Mchezowa ngumi za kulipwa ni mchezo pekee unaoweza kumpa mtu, taasisi au kampuni inayowekezafaida kubwa kwa kipindi kifupi sana. Ni mchezo ambao mbali na mingine ambayohuwa inategemea uchezaji wa ushirikiano wa wale wanaoshiriki una hamasa kubwasana hivyo kutoa fursa kubwa kuupromoti au kuudhamini.
Katikakipindi changu cha uongozi wa bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba yaUajemi nitajitahidi sana ili mtanzania mmoja mmoja, taasisi pamoja namakampuni ya biashara yaweze kufaidika sana katika mchezo huu.
Watuwengi huwa na imani hasi kuhusu mchezo wa ngumi na hivyo kutoweza kujua thamanina faida zinazopatikana kwenye mchezo huu.
Mbalina
kutoa ajira kwa njia ya kipato wanazopata washiriki kwa maana ya
mabondia, kunapia ajira kwa wale wanaohudumia hatua kwa hatua wakati wa
maandalizi ya pambanokama vile makampuni ya matangazo kama vile
magazeti, redio, televisheni na blogs mbalimbali.
Aidha
makampuni za huduma kama vile vinywaji, na vyakula. Makampuniya nguo.
Kamapuni ya huduma kama vile mapambo. Makampuni yanayotoa huduma ya
utalii na usafiri. Makampuni ya huduma za ulinzi, Pia, makampuni ya bima
yanawezasana kutoa huduma kwa washiriki pamoja na mapromota wa mchezo
huu.
Watanzaniahatuna
budi kuchangamkia fursa hizi zinazotolewa na mchezo huu unaopendwa sana
ulimwenguni. Mchezo huu mbali na soka ndio mchezo unaoweza kuingiza
pesa nyingisana kwa waandaaji, mabondia na wale wote wanaoshiriki.
Wenzetu kama Afrika yaKusini, Ghana, Namibia, Zambia wako mbali sana kwa
uwekezaji huu.
Napendakuwahimiza
watanzania watumie nafasi hii nzuri kujifunza na kuwekeza kwenyemchezo
huu. Shirikisho la Ngumi la Kimataifa IBF chini ya uongozi wangu
litakuwalinatoa semina mbalimbali kwa wadau wa mchezo huu ili waweze
kujua fursa zilizokona kuzitumia barabara!
Nafasiyangu
itaniwezesha kuipendelea Tanzania kwa kiwango kikubwa kwani “mtu ni
kwao” hivyo nadhamiria kuitumiafursa hii barabara!
Nitakuwana
ofisi za aina tatu. Moja nitakuwa na ofisi kwenye Shirikisho hili kule
NewJersey, Marekani kama kitengo kinachohudumia mabara (continents).
Nitakuwa naofisi nyingine kwenye nchi za Mashariki ya Kati (Middle East)
na Ghuba yaUajemi (Persian Gulf) kule Dubai, United Arab Emirates
(UAE).
Aidhanitakuwa na ofisi za shirikisho hili hapa kwetu Dar-Es-Salaam, Tanzania kuhudumianchi za bara la Afrika (Africa continent).
Ninaondokakwenda
kwenye mkutano mkuu wa mwaka kule Honolulu, Hawaii, Marekani
nikiwanimejiandaa vyema kuiwakilisha Tanzania. Tayari tumeshapata miadi
ya kukutanana balozi mbalimbali katika nchi za Afrika, Mashariki ya Kati
na Ghuba yaUajemi (ubalozi wa Tanzania jijini Washington DC ukiwa
mojawapo) ya kuzungumzianamna gani tutakavyoweza kushirikiana na
serikali zao kukuza “Sports Tourism” programambayo nina furaha kubwa
kuianzisha ndani ya IBF/USBA.
Karibunitushirikiane kuendelza mchezo wa ngumi.
Imetolewana:
OnesmoNgowi
Rais wa Shirikisho laNgumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi Cha Marekani (IBF/USBA)
Rais wa Shirikisho laNgumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi Cha Marekani (IBF/USBA)
Katika bara la Afrika,Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi
No comments:
Post a Comment