Thursday, March 21, 2019
Friday, March 1, 2019
SUNDAY KIWALE 'MORO BEST' NA IBRAHIMU MAKUBI KUPIGANA MOROGORO MARCH 2 MSAMVU TERMINAL
Na
Mwandishi Wetu
MABONDIA kutokwa kwa Super D Coach Uhuru GYM Sunday Kiwale 'Moro Best' na Ibrahimu Makubi wapo mkoani morogoro kwa ajili ya mpambano yanayo wakabili ambapo Sunday Kiwale 'Moro Best' atamkabili Said Chalachim kutoka Ifakara wakati Ibrahimu Makumbi atazipiga na Charles Chilala nae kutoka Ifakara
akizungumza baada ya kupima uzito kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mabondia wake wapo vitani hivyo awatofanya ajizi wala kuwa na msalia Mtume kwani kazi waliyotumwa na mashasbiki zao kutoka Dar es Salaam si yakitoto na awatotaka kuwangusha kwa kuwa wao ni watu wa kazi kazi
nae bondia kiwale anaetamba katika uzito wake amesema kuwa mabondia wengi nchini wanamuogopa ndio mana amekuja kucheza Mkoani ili kuendeleza kipaji chake kisije kikapotea bule kwa sababvu ya kuogopewa na mabondia wa Dar es salaam katika uzito wake kwani kazi yangu wanaijua na kuitambuwa niwapo ulingoni
na bondia Makubi alisema kuwa yeye ni bondia mchanga sana katika ngumi za kulipwa ila ni motto mkali katika masumbwi hivyo nawaomba wapenzi wa mchezo wa ngumi waje kwa wingu kushudia kazi atakayo ifanya
Mabondia hawo wote watakuwa wakisindikiza mpambano wa ubingwa kati ya Twaha Kiduku wa Morogoro na Mada Maugo watakaozipiga raundi kumi kugombea ubingwa wa Taifa nchini
Promota wa mpambano uho kaike Siraju alieleza kwa kusema kuwa ameandaa mapambano mengi sana nchini ususani Morogoro sasa baada ya kumuibua Fransic Cheka sasa ameibuwa mabondia wengine mbalimbali kutoka moro pamoja na vitongoji vyake hivyo kazi kwao mashabiki kutoa sapoti
aliongeza kwa kusema mbali na mapambano hayo kutakuwa na mitanange mingine ya kukata na shoka ambapo bondia Epson John atazipiga na Adamu Ngange na Cosmasi Cheka atakabiliana na Amani Bariki na kingilio katika mapambano yote hayo ni tsh 7000 na V.I.P 15000 na nyote mnakaribishwa
MADA MAUGO KUZIPIGA NA TWAHA KIDUKU MSAMVU MOROGORO MARCH 2
| Bondia Twaha Kiduku kushoto akiwa ameshika mkanda wa Taifa watakaogombania yeye na Mada Maugo March 2 Morogoro katika ukumbi wa Terminal Pub uliopo Morogoro Msamvu Picha na SUPER D BOXING NEWS |
| Bondia Twaha Kiduku kushoto akiwa ameshika mkanda wa Taifa watakaogombania yeye na Mada Maugo March 2 Morogoro katika ukumbi wa Terminal Pub uliopo Morogoro Msamvu Picha na SUPER D BOXING NEWS |
| BONDIA SUNDAY KIWALE 'MORO BEST' AKIPIMA UZITO |
| BONDIA IBRAHIMU NMAKUBI AKIPIMA UZITO |
Sunday, December 30, 2018
MABONDIA WAPIMA UZITO KUPIGANA DESEMBA 31 KINESI
| Bondia AZizi Uliza akingia na Farasi kwa ajili ya kupima uzito kupambana na Ramadhani Shauri desema 31 katika mpambano wa kufunga mwaka |
Wednesday, December 19, 2018
BONDIA AZIZI ULIZA AJIFUA KUMKABILI RAMADHANI SHAURI DESEMBA 31 KINESI SHEKILANGO
| Bondia Azizi Uliza akijifua kwa kupiga spidboll wakati wa mazoezo yake ya kujiandaa na mpambano wake na Ramadhani Shauri utakaofanyika katika uwanja wa Kinesi Shekilango Picha na Super D Boxing News' |
Na Mwandishi Wetu
BONDIA AZIZI ULIZA amendelea kujifua kwa ajili ya mpambano wake na Ramadhani Shauri utakaofanyika Desemba 31 katika uwanja wa Kinesi uliopo Shekilango nyuma ya urafiki
akizungumza na mwandishi wa habari hizi uliza amesema kuwa Shauri asumbui ata siku moja kwani yeye ni mkongwa na mimi ndio nachpkia hivyo sio kazi rahisi kushindana na mimi ingawa anatamba katika vyombo vya habari ikiwa kapigwa K,O mbaya na Idd Mkwera raundi ya 9 kwangu mimi asitegemee kuwa upenyo nitamwadabisha vya kutosha kwani nimejiandaa kwa ajili ya kupigana
hivyo nawaomba wapenzi na mashabiki wa mchezo wa masumbwi mje muone Uliza namfanya nini Shauri nitampiga kipigo ambacho akijawai kumtokea tangu aanze ngumi
alimaliza kwa kusema Azizi Uliza
nae Promota wa mpambano uho Josepher Nyilawila kutoka kampuni ya Ijuka Sports amesema mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine yatakayowakutanisha mabondia mbalimbali
siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katika
mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchini kama vile Glove gumshirt clip bandeji bukta protecter na vifaa vingine
Monday, December 17, 2018
MABONDIA WAJIANDAA KUZIPIGA DESEMBA 31 KINESI SHEKILANGO
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Ramadhani Shauri amendelea kujifua kwa ajili ya mpambano wake wa kufunga mwaka na kufungua mwaka utakaofanyika Desemba 31 katika uwanja wa kinesi shekilango maeneo ya urafiki Dar es salaam akimkabili Azizi Uliza katika mpambano wake wa raundi kumi
akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika kambi yake iliyopo mabibo mwembeni amesema kuwa yupo fiti kwa asilimia mia hivyo sasa anasubili mpambano tu yana natamani iwe ata leo tupate kumalizana mana nitampa kipigo ambacho si chakawaida alisema Shauri
aliongeza kwa kusema mashabiki wake wajitokeze kwa wingi waje kumwangalia kwani sasa anapigana ngumi za moto hatari kwani mpinzani wake atofika raundi ya sita hivyo nawaomba mashabiki wawai kuingia uwanjani mapema kabla mpambano aujaisha
nae Promota wa mpambano uho Josepher Nyilawila kutoka kampuni ya Ijuka Sports amesema mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine yatakayowakutanisha mabondia mbalimbali
siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katika
mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchini kama vile Glove gumshirt clip bandeji bukta protecter na vifaa vingine
BONDIA RAMADHANI SHAURI AJIFUA KUMKABILI AZIZI ULIZA DESEMBA 31 KINESI
Subscribe to:
Posts (Atom)














