Tangazo

Pages

Sunday, September 11, 2011

PACQIAO ATAKIWA KUMCHAPA MARQUEZ

PROMOTA maarufu wa mjini New York Marekani, Bob Arum Amemshauri bondia Manny Pacquaio kupigana kufa na kupona ili aweze kumchapa Juan Mrquez pindi watakapokutana Novemba 12 mwaka huu.

Alisema kuwa hafikirii kama Pacquiao ataweza kushinda kirahisi kama wengi wanavyofikilia pamoja na kukiri kuwa Pacquiao ni mzuri, lakini alimshauli kuwa macho na Marquez kwa sababu naye si wa kumpuuza 

'Namtambua Manny Pacquiao hana uwezo wa kujibu mashambulizi kwa uwezo mkubwa kama anavyofikiriwa; alisema
Aliongeza kuwa wakati  Pacquiao anapokutana na mpambanaji mzuri ,huwa anaishiwa nguvu

VITALI AMTAKA HAYE AJIONGEZEE REKODI

BINGWA wa WBC uzito wa juu Duniani, Vitali Klitschko ametangaza nia yake ya kutaka kupambana na David Haye.
Vitali mwenye rekodi ya kushinda mapambano 42 (39 kwa 'ko) na kushindwa mawili, alisema kuwa anamtaka haye kwa sababu nia yake ni kucheza mapambano makubwa matatu kabla ya kustaafu.
Alisema kuwa anatamani kucheza na bingwa huyo wa zamani wa WBA ambaye anaamini atakapomchapa itamsaidia kuongeza rekodi yake
Haye anatarajia kupanda ulingoni tena Oktoba 31, ili arejeshe mikanda ya IBF,WBA NA WBO aliyopoteza kwa kaka yake Vitali Wladimir Klitschko

Friday, September 9, 2011

TEMEKE KINONDONI NANI ZAIDI KATIKA MASUMBWI



MABONDIA Mbwana Matumla wa Temeke na Francis Miyeyusho wa Kinondoni Dar es Salaam wanatarajia kupanda ulingoni katika pambano la kudhihirishiana ubabe kati ya mabondia wa Temeke na Kinondoni litakalofanyika Oktoba 30 mwaka huu.

Pambano hilo pia litafuatiwa na lingine kati ya Ramadhani Shauri wa Kinondoni dhidi ya Issa Sewe wa Temeke ambapo yote yatafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha Msaidizi wa Kambi ya Kinyogoli Foundation ya Dar es Salaam, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema mapambano hayo yameandaliwa na Promota Mohamedi Bawaziri kuhamashisha mchezo huo."Mabondia wote wameanza mazoezi na kwa upande wa Temeke wapo kambini chini ya Kinyogori Foundation chini ya kocha Habibu Kinyogori akishirikiana na mimi na tunawaandaa kucheza ngumi za kisasa sio kurusha ngumi bila mpangilio.," alitamba Super D

Alisema pambano kati ya Matumla na Miyeyusho litakuwa la uzani wa Bantam Weight kilogramu 54 ambapo Shauri na Sewe watacheza kilogramu 58, uzito mwepesi (Light Weight).

Alisema licha ya kuhamasisha, kumekuwepo na tambo za mda mrefu kati ya mabondia wa Kinondoni, na wenzao wa Temeke ambapo mashabiki watajionea mapambano hayo.

Kocha huyo alisema mapambano hayo yatasindikizwa na mengine kutoka kwa mabondia wa Temeke na Kinondoni ambapo pia kutakuwepo na burudani mbalimbali zitakazotangazwa baadae.

Tuesday, September 6, 2011

Changarawe aenda Uingereza na bondia mmoja kutoka mkoa wa ilala




MAKAMU wa Rais wa Shrikisho la Ngumi za Ridhaa (BFT), Michael Changarawe, ameondoka nchini na bondia mmoja kwenda kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola ya vijana walio chini ya umri wa miaka 18, yatakayoanza Septemba 8 hadi 13 mwaka huu nchini Uingereza.

Bondia wa Mkoa wa Ilala Mussa Mohamedi (kushoto) akioneshana ufundi wa kutupa masubwi na Salehe Omari wa Ngome wakati wa fainal ya michuano ya Klabu bingwa Dar es salaam . uzito wa kilo. 49 Light fly

Changalawe amesema ameondoka na bondia Musa Mohamed 'Dogo Musa', kwenda nchini Uingereza kushiriki michuano hiyo ya vijana itakayoshirikisha nchi mbalimbali.

Katibu wa shirikisho hilo, Makore Mashaga, amewapongeza mabondia walioshinda katika mapambano yao ya kwanza nchini Msumbiji katika michuano ya All Africa Games.

SHAURI AMTWANGA BAKARI KWA POINT

Bondia Bakari Mohamed (kushoto) na Ramadhani Shauri wakioneshana viwango vya kutupa masumbwi wakati wa mpambano wao wa kirafiki uliofanyika Dar es salaam juzi, Shauri alishinda kwa point

Saturday, September 3, 2011

NGUMI KUPIGWA MWANANYAMALA JUMAPILI HII

MABONDIA Ramadhani Shauri na Bakari Mohamed 'Dunda'  wanatarajia kupanda jukwaani katika pambano lao lisilo la ubingwa litakalofanyika katika ukumbi wa CCM Mwinjuma, Mwananyamala A, Dar es Salaam jumapili hii.

Pambano hilo linatarajia kuwa katika uzito wa kg 57 likiwa katika raundi nane ambapo pia litapambwa na burudani ya muziki wa asili kutoka katika kundi jipya la Makhirikhiri la hapa nchini.


Akizungumza Dar es Salaam leo, baada ya kupima uzito bondia Shauri alisema anajiamini kwa maandalizi aliyoyafanya kuwa yatamuwezesha kumtwanga mpinzani wake katika raundi za mwanzo na kuibuka bingwa.

"Nina maandalizi ya kutosha na ninaimani nitamtwanga Dunda kwani na jiamini na hawezi kunifikia kiuwezo," alisema Shauri.

Naye kwa upande wake Dunda alisema, majibu ya tambo za mpinzani wake huyo yatapatikana ulingoni hivyo mikono yake ndio itatoa majibu ya majigambo yake yote.

"Siwezi kubishana kwa maneno kwani wakati nafanya mazoezi viungo vyangu hasa mikono ndio vilikuwa vinatumika hivyo naviacha vitende kazi yake," alisema Dunda.

Hata hivyo mratibu wa pambano hilo Ibrahim Kamwe 'Bigright' alisema, taratibu zote za kimaandalizi zimeishakamilika kwani siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha ambapo pambano litafunguliwa na burudani kutoka katika kundi hilo la Makhirikhiri.

Aliyataja mapambano mengine ya utangulizi kuwa ni Athony Mathias ambaye ataumana na Shabani Madilu, Joseph Mbowe na Ezekiel Juma ambapo Issa Omary ambaye atapigana na Kade Khamis huku mapambano haya yakiwa katika raundi nane, 

Katika raundi sita watakuwa ni Saadat Miyeyusho akichapana na Herman Richard, huku raundi nne wakidundana Yona Miyeyusho na Haruna Said, Martin Richard na Jumanne Kilumbelumbe na Mwaite Juma akiwa na Frank Pury.

Wakati huo huo Kocha wa klabu ya ngumi ya Ashanti na Timu ya Mkoa wa Ilala ,Rajabu Mhamila 'Super D' atasambaza kanda zinazotoa mafunzo ya mchezo huo katika pambano hilo.

Kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha  Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo."Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi", alisema Super D.

Thursday, September 1, 2011

NGUMI ZAFUNIKA MJI KASORO BAHARI


Bondia Deo Njiku (kushoto) akipambana na Maliki Kinyogoli wakati wa mchezo wao uliofanyika Morogoro juzi Njiku alishinda kwa point



Mabondia Mada Maugo (kushoto) na Fransic Cheka wakioneshana ufundi wa kutupa masubwi wakati wa mpambano wao uliofanyika morogoro juzi Cheka alishinda kwa point