Tangazo

Pages

Wednesday, January 20, 2016

MABONDIA SADIQ MOMBA NA BAINA M,AZOLA WASAINI KUZIPIGA MARCH 5 TASUBA BAGAMOYO

Mabondia Sadiq Momba kushoto wakitambiana na Baina Mazola baada ya kutia saini ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa pwani katikati ni promota Muhusin Sharif Picha na SUPER D BOXING NEWS

Promota wa mchezo wa masumbwi Muhusin Shsharif katikati akiwa pamoja na mabondia Sadiq Momba kushoto na Baina Mazola mara baada ya mabondia hawo kutiliana saini ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani Picha na SUPER D BOXING NEWS
KIONGOZI TOKA SHIRIKISHO LA MASUMBWI PST PEMBE NDAVA KATIKATI AKISAINI MKATABA WA KUKUBALI KUPIGANA BONDIA BAINA MAZOLA KUSHOTO NA KULIA NI PROMOTA MUHUSINI SHARIFU


Promota wa masumbwi nchini Muhusini Sharif Katyikati akiwainuwa mikono juu mabondia Sadiq Momba kushoto na Baina Mazola wakati wa kutambulisha mpambano wao utakaofanyika katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani Picha na SUPER D BOXING NEWS
BONDIA SADIQ MOBA AKITIA SAIN YA KUZIPIGA NA BAINA MAZOLA MARCH 5 KATIKA UKUMBI WA TASUBA BAGAMOYO MKOA WA PWANI WANAOSHUDIA KULIA NI PROMOTA MUHUSINI SHARIFU NA KIONGOZI TOKA SHIRIKISHO LA MASUMBWI PST PEMBE NDAVA

Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Sadiq Momba na Baina Mazola jana wamesaini mkataba wa kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo Mkoa wa Pwani uzito kwa kg 59
akizungumza wakati wa kutiliana saini kwa ajili ya mpambano huo promota Muhusini Sharif amesema ameamua kuwapambanisha mabondia hawo wanaotamba kwa sasa kwenye uzito uho kwa ajili ya kuleta chachu ya mchezo wa ngumi nchini

unajua Sadiq Momba ni bondia maarufu ambaye anakwenda sana nje ya nchi kwa ajili ya mapambano mbali mbali na amekuwa anafanya vizuri awapo nje ata hivyo mpambano wake wa mwisho nchini Thailand amepigwa kwa T.K.O ya raundi ya tatu na kurudi nyumbani hivyo anacho itaji ni ushindi na kupigana na mtu mwenye point za kutosha kumrudisha kileleni

na Baina Mazola katika uzito wake yeye  ni namba tatu katika boxrec nchini hivyo nae anataka kuwa zaidi ya bondia Momba na ndio anatishia amani katika uzito uho kwa sasa

nae bondia Momba amesema baada ya kupoteza mpambano wake nje ya nchi sasa wadogo zake wanamtaka kucheza nae kwani inaonekana kiwango changu kimepungua na kudiliki watoto wadogo kunitaka mimi ata ivyo nashukuru uhu mchezo mimi ni kazi yangu naitegemea ivyo nitaakikisha simpi nafasi ata chembe kwa kumpiga kipigo kibaya sana ambacho ajawai kupigwa tanga aanze mchezo wa masumbwi nchini 

nae bondia Mazola amesema kwa sasa yupo vizuri sana na anawaomba mashabiki zake kuwa na moli ya kwenda bagamoyo ambapo promota kafanya vizuri sana klupereka mpambao huu uko sisi mabondia wote wawili tuna umarufu mkubwa sana maeneo ya manzese na vitongoji vyake ata hivyo nita akikisha nampiga Momba kama begi kwa kuwa sasa ana jipya nimeona stail zake zote anazotumia kupigana sijaona jipya hivyo ajiandae kwa kipigo tu

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile





Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Monday, January 11, 2016

MCHUMIATUMBO ASAINI KUPIGANA NA BENK MWAKALEBELA JANUARY 30

Bondia Alphonce Mchumiatumbo kushoto akipokea mkataba alio saini kutoka kwa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa kwa ajili ya kupambana na Benk Mwakalebela wa Mbeya Picha na SUPER D BOXING NEWS


 Na Mwandishi Wetu

BONDIA Alphonce Mchumiatumbo amesaini mkataba wa kuzipiga na Benki Mwakalebelajanuary 30 katika ukumbi wa sativa Kyela Mbeya mpambano uho wa raundi nane wa uzito wa juu utafanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa uho

akisaini mkataba uho mbele ya Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa amesema ata akikisha kuwa mabondia wa uzito wa juu wanakuwa juu zaidi kwa mapambano hayo katika uzito uho

Mchumiatumbo alisema kuwa kwa sasa yupo katika mazoezi mazito chini ya kocha wake
Juma Urungu 'Mkebezi' 


ambapo kwa siku amekuwa akifanya mazoezi mara mbili au tatu kwa ajili ya kujiandaa na mpambano uho

nae Rais wa  TPBC Chaurembo Palasa ameongeza kwa kusema chama chao kimejizatiti kuinua mchezo wa ngumi kwa kufata taratibu na sheria za mchezo uho wa masumbwi nchini

kwanza wata akikisha kila bondia anapima afya na uzito wake kwa usalama wa mabondia wenyewe na usalama wao wawapo mchezoni

aliongeza kwa kusema kuwa watapima afya siku tano kabla ya mpambano huo ili kujilidhisha na afya za mabondia hawo wenye uzito wa juu nchini ambapo mabondia hawo wamekuwa adimu sana hapa nchini

BONDIA MCHUMIATUMBO KUMKABILI BENK MWAKALEBELA JANUARY 30 KYELA MBEYA

Bondia Alphonce Mchumiatumbo kushoto akipokea mkataba alio saini kutoka kwa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa kwa ajili ya kupambana na Benk Mwakalebela wa Mbeya Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Alphonce Mchumiatumbo kulia akisoma mkataba wake na kocha wake Juma Urungu 'Mkebezi'

Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa kulia akizungumza na promota juu ya mpambano wa Alphonce Mchumiatumbo katikati

Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa kulia akimpatia kiasi cha fedha bondia Alphonce Mchumiatumbo kushoto ni

Bondia Alphonce Mchumiatumbo akisaini mkataba wa kupambana na Benki Mwakalebela January 30



Friday, January 8, 2016

MABONDIA KAONEKA NA MAPAMBANO KUZICHAPA FEB 14 TANDIKA

Mabondia Shabani Kaoneka kushoto akitunishiana misuli na Imani Mapambano baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kupambana feb 14 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika maguruwe katikati ni mdau wa mchezo wa masumbwi Zahoro Maganga 'Super Diego'  picha na SUPER D BOXING NEWS
Mdau wa mchezo wa masumbwi nchini Zahoro Maganga 'Super Diego'  kushoto akimsainisha bondia Shabani Kaoneka kwa ajili ya mpambano wake na Imani Mapambano feb 14 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika maguruwe kulia ni Rais wa TPBO Yassin Abdallah
picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu
Mabondia Shabani Kaoneka na Imani Mapambano wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya feb 14  uzito wa kg 74 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika maguruwe

mpambano huo wa raundi nane utasimamiwa na oganaizesheni ya ngumi za kulipwa TPBO chini ya rais wake Yassin Abdallah 'ostadhi' mpambano huo wenye kugombaniwa kwa kila mmoja kuwa juu ya mwenzie ambapo bondia Kaoneka ni namba 11 katika viwango vya ubora nchini ambapo amepigana mapambano 13 akishinda 5 kupigwa 5 na sale 3

 atakuwa na kibarua kizito cha ku lilia namba yake kwa mtu wa chini yake Imani Mapambano anaeshikilia nafasi ya 12 ya ubora kwa mabondia wa Tanzania akiwa amecheza mapambano 7 akishinda 4 na kupoteza 3

katika mpambano mwingine utawakutanisha mabondia Hassan Mwakinyo atakae pambana na Salumu Salumu kg 72 katika mpambano wa raundi sita 


Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile

Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Sunday, January 3, 2016

CHEKA KUPANDA URINGONI FEB 23 DAR ES SALAAM

Promota Juma Msangi kushoto akitambulisha mpambano wa bondia Fransic Cheka atakaepambana na Geard Ajetovic wa Serbia mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam jana mpambano utakaofanyika feb 27 katika uwanja wa leaders club wengine ni Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' pamoja na Meneja msaidizi wa bondia  Faransic Cheka  Picha na Picha na SUPER D BOXING NEWS
Promota Juma Msangi kushoto akitambulisha mpambano wa bondia Fransic Cheka atakaepambana na Geard Ajetovic wa Serbia mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam jana mpambano utakaofanyika feb 27 katika uwanja wa leaders club wengine ni Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' pamoja na Meneja msaidizi wa bondia  Faransic Cheka  Picha na Picha na SUPER D BOXING NEWS
 Picha na SUPER D BOXING NEWS




Saturday, January 2, 2016

MABONDIA WATIFUANA KATIKAS KUFUNGUA MWAKA

Mabondia Shedrack Ignas kushoto akipambana na Abdallah Luwanje wakati wa mpambano wa kufungulia mwaka uliofanyika katika ukumbi wa frends corner manzese Luwanje alishinda kwa point katika mpambano uho wa kufungulia mwaka 2016 Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Abdallah Luwanje akinyooshwa mkono kuashilia ushindi

Bondia Hassani Mgos kushoto akipambana na Hassani Kitango wakati wa mpambano wao Kitango alishinda kwa point katika mpambano uho wa kufungulia mwaka 2016 Picha na SUPER D BOXING NEWS

Hassan Kitango akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi

Mohamed Kashinde akipambana na Mwinyi Mzengela masbondioa hawo walitoka droo

matokeo ni drooo


Hussein Mbonde akipambana na Shomari milundi katika mpambano uho wa kufungulia mwaka 2016 Picha na SUPER D BOXING NEWS

Hussein Mbonde akipambana na Shomari milundi katika mpambano uho wa kufungulia mwaka 2016 Picha na SUPER D BOXING NEWS

MABONDIA KUNYUKANA LEO MANZESE FRENDS CORNER

Mabondia Mwinyi Mzengela akitunishiana misuli na Mohamed Kashinde  baada ya kupima uzito jana kwa ajili ya mpambano wao wa leo litakalofanyika katika ukumbi wa frends corner manzese leo jumanmosi ya january 2 Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Shomari Milundi akipima uzito kwa ajili ya mpambano wa leo kushoto ni mpinzani wake Hussein Mbonde mpambano wao wa leo litakalofanyika katika ukumbi wa frends corner manzese leo jumanmosi ya january 2 Picha na SUPER D BOXING NEWS