Tangazo

Pages

Saturday, May 12, 2012

MBUNGE WA KINONDONI IDD AZAN MGENI RASMI PAMBANO LA NGUMI LA UBINGWA WA TAIFA KATI YA MOKIWA NA KUMBELE MEI 20 UKUMBI WA VIJANA KINONDONI


MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azan, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika pambano la ngumi la Ubingwa wa Taifa katika Ramadhan Kumbele na James Mokiwa, litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Vijana uliopo Kinondoni Mei 20, mwaka huu.



Akizungumza na Mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, mratibu wa pambano hilo, Twalib Asenga, asema kuwa maandalizi ya pambano hilo yanaendelea vizuri, ambapo tayari Mbunge wa Kinondoni Idd Azan, amekwishathibitisha kuwa mgeni rasmi.


Mbali na maandalizi hayo pia siku ya pambano hilo kutakuwa na Burudani mbaimbali za kusindikiza pambano hilo.

Aliwataja baadhi yawasanii watakaotoa burudani siku hiyo kuwa ni pamoja na Msanii wa muziki wa Kizazi kipya wa miondoko ya Hip Hop, Kala Pina, Temba wa Kino, Chungai wa Kondoa na wengineo.

Aidha katika pambano hilo, wafanyabiashara wajasiliamali watapata fulsa ya kutangaza biashara zao katika meza 10, zilizoandaliwa kwa ajiliya wale watakaokamiisha taratibu za kujisajili na kumaliza malipo ya kiingilio.

Pia wajasiliamali hao kwa watakaowelipia jumla ya Sh. 200, 000, wataweza kutangaza biashara zao kupitia Projector zitakazokuwapo ukumbini hapo, na ikiwezekana katika DVD za Ngumi.

No comments:

Post a Comment