Shirikisho
la Ngumi la Kitaifa bara la Afrika, mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi
(IBF) limetangaza kumvua ubingwa wa mabara katika uzito wa Junior Light
uliokuwa unashikiliwa na bondia Emmanuel Tagoe wa Ghana (Pichani).
Katika
kumvua ubingwa huo ambao Tagoe alikuwa autetee tarehe 26 May Rais wa
Shirikisho hilo barani Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi
bwana Onesmo Ngowi alisema kuwa Tagoe anavuliwa ubingwa kutokana na
kudanganya kwake kwenye vipimo vya afya!
Hii ni mara ya kwanza kwa Shirikisho hilo kumvua ubingwa bondia kwa madai ya kudanyanya kwenye vipimo vya afya!
Bondia
Emmanuel Tagoe alikuwa azipige na bondia Antonio De Vitis wa Italia
kugombea ubingwa wa Junior Lightweight May 26, mwaka huu!
Msimamizi
mkuu wa mpambano huo alikuwa Rais wa IBF katika bara la Afrika,
Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi. Ngowi pia
ni Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania na Mkurugenzi wa
Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC).
Hii
inawaweka mabondia wote katika hali ya hatari ya kuvuliwa ubingwa wao
endapo tu wataonekana kuwa wamedanganya katika vipimo vya afya zao.
Aidha, tabia ya mabondia wengi kutumia madawa ya kulevya inahatarisha
ushiriki wao katika mchezo wa ngumi.
Katika
msimamo wake huo Ngowi alisema kuwa ameuchukua uamuzi huo ili kutoa
fundisho kwa wale wote wanaofikiri kuwa udannganyifu hususan utumiaji wa
madawa ya kuongeza nguvu utawasaidia katika michezo.
Wanamichezo
wanatakiwa wajue kuwa vipaji, juhudi za kufanya mazoezi na kujituma
ndivyo pekee vitakavyowapa ushindi katika michezo na sio dawa za
kulevya.
Matumizi ya
madawa ya kuongeza nguvu yamepigwa marufuku hata michezo mbalimbali
kama Olympic, World Cup na mashindano mengi ya ya kitaifa na kimataifa.
Hili ni
fundisho rasmi kwa mabondia wa kitanzania wanaotumia madawa ya kulevya
kama bangi na mengine ili washinde katika mapambano yao. Kwa kazi hii
mchezo utabaki kwa wa wenye vipaji tu!
Imetolewa na
Kitengo cha Mahusiano (PRO)
International Boxing Federation Africa (IBF/AFRICA).
No comments:
Post a Comment