Tangazo

Pages

Friday, August 9, 2013

MABONDIA FRANCIS MIYEYUSHO NA FIDELIS LIPUPA WAPIMA AFYA NA UZITO KUZIPIGA IDD MOSI
 Mabondia Francis Miyeyusho wa Tanzania (kulia) akitunishiana misuli na bondia Fidelis Ipupa wa Zambia, wakati wa zoezi la kupima uzito kwa ajili ya pambano lao la Kimataifa litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Dar Live, jijini Dar es Salaam.

Mabondia hao, wamewaongoza  mabondia wengine waTanzania watakaopanda ulingoni kesho katika mapambano ya utangulizi

Zoezi zima la upimaji liliongozwa na Katibu Mkuu wa ngumi za kulipwa, Ibrahim Kamwe,  akisaidiwa na Dk Madono.
''Mabondia wote waliopima wapo vizuri kwa mapambano yao ambapo Francis Miyeyusho, amepata Kg 55.5 na mpinzani wake Fidelis Ipupa, amepata Kg 56  na Ramadhan Kido wa Dare s salaam amepata  Kg 89.7 na mpinzani wake Kg 90.2.
Aidha kutakuwepo na mapambano mengine manne ya utangulizi na  mabondia wameuwiana vema na wale kina dada Esther  na  Lulu watazichapa kama kawaida''. alisema kamwe. 
Siku hiyo kutakuwa na uhuzwaji wa DVD mpya kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi zitakazokuwa zikisabazwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
 
DVD hizo mpya ni kati ya  
mike tyson vs evander holyfield na felix trinidad vs roy jones jr

Felix 'Tito' Trinidad vs Pernell Whitaker

ambapo dvd hizo zilizo rekodiwa kwa ubora wa hali ya juu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mchezo wa masumbwi nchin


--
Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
           mhamila1@gmail.com
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

No comments:

Post a Comment