTAMBA MBELE YA BENJAMINI SIMONI WA UJERUMANI


BONDIA Rashid ‘Snake Man’ Matumla juzi alipigwa kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya nne na Benjamin Simon wa Ujerumani, katika pambano lililokuwa la raundi 12, la kuwania taji la IBF, uzito wa Super Middle lililofanyika kwenye ukumbi wa Universal, Berlin, Ujerumani. Hilo lilikuwa pambano la pili kuwakutanisha mabondia hao, awali Matumla alishindwa kwa pointi, ila juzi ‘alipotea mapema’. Matumla alitafutiwa mechi hiyo na bondia maarufu wa zamani nchini, Ally Bakari ‘Champion’ kwa kushirikiana na African Camp Promotion ya Nairobi, Kenya, chini ya Mkurugenzi wake, Thomas Mutua. Matumla anarejea nchini kesho. Pichani ni refa Jean Pierre akimuinua juu mkono Benjamin kumtangaza mshindi dhidi ya Matumla kushoto.  

No comments:

Post a Comment