Tangazo

Pages

Tuesday, July 26, 2011

Timu ya wabunge ya POOL yakikabidhiwa zawadi Dodoma


Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) akimkadbidhi Mshindi wa jumla wa mashindano ya mchezo wa POOL George Simbachawene Mbunge wa Kibakwe (Kulia) zawadi ya ngao aliyopewa na Chama Cha mchezo huo (TAPA) mara baada ya kuibuka mshindi wakati wa mashindano ya timu ya bunge na combine ya TBL na TAPA yaliyofanyika jumamosi iliyopita mjini Dodoma. Hafla hiyo fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi ilifanyika leo nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Viongozi wa Serikali, wachezaji wa timu ya Pool ya Bunge na viongozi wa Chama Cha POOL Tanzania (TAPA) wakiwa katika picha ya pamoja nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kukabidhiwa kwa zawadi za washindi wa mashinndano hayo yaliyoandaliwa na TAPA yaliyofanyika jumamosi iliyopita mjini Dodoma.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) akimkadbidhi Mshindi wa pili wa mashindano ya mchezo wa POOL Dkt. Charles Tibeza Mbunge waBuchosa (Kulia) zawadi ya fimbo ya kuchezea aliyopewa na Chama Cha mchezo huo (TAPA) mara baada ya kuibuka mshindi wakati wa mashindano ya timu ya bunge na combine ya TBL na TAPA yaliyofanyika jumamosi iliyopita mjini Dodoma. Hafla hiyo fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi ilifanyika leo nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment