Tangazo

Pages

Friday, May 25, 2012

MABONDIA DIMOSO NA MROSO KUPSAMBANA JUNE 2 DDC KARIAKOO






Na Mwandishi Wetu


MPAMBANO wa masumbwi kufanyika june 2 mpambano huo ulioandaliwa na Zugo Promoter ni wa kirafiki utakao wakutanisha mabondia kutoka Arusha na Dar es salaam akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Zugo. Suleiman Zugo.


Alisema mabondia hawo ni George Dimoso wa Dar es salaam atakayepambana na Robert Mroso mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa DDC Kariakoo jijini Dar es salaam

Mpambano huo utakaotanguliwa na Ambukile Chusa atakaezichapa na Ysufu Jibaba, Emanuel Philimoni na Saidi Mbelwa,Abeid Zugo na Rashidi Nyagatwa na mpambano mwingine utawakutanisha James Martin na Ally Mahiyo


Katika mpambano huo kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazotolewa na wasanii aiza mchezo huo umeandaliwa kwa ajili ya kuinua mchezo wa masumbwi ili uweze kusonga mbele.


Zugo aliongeza kwa kusema wanatakiwa wafadhili wajitokeze kuzamini mchezo huo ili uweze kusonga mbele na kuliletea sifa taifa letu.
 Mbali ya kuwepo na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na
huuzwaji wa DVD za Mafunzo ya Mchezo wa Masumbwi wakiwemo mabondia Lenox Lewis,
Evander Holfiled,David Haye, Waldmil Klitichiko,Manny Paquaio, Floyd Maywether,
Roj Jones na wengine wengi

Zitakuwa zikisambazwa kwa ajili ya kuwapa

mabondia,mashabiki marefarii kutambua sheria na kanuni za mchezo huo Duniani
ambazo zimeandaliwa na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini, Rajabu
Mhamila Super D Alisema kuwa tangia aanze kutoa mafunzo kwa njia hiyo watu wengi wameanza kuwa na uwelewa wa mchezo wa masumbwi nchini kwa kutambua sheria na mambo mbalimbali ya mchezo alisema Super D boxing Coach ambapo mpaka sasa ameweza kutoa matoleo nane tofauti ya mabingwa wa ngumi Duniani Akichanganya na mabondia wa Nchini.

No comments:

Post a Comment