Msimamizi wa  Mchezo wa ngumi katika kambi iliyopo sinza
makaburini,
 Bernald Lumbila (kushoto) akimwelekezai bondia Kalama Nyilawila jinsi 
ya kupiga ngumi katika mbavu Dar es saam Nyilawila anajiandaa na 
mpambano wake dhidi ya Ibrahimu Maokola utakaofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Msasani Klabu Picha nawww.superdboxing coach.blogspot.com 
 Kalama Nyilawila akijifua 
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Kalama Nyilawila yupo katika mazoezi makali ya mwisho mwisho kabla ajamkabili mpinzani wake Ibrahimu Maokola siku ya Desemba 31  mpambano wa kufunga mwaka utakaoshirikisha mabondia mbalimbali akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kalama ameseme yeye yupo fiti wakati wowote kwa ajili ya mpambano huo kwa ana usongo wa kuonesha ngumi zinachezwaje kwa mabondia chipkizi nchini
Mpambano huo utaanza kabla ya bondia Fransic Miyeyusho kupanda jukwaani kuvaana na David Chalanga kutoka Kenya mpambano wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi
na mapambano mengine ni Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atavaana na Mohamed Kashinde uku Cosmas Cheka akioneshana ubabe na Iddy Mnyeke mpambano mwingine ni Antoni Mathias atakae menyana na Fadhili Majiha mapambano yote ya utangulizi ni ya raundi sita sita 
siku hiyo itasindikizwa na burudani za kila aina akiwemo mwana hi pop mashuhulu Kala Pina, Kimbunga Noma na wengine wengi ambao wata uanga mwaka na kukaribisha mwaka mpya kwa njia ya burudani
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa 
na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria
 zake zikiwa na mabondia wakali kama vile 
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia
 kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
 mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa 
taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha