Thursday, June 17, 2021
Friday, March 12, 2021
BONDIA JONAS SEGE NA TWAHA KIDUKU KUPANDA ULINGO MMOJA MARCH 19 NA MABONDIA WA MATAIFA MENGINE
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Jonas Segu 'Black Mamba' ametamba kumpiga mpinzani wake Hanock Phili kutoka Malawi akizungumza mbele ya wahandishi wa habari kusiana na mpambano wake uho utakaofanyika March 19 katika ukumbi wa Ubungo Plaza
Segu amesema kuwa yeye alienda nchini Africa ya kusini na kuhishi uko kwa ajili ya mchezo wa ngumi na kufanikiwa kuchukuwa ubingwa wa WBF ambao ata utetea siku hiyo ata hivyo amekuwa apati mapambano ya ndani kutokana na mabondia wengi kumkwepa baada ya kutembeza kipigo kwa mabondia kadhaa wa Tanzania
ambapo alishawai kumchapa Habibu Pengo Idd Pialali na alifanikiwa kumchapa Mfaume Mfaume ata hivyo kutokana na Figisu majaji wakatoa Droo sasa nimeruni nchini Tanzania na mpambano huu ndio utakuwa wa kwanza kwangu kucheza baada ya miaka mitano iliyopita ambapo sijacheza katika ardhi ya Tanzania naomba mashabiki wa ngumi morogoro dar es salaam pwani Tanga na mikoa mingine yote waje kuona ngumi ambazo zenye radha na manufaa katika mchezo huu wa tarehe 19 march
nae promota wa mpambano huo Evalist Elnest 'Mopao' amesema mbali na mpambano huo kutakuwa pia na mpambano wa Twaha Kiduku na Tishibangu Kayembe wa Kongo na mpambano wa kina dada utakao wakutanisha Najma Isike na Halima Bandola pia kutakuwa na takribani jumla ya mapambano nane tu kwa siku hiyo
hivyo naomba wapenzi wa ngumi waje mapema kuangalia ngumi nzuri zilizo andaliwa vema kabisa kwa galama nafuu kabisa
Thursday, February 18, 2021
BONDIA JEMS KIBAZANGE AMTILIA MKWALA MZITO HAMIDU KWATA WATAZIPIGA APRIL 2 P.T.A SABA SABA
![]() |
| JEMS KIBAZANGE 'DOG LA KIVITA' |
BONDIA Jems Kibazange 'Dog la Kivita' ameapa kuwa lazima amsambalatishe Hamidu Kwata ifikapo April 2 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba mpambano uho uliopewa jina la 'No Pain No Gain Nigth Fight' kuwa ana uwakika wa kumchakaza Kwata kama mfuko wa mazoezi
akizungumza wakati wa mazoezi yake katika GYM, ya kocha Maneno iliyopo Manzese Midizini amesema kuwa mimi ndio kiboko ya mbwa koko na kwata ajakutana na viama mimi nimesha wapiga mabondia wote waliopo katika uzito wangu ndio
mana natamba na kwa Tanzania hii mimi sina mpinzani kwani mabondia wote kwangu ni viande nashangaa huyu amekubali vipi kupigana na mimi
naisi njaa tu inamsumbua hivyo naona pesa zake atakazo zipata zitaisha katika matibabu yake kwa kuwa nitampiga bila ya huruma kwani mimi ni kamanda katika mchezo huu wa masumbwi na akuna mtu asiejua uwezo wangu niwapo ulingoni
nakuwa mtu mwingine kabisa ndio mana mtaani kwetu wananita Dog la Kivita na vita hii itaenda kumwangamiza Kwata na kumsababishia kilema cha maisha kwani ngumi ni mchezo wangu nilio uwekea nadhiri ya kuendesha maisha yangu hivyo sito kubali bondia mdogo kama huyu aje kuniaribia kiraisi tu
Nae Promota wa Mpambano Uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia
Wednesday, February 17, 2021
SUPER D AWASAINISHA MABONDIA MAONO ALLY KUZIPIGA NA MESHACK MWANKEMWA APRIL 2
BONDIA Maono Ally kutoka Bagamoyo mkoa wa Pwani amesaini mkataba wa kuzipiga na Meshack Mwankemwa kutoka Mbeya mpambano utakaofanyika April 2 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba mpambano wa raundi kumi uzito wa kg69 kutafuta nani zaidi kati yao
mpambano uliopewa jina la No Pain No Gain Fight Night mabondia hawo watazipiga siku hiyo katika mpambano ulio andaliwa na kiampuni Tanzu ya Kizarendo ya Super D Boxing Promotion
Maono amesema kuwa katika mpambano uho atokuwa na msalia mtume kwani ngumi kwake ni kazi kwa kuwa mabondia wengi wamekuwa wakimkimbia pindi wanapo pangiwa mapambano na yeye hivyo Mwankemwa akae tayari kwa kipigo tu
Na afanye mazoezi ili apunguziwe kipigo ingawa kipigo kipo pale pale nitampiga mwankemwa kama mfuko wa mazoezi kwani nimejiandaa vya kutosha na sina wasiwasi na pambano hilo
kwa upande wa Mwankemwa amesema asnashukuru kupata mpambano uho utakaofanyika Dar hivyo nipo vizuri na nategemea ushindi ambao sito washirikisha majaji ambapo nitampiga K,O mbaya sana aikuwai kutokea
Nae Promota wa Mpambano Uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia
vicent Mbilinyi vs Deo samweli rd 10Ramadhani Mbegu "Migwede" vs Albano Clement Rd 84.Daudi Mwita vs Abdul Ubaya Rd 65. Hamidu kwata vs James kibazange 10 rd6.Mustafa Khalidi vs Mrisho mzezele rd 67.kassim Ahmad vs Gabriel Chola rd 88.Juma Abdul vs Hamza Mchanjo rd69.Veronika Thomas vs Fatima Yazidu rd610.Frank Lucian vs Juma Kaiza rd8pia kutakuwa na burudani mbalimbali kwa ajili ya kusapoti mchezo uho utakao kuwa siku ya Ijumaa kuu ya Pasaka
Tuesday, February 9, 2021
SUPER D AMSAINISHA DEO SAMWELI KUZIPIGA NA VICENTI MBILINYI APRIL 2 P.T.A SABA SABA
BONDIA DEO SAMWELI amesaini mkataba wa kuzipiga na Vicenti Mbilinyi mpambano wa raundi kumi kumi utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Saba saba siku ya Ijumaa Kuu April 2
Akisaini mkataba uho mbele ya mkurugenzi wa kampuni Tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa amekuja kufanya kazi hivyo mashabiki waje kwa wingi kwani kazi atakayo ifanya siku hiyo si ya kitoto
aliongeza kwa kuserma kwa sasa anarudi upya katika masumbwi kwani mwishoni mwa mwaka jana alijeruhiwa kidogo hivyo ame mtahadharisha mbilinyi kufanya mazoezi kweli kweli kwani siku hiyo akuto kuwa na msalie mtume
Katika mpambano uho atampiga kipigo cha mwana ukome ambapo mbilinyi ato weza tena kumtaka Deo Samweli warudiane nae tena
Nae Promota wa mpambano uho Super D amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na burudani ya masumbwi ni vitasa kwa kwenda mbele katika mpambano uliopewa jina la 'No Pain No Gain Fight Nigth'
pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ya mabondia mbalimbali ambapo Jemsi Kibazange atazipiga na Hamidu Kwata wakati kassim ahamdi atazidunda na Gabriel Chola na Ramadhani Migwede atazichapa na Albano Clement na mpambano mwingine wa kutisha utakuwa kati ya Maono Ally kutoka bagamoyo atazipiga na Meshacki Mwankemwa kutoka Mbeya na Abdul Ubaya kutoka Mlandizi atazidunda na Daudi Mwita wa Dar
Saturday, January 9, 2021
BONDIA AMOSI MWAMAKULA KURUDI KIVINGINE KUZIPIGA FEB 6
Kocha wa mchezo wa masumbwi na mateke /kicki Boxing Esmail Abdallah 'Van Dame' kushoto akimtambulisha bondia Amosi Mwamakula kwa ajili ya mpambanmo wake wa kuzipiga Feb 6 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba na Hashimu Kilaga
Na Mwandishi Wetu
BONDIA AMOSI MWAMAKULA ametambulisha mpambano wake wa kuzipiga na Hashimu Kilaga mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Saba saba SIKU YA FEB 6 Dar es salaam
akizungumza na waandishi wa habari juu ya mpambano uho kocha wa masumbwi na Mateke Kicki Boxing Esmail Abdallah 'Van Dame' amesema kuwa mwamakula amejiandaa vya kutosha hivyo mpinzani wake nae ajiandae vya kutosha kwani kwa sasa amerudi kivingine
ameongeza kwa kusema kwa sasa wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya pambano hilo ambalo linandaliwa kwa ubora wa aina yake kwani maandalizi ya mpambano uho sasa yamepamba moto
alieleza kuwa mbali na pambano hilo la masumbwi pia kutakuwa na mapambano mengine ya ngumi ambapo bondia Lulu Kayage atazipiga na Agnes Kayange na Jitu Rajabu kutoka kwa Super D Coach atazipiga na Daniel Mwakafyale na Shabani kaoneka atazipiga na Butel Obedi mambano huo unaletwa na Jamukaya kwa kushilikiana na Black Panda utakuwa na kingilio cha shilingi 10,000 TU kwa siku hiyo
pia kutakuwa na ngumi za mateke kick Boxing na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri wa Sanaa Michezo Na Utamaduni
Friday, January 1, 2021
SUPER D BOXING PROMOTIOBN KUMRUDISHA HAMISI MAYA ULINGONI APRIL 2 SABASABA
BONDIA HAMISI MAYA
Hamisi Maya ambaye ni bingwa wa GBC mkanda unaotambulika Duniani akwa amevalishwa mkanda baada ya kumdunda Piergiulio Ruhe wa ujerumani na kufanikiwa kurudi na mkanda
NA MWANDISHI WETU
BONDIA HAMISI MAYA sasa kupanda ulingoni rasmi April 2 katika ukumbi wa Sabasaba Hall uliopo katika viwanja vya Sabasaba akimvaa bondia Alvin Omondi wa Kenya mpambano wa Raundi 8 utakaopigwa katika uzito wa KG 66
Akizungumza kuusu mpambano uho Mratibu wa pambano hilo Chaurembo Palasa amesema kuwa baada ya muda mrefu kukaa kimya kwa bondia huyo sasa anaibuliwa upya na kampuni tanzu ya kizarendo ya Super D Boxing Promotion ambao ndio waandaaji wa mpambano uho kwa sasa
Hamisi Maya ambaye ni bingwa wa GBC mkanda unaotambulika Duniani ambapo mpaka sasa anasifika kwa kuwapiga mabondia mbalimbali akiwa nje ya nchi ambapo alishawai kumpiga K,O mbaya sana Jems Onyango wa Kenya mpambano uliofanyika Charter Hall, Nairobi Kenya na kurudi na ubingwa wa Afrika na kumgalagaza bila ya huruma bondia Piergiulio Ruhe wa ujerumani na kufanikiwa kurudi na mkanda
Alisema Palasa ata hivyo mapromota wengi wamekuwa wakimkwepa Maya kutokana na uchezaji wake awapo ulingoni ni kama bondia aliyekusudia kuuwa mtu akiwa mchezoni ndio mana ajapata mapambano tangu mwaka 2019 hata hivyo kupitia kampuni yetu ya Super D Promotion tunampa nafasi ya kuonesha Kipaji chake kwa mara nyingine kwa mwaka uhu 2021
aliongeza kwa kusema kuwa mbali na mpambano uho pia kutakuwa na mapambano mengine ya lkukata na shoka ambapo bondia machachali awapo ulingoni Vicent Mbilinyi atazipiga na George Onyango na Fransic Miyeyusho atazipiga na Gabriel Chola wakati Hamidu Kwata atazidunda na Jems Kibazange na juma Abdul wataoneshana kazi na Hamza Mchanjo na Bakari Magona atazipiga na Emanuel Mwakyembe





