Tangazo

Pages

Thursday, July 9, 2020

BONDIA HASSANI MWAKINYO ATANGAZA MPAMBANO WAKE WA AGOST 14 MLIMANI CITY ATAMVAA TSHIBANGU KAYEMBE WA DRC YA CONGO

Bondia Hassani Mwakinyo kushoto akizungumza na wahandishi wa habari wakati akitangaza mpambano wake wa Agost 14 utakaofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Dar Esa Salaam Tanzania wa pili ni Mlatibu wa mpambano uho Beatrice Said na kulia ni bondia Tonny Rashidi nae atamsindikiza Mwakinyo siku hiyo Picha na Super D


Mlatibu mkuu wa mapambano Beatrice Said kulia ambaye ameandaa mchezo wa masumbwi yatakayofanyika Agost 14 akiwa na bondia Tonny Rashidi atakae tetea ubingwa wake huo na Gabriel Ochieng wa Kenya  

Mratibu wa mpambano wa masumbwi Beatrice Said akiwa na bondia Hassani Makinyo wakati wa kutangaza mpambano wake wa agost 14 utakaofanyika katika ukumbi wa mlimani city




BONDIA Mtanzania Hassan Mwakinyo anatarajia kupanda ulingoni Agosti 14 mwaka huu kumenyana na Bondia kutoka DRC ya Congo Tshibangu Kayembe.
Pambano hilo la aina yake la kuwania ubingwa wa WBF linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani city ambapo mabondia hao watapambana raundi 12.
Akizungunzia mtanange huo Mwakinyo amesema yuko tayari kwa pambano hilo kwani amejiandaa vya kutosha kuhakikisha anamaliza pambano hilo mapema.
Amesema, maandalizi mazuri ambayo ameyafanya na kuendelea kuyafanya yanazidi kumpa morali zaidi kuelekea pambano hilo ambalo hatokubali kuiangusha Nchi.
"Tarehe 14 mwezi ujao natamani sana pambano lifike hata siku zikimbie ziwe tano tano, nimejiandaa na naendelea kujiandaa sina shaka wala hofu na bondia yoyote yule aje tu tukutane ulingoni,"
Aidha Mwakinyo alimuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuri kuunga mkono jitihada za mabondia hapa nchini kama ambavyo amefanya mambo makubwa katika kuendeleza  nchi na jina lake kuzidi kuwa kubwa.
Anasema Rais akisapoti mchezo huo hata wao mabondia itakuwa vyema kwao na itazidi kuwapa morali ya hali ya juu kuzidi kulitangaza Taifa.
"Naimani kubwa na Rais wetu pia nawaomba wadhamini nao wasiutupe mchezo wetu huu unapeperusha vyema bendera ya Tanzania kupitia sisi na hiyo Agosti 14 nitawahahakikishia Watanzania mimi ni nani,"
Kwa upande wake Mratibu wa matukio kuelekea pambano hilo Beautrice Said amesema katika pambano hilo kutakuwa na mapambano ya utangulizi nane ya utangulizi ambayo yatawakitanisha mabondia wa hapa Tanzania.
Baadhi ya mapambano hayo ni Seleman Kidunda ambaye ataumana na Shaban Kaoneka uzito kg 72, Issa Nampepecha na Khareed Manjee kg 61.
Pia katika pambano hilo kutakuwa na pambano lingine la Kimataifa ambalo litamkutanisha Tony Rashid atakayemualika Mkenya Gabriel Ochieng pambano la raundi 12 kutetea ubingwa wa ABU.
Mwakinyo amepambana mapambano 18 na kupoteza mawili huku mpinzani wake Kayembe amecheza mapambano 12 kashinda 9 na kutoka sare 3. 

aliongeza kwa kusema kuwa mapambano mengine yatawakutania bondia Juma Choki dhidi ya Emanuel Mwakyembe na Baina Mazola atamkabili Haidari Mchanjo mbali na mapambano hayo kutakuwa na mapambano kumi kabla ya mpambano mkubwa wa Mwakinyo




No comments:

Post a Comment