Tangazo

Pages

Thursday, July 30, 2020

SUPER D AMNOWA JUMA CHOKI KUJIANDAA KUMKABILI EMANUEL MWAKYEMBE AUGUST 14 MLIMAN CITY


Bondia Juma Choki kushoto askioneshana Umwamba wa kutupiana makonde na bondia wa kimataifa Ibrahimu Class wakati wa mazoezi yake katika Kambi ya Super D Coach Shule ya Uhuru ya kujiandaa na mpambano wake na Emanuel Mwakyembe utakaofanyika Augost 14 Mlimani City Dar Es Salaam



Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akipambana na Juma Choki katika mazoezi yaliyofanyika katika Kambi ya Super  D Coach Shule ya Uhuru Dar Esa salaam Choki anajiandaa na mpambano wake na Emanuel Mwakyembe utakaofanyika augost 14 katika ukumbi wa Mlimani City
Na Mwandishi Wetu

Bondia Juma Choki anaye jiandaa na mbambano wake dhidi ya Emanuel Mwakyembe AUgust 14 katika ukumbi waMlimani City jijini Dar es es salaam amejinasibu kumpiga bondia huyo na kuendeleza ubabe baada ya mara ya kwanza kumpiga na kuwa bingwa wa ubingwa wa king of The Ring katika mashindano yaliyofanyika mwaka jana

akijinasibu bondia huyo alivyotembelewa kambini kwake kwa Super D Coach iliyopo shule ya Uhuru Jijini Dar es salaam 

Amesema kuwa mwakembe ana uwezo wa kukanyaga moto wake ata siku moja kwani kichapo alichompa mara ya kwanza kitakuwa zaidi ya kile 
naomba mashabiki waje kuangalia kichapo nitakachompa ulingoni 
 kwani ndipo pa kuoneshana uwezo kama anavyosemaga kocha Super D Kazi Kazi No Pain No Gain yani siku hiyo patachimbika hivyo mwakyembe ajipange sana kwana mazoezi ninayofanya na mbinu ninazofundishwa sio za kitoto hatari tupu

Nae kocha wa bondia huyo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema hii ni vita kubwa sana kwa kuwa kocha wa mwakyembe  Edward Lwiyakwipya wamesoma nae pamoja katika ngazi kubwa ya kozi ya kimataifa hata hivyo mimi nina mbinu nyingi zaidi yake ndio mana nilimtwanga katika mpambano wa kwanza na sasa naenda kupiga begi langu tena ata hivyo nita akikisha napata ushindi usiokuwa wa kuwachosha majaji hivyo matumaini yangu ni kumpiga k,o mbaya zaidi

ikumbukwe kuwa mabondia wote wenye viwango vya juu nchini wanatoka kwangu ukiangalia mabondia wote wakubwa wanatoka kwangu
wanakuwa na viwango vya kimataifa hivyo najivunia kwa hilo ukiangalia mabondia wanaotoka kwangu akuna ata mchovyu mmoja alijinasibu Super D

Aliongeza kwa kusema mikono yake wamepita mabondia wengi sana akiwemo Sanday Kiwale, Idd Mkwera Vicent Mbilinyi Ibrahimu Class' King Class Mawe' Shomali Milundi  Shabani Kaoneka na mabondia mbalimbali nchini wote wamepita katika mikono yangu kwa njia moja au nyingine hapa ndio No Pain No Gain kazi kazi hivyo wapenzi wa ngumi muje kwa wingi kuangalia kazi hii ambayo aita muacha mtu salam siku hiyo katika viwanja vyua mlimani City

No comments:

Post a Comment