Na
Mwandishi Wetu
MABONDIA kutokwa kwa Super D Coach Uhuru GYM Sunday Kiwale 'Moro Best' na Ibrahimu Makubi wapo mkoani morogoro kwa ajili ya mpambano yanayo wakabili ambapo Sunday Kiwale 'Moro Best' atamkabili Said Chalachim kutoka Ifakara wakati Ibrahimu Makumbi atazipiga na Charles Chilala nae kutoka Ifakara
akizungumza baada ya kupima uzito kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mabondia wake wapo vitani hivyo awatofanya ajizi wala kuwa na msalia Mtume kwani kazi waliyotumwa na mashasbiki zao kutoka Dar es Salaam si yakitoto na awatotaka kuwangusha kwa kuwa wao ni watu wa kazi kazi
nae bondia kiwale anaetamba katika uzito wake amesema kuwa mabondia wengi nchini wanamuogopa ndio mana amekuja kucheza Mkoani ili kuendeleza kipaji chake kisije kikapotea bule kwa sababvu ya kuogopewa na mabondia wa Dar es salaam katika uzito wake kwani kazi yangu wanaijua na kuitambuwa niwapo ulingoni
na bondia Makubi alisema kuwa yeye ni bondia mchanga sana katika ngumi za kulipwa ila ni motto mkali katika masumbwi hivyo nawaomba wapenzi wa mchezo wa ngumi waje kwa wingu kushudia kazi atakayo ifanya
Mabondia hawo wote watakuwa wakisindikiza mpambano wa ubingwa kati ya Twaha Kiduku wa Morogoro na Mada Maugo watakaozipiga raundi kumi kugombea ubingwa wa Taifa nchini
Promota wa mpambano uho kaike Siraju alieleza kwa kusema kuwa ameandaa mapambano mengi sana nchini ususani Morogoro sasa baada ya kumuibua Fransic Cheka sasa ameibuwa mabondia wengine mbalimbali kutoka moro pamoja na vitongoji vyake hivyo kazi kwao mashabiki kutoa sapoti
aliongeza kwa kusema mbali na mapambano hayo kutakuwa na mitanange mingine ya kukata na shoka ambapo bondia Epson John atazipiga na Adamu Ngange na Cosmasi Cheka atakabiliana na Amani Bariki na kingilio katika mapambano yote hayo ni tsh 7000 na V.I.P 15000 na nyote mnakaribishwa
No comments:
Post a Comment