Tangazo

Pages

Tuesday, September 11, 2012

SUPER D KUANDAA DVD YA KIDUNDA AKIWA KATIKA MASHINDANO YA OLIMPIC 2012


Na Mwandishi Wetu

KOCHA Kimataifa  wa mchezo wa ngumi wa Klabu ya Ashanti na Timu ya Mkoa wa Ilala Kimichezo, Rajabu Mhamila'Super D', anatarajia kuandaa CD ya bondia wa mchezo huo, Seleman Kidunda.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Super D alisema kuwa anatarajia kuandaa DVD hiyo ambayo itakuwa inaonesha matukio mbalimbali yaliyofanyika Mjini London wakati Kidunda alipokwenda kwenye mashindano ya Olimpic.

Alisema kuwa DVD hiyo inatarajiwa kuingia sokoni mwisho wa mwezi huu ambapo pia itaonesha kambi ya Kidunda wakati alipokuwa London.

Kocha huyo alisema kuwa anatarajia kuandaa DVD hiyo ili kuweza kutoa fursa kwa mashabiki na wapenzi wa mchezo wa ngumi, kuweza kuona matukio mbalimbali yaliyotokea na yaliyomhusisha Kidunda.

Alisema kuwa mashabiki pamoja na mabondia watajifunza mambo mengi kwa kupitia DVD  hiyo ikiwemo mafunzo ya mchezo huo pamoja na sheria zake ambazowadau wote wanapaswa kujua hizo taratibu na sheria za mchezo huo DVD ambayo itatoka mwishoni mwa mwezi huu.

"Ninatarajia kutoa DVD ambayo itakuwa inaonesha matukio mbalimbali yaliyotokea nchini London wakati Kidunda alipokwenda kwenye michuano ya Olimpic" alisema.

Kuanzia kambi aliyofikia mpaka alipokuwepo ulingoni akishiliki mashindano hayo hii ni historia ya pekee kwa tanzania ambapo iliwakilishwa na bondia mmoja ambaye ni selemani Kidunda katika DVD hiyo pia kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia wa Tanzania waliowai kucheza nashindano ya kimataifa wakiwa nje ya Nchi

Pamoja na ndani ya nchi Super D ambaye utumia kufundisha mbinu mbalimbali za masumbwi kupitia DVD ambapo mpaka sasa amekwisha towa matoleo 16 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo huo yakishilikisha mabondia  Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye, Nonito Donaire na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.


Super D usambaza DVD zake Katika Michezoya  ngumi  yote ambapo pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Mkoa wa Kimichezo wa Ilala, Rajabu Mhamila ‘Super D’ kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.Ndani yake wakiwemo mabondia wengi wanaotamba kitaifa na kimataifa



MASHINDANO YA TAIFA YA MASUMBWI KUANZA SEPTEMBA 17

Kocha wa mchezo wa ngumi Hasan Mzonge akiwaelekeza mabondia wa timu ya taifa ya masumbwi jinzi ya kupiga ngumi zilizonyooka wakati wa mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika katika GMY ya Gmykhana Klabu.picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
                                 SHIRIKISHO LA NGUMI LA TAIFA (BFT)
                                                                                                        S.L.P 15558                                                                             

       DAR ES SALAAM
                                                                                                               September 10, 2012
                                                                                 Email:-bft.tanzania2009@gmail.com
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
          YAH:-MASHINDANO YA UBINGWA WA TAIFA 17-22/09/2012.
Shirikishi la ngumi Tanzania (BFT)limeandaa mashindano ya ngumi ya ubingwa wa Taifa 2012 yatakayofanyika kuanzia jumatatu ya tarehe 17-22/09/2012 uwanja wa ndani wa taifa (indoor stadium) kila siku kuanzia saa 9.00 alasiri.
Awali mashindano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika kuanzia tarehe 15/09/2012 lakini kutokana na uwanja wa ndani wa taifa kuwa na shughuri nyingine ya kimichezo ya ligi ya mpira wa kikapu,sasa mashindano hayo yataanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 17/09/2012.
Lengo la mashindano hayo ni kupata timu ya taifa ya ngumi yenye sura ya kitaifa ,itakayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania bara.ili kuanza maandalizi ya mapema na ya uhakika kwa ajili ya kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola 2014,mashindano ya Afrika 2015,mashindano ya olimpiki 2016,ubingwa wa dunia na mashindano mbalimbali tutayopata mwaliko kwa ajili ya kuwakilisha taifa.
Hadi  leo jumla ya mikoa kumi na nane (18) imethibitisha kuja kushiriki katika mashindano hayo,mikoa hiyo ni mikoa ya kimichezo ya Temeke,Kinondoni  na Ilala.Mingine ni Ngome ya JWTZ,JKT,Magereza na Polisi.Mingine ni Pwani,Morogoro,Mbeya,Ruvuma,Dodoma,Kigoma,na Bukoba.mikoa mingine ni Tanga,Arusha ,Tabora na Mwanza.
Uongozi wa BFT licha ya kutopata udhamini wa uhakika wa kufanikisha mashindano haya,kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tumejipanga vema kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kiwango cha hali ya juu ili kufikia lengo la kupata timu ya taifa kwa wakati kwa maandalizi ya mapema.mashindano hayo yana takiwa kufanyika kwa bajeti ya milioni ishirini na sita (26,000,000/=).
Sasa Mabadiliko ya ratiba ya mashindano itakuwa kama ifuatavyo:-

TAREHE    MUDA    TUKIO      
16/09/2012        Timu zote kuwasili dare s salaam.      
17/09/20123    1.00-4.00 Asb
4.00-5.00 Asb
5.00-7.00 Mch    Kupima uzito na afya,uwanja wa taifa wa ndani.
Zoezi la draw na bye na ratiba ya mashindano.
Semina kwa waamuzi,timu manaja,makocha kwa ajili ya kupatiwa kanuni na sheria za mashindano.      
18/09/2012    1.00-2.00 Asb
8.00-2.00 Usk    Kupima uzito na afya,uwanja wa taifa wa ndani.
Gwaride la ufunguzi na kuanza mashindano hatua ya mtoano      
19/09/2012    1.00-2.00 Asb
9.00-2.00 Usk    Kupima uzito na afya
Mashindano kuendelea hatua ya mtoano      
20/09/2012    1.00-2.00 Asb
9.00-2.00 Usk    Kupima uzito na afya
Mashindano kuendelea kwa hatua ya robo fainali      
21/09/2012    1.00-2.00 Asb
2.30-8.45Mch
9.00-2.00 Usk    Kupima uzito
Mkutano mkuu  wa BFT(indoor stadium)
Mashindano kuendelea hatua ya nusu fainali      
22/09/2012    1.00-2.00 Asb
8.00-2.00 Usk    Kupima uzito na afya.
Gwaride la kufunga na kuendelea kwa mashindano hatua ya fainali.      
23/09/2012        Timu zote kuondoka   
Aidha ajenda za mkutano mkuu wa wanachama wa bft ni mbili tuambazo ni kupitia na kupitisha rasmu ya katiba ya BFT na maandalizi ya uchaguzi wa BFT wa kuwapata viongozi makiniwa kuongoza BFT kwa kipindi cha miaka mine kuanzia marchi 2013 kwa mujibu wa katiba .
Makore Mashaga
Katibu Mkuu BFT.,
   Mob:-0713/0784/0763/0773 -58 88 18
Email:- mashagam@yahoo.om

Sunday, September 9, 2012

VITALI KLITSCHKO AMCHAPA MANUEL CHARR WA UJERUMANI


Bondia Manuel Charr wa Ujerumani akiokolewa na mwamuzi baada ya kupigwa na Vitali Klitschko na kuchanika jichoni na kutokwa damu nyingi kama anavyoonekana.
 
MOSCOW, Russia

Manuel Charr, ambaye alshinda katika raundi kama hiyo alipoumana na Danny Williams, juzi alilazimika kutoendelea na pambano lake dhidi ya Vitali, kutokana na konde zito lililomchana juu ya jicho lake la kulia

BINGWA wa WBC Vitali Klitschko, alifanya kazi rahisi ulingoni kumuwezesha kuibuka na ushindi pasipo changamoto kubwa kutoka kwa Mjerumani Manuel Charr, katika dakika ya mwisho ya raundi ya nne jijiji hapa. 

Klitschko, 41, ameibuka mbabe wa pambano hilo dhidi ya mpinzani wake ambaye hakuwahi kupigwa huko nyuma.

Charr, ambaye alipata ushindi wa raundi kama hiyo alipoumana na Mwingereza Danny Williams, alilazimika kutoendelea na pambano hilo kuokana na konde zito lililomchana juu ya jicho lake la kulia na kumsababishia kumwagika kwa damu nyingi.

Hata hivyo Charr alikuja juu kupinga maamuzi – kufuatia majibu ya uchunguzi wa madaktari kuwa alikatwa na kitu na kwamba jeraha lake halikutokana na ngumi, hivyo kupinga matokeo.

Klitschko kwa mara nyingine anaingia katika ushindi wa utata, baada ya Februari mwaka huu kumchapa Dereck Chisora kwa pointi, na kusababisha mgogoro baina yam kali huyo na David Haye wakati wa mkutano na vyombo vya habari.

Haye, ambaye alipigwa kwa pointi na ndugu wa kuzaliwa wa Vitali, Wladimir mwaka jana, alifanikiwa kumchapa Chisora KO Julai mwaka huu nma kuamua kuomba pambano dhidi ya mkongwe huyu Vitali.

Pambano baina ya Haye na Vitali, linaweza tu kufanyika kama raia huyo wa Ukraine atashindwa uchaguzi wa nchi yake ambako anawania ubunge, ambapo kama akishinda atalazimika kustaafu masumbwi.

Friday, September 7, 2012

TAMASHA LA MASUMBWI LA KIMATAIFA-MTWARA


 Kushoto Rashid Matumla,Mohamed Matumla,Matumla,Mbwana Matumla na Mkwanda Matula 
 .
OGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA [TPBO]

IANWAPA TAARIFA KWAMBA IFIKAPO TAREHE 27-10-2012 KUTAFANYIKA TAMASHA KUBWA LA MASUMBWI YA KULIPWA YATAKAYOWASHIRIKISHA MABONDIA KUTOKA KENYA NA TANZANIA .
TAMASHA HLI LINAANDALIWA NA REDIO SAFARI CHINI A MKURUGENZI WAKE NDG  HARUN MTAFAKARI NA LINASIMAMIWA NA TPBO AMBAYO TAYARI IMESHATOWA KIBALI CHA MAPAMBANO HAYO

BONDIA MAARUFU NCHINI NA DUNIANI KOTE MBWANA MATUMLA ATAPAMBANA NA BONDIA ABDUL NOOR KUTOKA KENYA /
 KATIKA UZITO WA SUPER BANTAM kilo gramms 55.8 WATAPIGANA RAUNDI 8

NA BONDIA MKONGWE NA BINGWA WA DUNIA KATIKA MATAJI MBALI MBALI RASHID MATUMLA ATAPAMBANA NA BONDIA KUTOKA KENYA PATRIC AMOTE KWENYE UZITO WA SURPER MIDDLE KILOGRAMMS 76 NA WATAPIGANA RAUNDI 8

TAMASHA HILO PIA LITAWASHIRIKISHA MABONDIA KUTOKA BLACK MAMBA YA MTWARA  WAO WATAPAMBANA NA MABONDIA KUTOKA DAR-ES-SALAAM

MAANDALIZI YA TAMASHA HILI YANAENDELEA VYEMA NA MABONDIA WOTE WAMESHASAINISHWA MIKATABA YA MAPAMBANO YAO NA WANAJIFUWA VILIVYO.


TPNO INAFURAHISHWA SANA NA JINSI MAPROMOTA WANAVYOJITOKEZA SEHEMU MBALIMBALI NCHINI NA KUWAANDALIA MABONDIA MAPAMBANO ILI WAJIPATIE RIZIKI ZA KUJIKIMU KIMAISHA NA TPBO INAWATAKA WALE MABONDIA AMBAO HUCHUKUWA MALIPO YA AWALI KWA MAPROMOTA NA KISHA KUINGIA MITINI BILA KUFIKA ULINGONI ,WAACHE MARA MOJA MTINDO HUO KWANI ITAWAKATISHA TAMAA MAPROMOTA NA KUUKIMBIA KABISA MCHEZO WA NGUMI NA ITAPELEKEA MABONDIA KUJIINGIZA KATIKA VTTENDO VYA UHALIFU KWA KUKOSA HELA ZA MATUMIZI, VITENDO AMBAVYO TPBO INAVILAANI MARA ZOTE. NA TPBO DAIMA HAITAKUWA TAYARI KUFANYA KAZI NA MABONDIA WENYE TABIA HIZO ZA KITAPELI.


IMELETWA KWENU NAMI

YASSIN ABDALLAH -USTAADH

RAIS TPBO

Tuesday, September 4, 2012

KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA MASUMBWI HASSANI MZONGE AHAMUA KUZIPIGA NA MABONDIA WAKE


Kocha wa timu ya Taifa ya Masumbwi Hassani Mzonge kushoto akipambana na Bondia Nasser Mafuru wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika GYM Khana
Bondia Nasser Mafuru kulia akipambana na mwenzake wakati wa mazoezi yake leo




Saturday, September 1, 2012

TIMU YA TAIFA YA MASUMBWI IKIWA MAZOEZINI

Bondia Selemani Kidunda kulia akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo cha televisheni ya Mlimani walipotembelea mazoezi ya timu ya taifa ya masumbwi yanaoendelea katika viwanja vya GYM Khana Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa ngumi Hassani Mzonge katikati akioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi na Undule Langson wakati wa mazoezi ya timu ya taifa  kulia ni Abdallah Kasimu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa ngumi Hassani Mzonge katikati akioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi na Undule Langson wakati wa mazoezi ya timu ya taifa  kulia ni Abdallah Kasimu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Undule Langsonkushoto na Abdallah Kasimu wakioneshana uwezo wa kutupiana masumbwi wakati wa mazoezi ya timu ya taifa

KOCHA WA KIMATAIFA WA MASUMBWI SUPER D ATEMBELEA KAMBI YA TIMU YA TAIFA


Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' aliechuchumaa akiwa katika picha ya pamoja na mabondia wa Timu ya Taifa pamoja na Makocha wa timu hiyo alipotembelea mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea katika GYM ya Gymkhana  kushoto ni Selemani Kidunda aliekuwa akituwakilisha katika mashindano ya Olimpic 2012 yaliyomalizika hivi karibuni wachezaji hawo kwa sasa wanajiandaa na mashindano ya Taifa yatakayoanza September 15 katika uwanja wa Ndani wa Taifa .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa katika picha ya pamoja na mabondia wa timu ya taifa na makocha wenzake alipotembelea mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea katika GYM ya Gymkhana.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D'  wa pili kulia akiwa katika picha ya pamoja na mabondia wa timu ya taifa na makocha wenzake alipotembelea mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea katika GYM ya Gymkhana.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com