Ethan Miller/Getty Images
Jela inaweza kumfanya vipi mtu?
Kwa marehemu 2Pac ilimuwezesha kupasua
zaidi, na matokeo yake ilikuwa ni albamu kali daima ya disc mbili, All Eyez on
Me.
Kwa Wesley Snipes, imemuangusha ile mbaya
na kumhsusha umaarufu wake kwa haraka kuliko ilivyokuwa kwa Mike Tyson.
Kumzungumzia Iron Mike, kukaa kwake jela
kulimfanya awe mwenye hasira na aliyechanganyikiwa na dunia.
Jela inaweza kusababisha athari kubwa kwa
mtu anayekwenda kulala kwenye sero zake.
Kwa Floyd Mayweather anayetarajiwa kuishi
jela kwa siku 87 kuanzia Juni 1, mwaka huu kwa kosa alilofanya mwaka 2010 la
unyanyasaji, swali kubwa ni jinsi gani May Fedha atayakabili maisha ya jela.
Huku Money May akikadiriwa kuingiza kiasi
cha dola za KImarekani Milioni 40 kwa ushindi wake dhidi ya Miguel Cotto,
hajawahi kuwa maarufu duniani kwenye michezo kama ilivyo sasa. Anafahamu hili, anapenda, na amekuwa
akijitokeza kwenye vyombo vya habari na atahakikisha anadumu kwenye chati.
Hiki ni aina ya chumba cha jela ambacho Mayweather atakwenda kuishi.
Jinsi gani atakabiliana na maisha hayo?
Atakuwa jela wakati mpinzani wake mkubwa,
Manny Pacquiao atakuwa akipigana na Tim Bradley. Pacman atakuwa ameishika dunia
ya ngumi, wakati huo Mayweather anapanga foleni kwa ajili ya huduma za jela.
Ethan Miller/Getty Images
Atakuwa anatumiaje muda wake?
Atakuwa anazurura zurura tu muda wote,
lakini hilo ni wazo zuri? Bila uwezo wa kufanya mambo yake aliyozoea katika
maisha yake ya uraiani, atakuwa akifanya mazoezi.
Hiyo itakuwa ngumu? May Fedha aliongezeka
uzito kabla ya pambano lake na Cotto, na kama hatakuwa makini ataongezeka
zaidi. Wakati tukiwa hatujui mpinzani wake wa kwanza mara tu atakapotoka jela,
kama atakuwaPacquiao, spidi ulingoni litakuwa jambo muhimu kuliko nguvu.
Kisha tena katika rekodi ya mapambano 43
bila kupoteza hata moja, Mayweather ni mtu safi na anayechukuliwa vizuri;
hatakwenda kugombana ovyo kwa sababu hatakuwa na kitu cha kufanya.
Swali haswa kwa Mayweather, anaingia jela
akiwa katika chati ya juu. Alikuwa akizungumzia kustaafu baada ya kumpiga
Cotto, lakini tunajua bado hajaisha. Atapigana tena; swali pekee ni " nani
atakuwa mpinzani wake?
Mayweather 'atapigika' jela? Atakuwa na
hasira kuliko alivyo sasa? Kulingana na jinsi anavyoishi maisha yake sambamba
na Ms. Jackson na 50 Cent, anaonekana aliyeridhika na ana amani ya maisha. Je, hayo yatabadilika
akiwa jela?
Al Bello/Getty Images
No comments:
Post a Comment