Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Idd Mkwera na Rojas Masamu wamesaini kuzipiga April 20 kaika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu uliopo magomeni Mapipa akizungumzia mpambano uho Promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa pambano hilo litafanyika siku hiyo kwa kupewa nguvu na
Bondia Mtanzania Omari Kimweri 'Lion Boy 'anaefanya shughuli zake nchini Australia bondia huyo ndie aliesababisha mabondia hawo wazipige siku hiyo kwa kuwa vijana wanatakiwa kuendeleza rekodi zao za masumbwi kila wakati ndio mana akaongeza nguvu ili mpambano uho ufanyike
Super D aliongeza kwa kusema kuwa mbali na pambano hilo siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali yatakayokuwa yanafanyika siku hiyo ambapo bondia Hussein Pendeza atamkabili Juma Ramadhani 'Choki' na Shomari Milundi ataoneshana umwamba na Bakari Mbede wakati ibrahimu Makubi atavaana na Haruna Ndalo na Ramadhani Mbegu 'Migwede' atakabiliana na Rashidi Mnyagatwa na Salum Tandu zidi ya Gerald Mkude na Sunday Kiwale 'Moro Best' atalindima na Luckman Ramadhani Vicent Mbilinyi na Azizi Iddi Hussein Shemdoe na Jitu Rajabu
Mapambano yote hayo yanaletwa kwenu na kampuni tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion ambayo ipo nchini Tanzania kwa ajili ya kuinuwa vipaji ya vijana mbalimbali ili kuendeleza vipaji vyao pendwa
na kupitia kampuni ya Super D Promotion imejizatiti kuweka angalau pambano moja kila baada ya miezi milili ili kuwasaidia vijana mbalimbali kukuza vipaji vyao na kujiendeleza kupitia mchezo uho wa masumbwi nchini
No comments:
Post a Comment