Tangazo

Pages

Tuesday, May 1, 2012

MASHINDANO YA KUSAKA 10 BORA WA MASUMBWI KUANZA MEI 4 MWAKA HUU


 Na Mwandshi Wetu

MASHINDANO ya kumi bora ya mchezo wa masumbwi yanatarajia kufanyika
mei 4 mwaka huu katika ukumbi wa Panandi Ilala Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Kocha wa kimataifa wa mchezo wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' alisema vijana wengi wamejitokeza kushiriki michuano hiyo yenye lengo la kupanga viwango vya mabondia.
Aliwataja baadhi ya mabondia watakaopambana siku hiyo kuwa ni pamoja na Ibrahim Class atakayezichapa na Idi Mnyeke, Amiri Macho na West Scorpion, Charo Issa na Hamis Nassoro,Athumani Sadara na Abuu Mtambwe, Hassan Mijugu ataoneshana Kazi na Saidi Ally, Sandari Nyambara na Pascal Ignus.
Super D aliwataka wadhamini kujitokeza kudhamini mashindano hayo ili kuweza kufikia malengo waliyokusudia.
Alitaja baadhi ya maitaji kwa siku hiyo kuwa ni maji kwa wachezaji wakati wa mchezo, zawadi za kuwatia moyo wachezaji pamoja na madawa mbalimbali yatakayotumika kwa ajili ya kuwapatia mabondia huduma ya kwanza.
Kwa yoyote mwenye nia ya kusaidi mashindano hayo kwa namna moja au nyingine anaweza kuwasiliana na kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli kwa namba ya simu 0655928298 au unaweza fika katika klabu ya Amana CCM iliyopo Ilala Dar es Salaam vilevile waweza kuwasiliana na kocha Super D 0713/0787-406938 au unaweza fika Klabu ya Ashanti Iliyopo Ilala Soko la Mitumba kwa mawasiliano zaidi
kwa maelezo zaidi tembeleawww.superdboxingcoach.blogspot.com

No comments:

Post a Comment