Tangazo

Pages

Tuesday, March 5, 2013

BINGWA WA NGUMI NA BINGWA WA KICK BOXER KUZICHAPA MACH 17




Bingwa wa kickboxing, Hamis Mwakinyo, anatarajia kupanda ulingoni kuzipiga na bingwa wa Taifa wa ngumi za kulipwa nchini uzito wa light weight kg 60, Said mundi, wa Tanga katika pambano la raundi nane.
SAIDI MUNDI KUSHOTI NA KING CLASS MAWE
Pambano hilo litakuwa ni maalum kwa ajili ya kusindikiza pambano la ubingwa wa mabara wa WBF kati ya Alan kamote na Jumanne Mohamed, litakalopigwa katika uwanja wa mkwakwani  jijini Tanga Machi 17, mwaka huu.
Hamis Mwakinyo ambaye ni bingwa wa ngumi na mateke afrika mashariki na kati wa  WKN-AFRIKA (World kickboxing Network- Afrika) na ameshawahi kuchalenji ubingwa wa dunia nchini iran, atazichapa na mpinzani wake huyo, ambapo pambano hilo linatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa. 
Aidha pambno hilo limezidi kuwa gumzo midomoni  mwa mashabiki wengi wa mchezo huo, mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa muandaaji wa pambano hilo Promota, Ally Mwanzoa, amesema kuwa mabondia  hao tayari wameshakubaliana na kuridhia kutiliana saini  mkataba wa makubaliano wa pambano hilo.
Mwanzoa, alisema kuwa pia kutakuwa na mapambano mengi ya utangulizi kwa  mabondia kutoka sehemu mbalimbali za  Tanzania hususani  jijini Dar es salaam na anategemea kuongeza nguvu  za majaji wa mchezo huo kutoka nje  ya Tanzania ili  kuondoa malalamiko yeyote yanayoweza kujitokeza.

Monday, March 4, 2013

Ndomba: Mkali wa ngumi anayeota makubwa kimataifa


Bondia Pascal Ndomba



Bondia Pascal Ndomba akiwa Marekani
WAKATI mabondia wengi nchini, wakiwamo wenye majina makubwa, wakilia juu ya mchezo wa ngumi kutowapa mafanikio ya kujivunia, kwa Pascal Ndomba hali kwake ni tofauti.
Bondia huyo anayefahamika zaidi kama 'Kimondo', anasema ngumi zimempa mafanikio ya kujivunia kiasi kwamba hajutii kuucheza mchezo huo.
Ndomba anasema mbali na ngumi kumwezesha kuzitembelea nchi mbalimbali duniani, lakini pia zimemfanya ajenge nyumba Kimara Suka, akimiliki kiwanja eneo la Mbezi Beach pamoja na kuitunza vema familia yake.
Bingwa huyo wa zamani wa Taifa wa TPBC na Afrika Mashariki na Kati, anasema na hivi karibuni ameingia mkataba nchini Marekani ambao unamfanya azidi kuuheshimu mchezo huo.
Anasema mkataba huo wa muda wa miaka minne aliingia mwishoni mwa mwaka jana na kampuni ya Nelson Boxing Promotion na umeanza kutumika mwaka 2013 hadi 2017.
"Ingawa ni kweli ngumi kwa hapa nchini na hata kanda ya Afrika Mashariki zimekuwa hazina tija kutokana na ubabaishaji uliopo, nashukuru Mungu zimenisaidia kwa mengi," anasema.
Anasema siri ya kufanikiwa kupitia mchezo huo ni kujitambua kwake na kuwa na nidhamu kwa kila senti anayoipata, huku akimwagia sifa 'bosi' wake Humoud M. Sumry, anayemfadhili.
"Bosi wangu Humoud Sumry, ndiye kila kitu kwangu kwa msaada anaonipa chini ya kampuni yake ya mabasi ya Sumry," anasema.


SIRI
Bondia huyo anafichua siri kwa kusema kuwa chanzo cha mabondia wengi nchini na hata Afrika kushindwa kufanikiwa kimaisha na kimichezo kupitia ngumi inatokana na ubabaishaji uliopo katika sekta hiyo.
Anasema mapromota na viongozi wa ngumi wamekuwa wakiwanyonya mabondia kwa kutumia udhaifu wao wa kuwa na elimu ndogo ama kushindwa kujitambua wapo katika mchezo huo kwa ajili ya nini.
Pia anasema kumekuwa na hila zikifanywa kati ya viongozi wa vyama na mapromota wa nje wa kutaka mabondia dhaifu ndiyo wapelekwe nje kuicheza na hata kama ni wakali basi hulazimishwa wacheze chini ya kiwango.

Pascal Ndomba akiwa nje ya nchi
"Hufanya hivyo kwa lengo la kutaka mabondia wao kuendeleza rekodi zao na ikitokea bondia anayepelekwa huko akashinda kama alivyofanya Karama Nyilawila basi huzua tafrani baina ya pande mbili zilizokubaliana," anasema.
Akaongeza hiyo ndiyo sababu inayofanya mabondia wengi wa Tanzania au barani Afrika kupigwa kila wanapoenda nje.
"Ni 'dili' tu zinazofanywa na baadhi ya watu wachache kwa tamaa za fedha," anasema.
Ndomba anayependa kula ugali au ndizi kwa nyama na kunywa Fanta, pia anasema mabondia wamekuwa wakidhulumiwa haki zao na baadhi ya viongozi wa ngumi kwa kuwapunja fedha za malipo tofauti na makubaliano.

Pascal Ndomba akiwa na 'bosi' wake, Humoud Salim
Anasema inawezekana bondia ameitwa kwenda kucheza nje kwa dola 5,000, lakini huishia kulipwa 3,000 au nusu ya hapo kwa kisingizio hiki na kile, wakati mwingine asipewe kabisa.
Bondia huyo aliyeingia kwenye ngumi kwa kuvutiwa na bingwa wa zamani wa dunia, Mike 'Iron' Tyson, anasema ni vema kungekuwa na utaratibu chini ya serikali kuhakiki mikataba na kujua kinachompeleka bondia nje ya nchi.
"Japo hizi ni ngumi za kulipwa, ni vyema kungekuwa na chombo cha namna hiyo kusimamia safari za mabondia nje kuepusha kudhulumiwa na kuichafua nchi nje kwa vile hupeperusha bendera ya taifa," anasema.

MATAJI
Ndomba, mume wa Ikupa aliyezaa naye watoto wawili, Michael (8) na Abel (5) wanaosoma Shule ya Msingi Makuburi, anasema alianza rasmi ngumi mwaka 1996 katika klabu ya Kiwira iliyopo Kyela Mbeya.
Kocha aliyemnoa anaitwa Said Tambwe na alishiriki michuano kadhaa ya ngumi za ridhaa na alipoona hazina tija yoyote, mwaka 2000 aliamua kuhamia ngumi za kulipwa.
Anasema akizcheza ngumi hizo aliweza kunyakua ubingwa wa mkoa wa Mbeya na kupata fursa ya kupigania ubingwa wa Taifa wa TPBC mwaka 2005 kwa kumpiga Fike Wilson.
Aliendelea kutoa vipondo kwa wapinzani wake kabla ya mwaka 2009 kutwaa taji la Afrika Mashariki na Kati kwa kumchapa kwa KO Mkenya Joseph Odhiambo.
Pia amewahi kuwania mikanda ya kimataifa inayotambuliwa na WBC, WBO na IBF, uzito wa Cruiser mara ya mwisho ikiwa Desemba, 2012 alipoenda Ghana kupigana na Mghana asiyepigika Braimah Kamoko na kunyukwa.

Pascal Ndomba (Kushoto) akichapana na Mghana Braimah Bamoko
Ndoto zake kubwa ni kuja kutwaa ubingwa wa dunia akiamini ana uwezo wa kufanya hivyo, pia akitamani kuja kumiliki gym na klabu ya kufunzia vijana mchezo huo.
"Napenda nije kuwafunza na kuwarithisha vijana kipaji changu, najua siwezi kusalia kuwa bondia milele," anasema.
Licha ya kucheza mapambano mengi, Ndomba analitaja pambano la kuwania ubingwa wa vijana wa IBF uzani wa 'cruiser' dhidi ya Mswisi, Agron Dzila, kuwa ndilo gumu kwake na asiloweza kusahau kwa 'kisago' alichoikipata.

CHIMBUKO
Pascal Ndomba alizaliwa mwaka 1983, Kyela Mbeya akiwa ni mtoto wa nne kati ya watano wa familia yao na alisoam  Shule ya Msingi Lema ya Kyela kabla ya kujiunga Tabora Boys kwa masomo ya Sekondari.
Tangu shuleni alipenda michezo, ila alivutiwa na ngumi na kujifunza kabla ya kuanza kuzipiga ulingoni na mabondia kama akina Bagaza Mwambene, George Sabuni, Hassani Matumla, Karama Nyilawila na Maneno Osward.
Ndomba anasema hana furaha mpaka atakapopanda ulingoni kupigana na Japhet Kaseba aliyenukuliwa hivi karibuni akidai amekuwa akikwepa na baadhi ya mabodnia kwa umahiri wake.
"Kwa kweli kiu yangu ni kuzichapa na Kaseba, dai lake kwamba amekuwa akikimbiwa na mabondia siyo kweli kwa vile nimekuwa nikiomba kucheza naye bila mafanikio," anasema.
Ndomba anayeiomba serikali itupie macho mchezo wa ngumi kwa madai umekuwa ukiiletea sifa Tanzania nje ya nchi kwa mabondia waliowahi kutwaa mataji ya kimataifa.

Pascal Ndomba (kushoto) akiwa kwenye kazi yake ya uwakala wa mabasi kituo cha mabasi cha Ubungo
Bondia huyo anayependa kusikiliza muziki na kuangalia runinga mbali na kucheza ngumi pia ni wakala wa kampuni ya mabasi ya Sumry, akiishabikia Simba na Manchester United, na anawazimia Shomari Kapombe na Patrick Evra.
Tukio la furaha kwa Ndomba, ambaye anamkubali sana bondia mkongwe Mbwana Matumla, ni siku mkewe alipojifungua mtoto wake wa kwanza mwaka 2005. "Tukio la huzuni nisilolisahau ni kifo cha baba yangu kilichotokea mwaka 2002," anasema.

Pascal Ndoma (kushoto) akiwa na wakala mwenzake wa mabasi ya Sumry

Sunday, March 3, 2013

BONDIA KASEBA ALIPO MSAMBALTISHA MANENO


Bondia Maneno Osward kushoto akipambana na Japhert Kaseba wakati wa mpamba
 no wao wa ubingwa wa taifa uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa Kaseba alishinda kwa point mpambano huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Japhert Kaseba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Maneno Osward wakati wa mpambano wao wa kugombea ubingwa wa taifa Kaseba alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Japhert Kaseba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Maneno Osward wakati wa mpambano wao wa kugombea ubingwa wa taifa Kaseba alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Japhert Kaseba akinyooshwa mkono juu na refarii Antoni Ruta baada ya kuibuka mshindi kwa kumgalagaza Maneno Osward picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Aliphonce Mchumiatumbo kushoto akioneshgana uwezo wa kutupiana masumbwi na Josephe Marwa mpambano wa uzito wa juu uliofanika jumamosi Mchumiatumbo alishinda kwa K,O raundi ya siti picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Putile Gama kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Tom Kato kutoka Japani anaeishi mjini Bagamoyo Kato alishinda kwa K,O raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Aliphonce Mchumiatumbo kushoto akioneshgana uwezo wa kutupiana masumbwi na Josephe Marwa mpambano wa uzito wa juu uliofanika jumamosi Mchumiatumbo alishinda kwa K,O raundi ya siti picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Tom Kato kulia  kutoka Japani anaeishi mjini Bagamoyo akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Putile Gama Kato alishinda kwa K,O raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MPAMBANO WA UBINGWA WA NGUMI KUFANYIKA MKWAKWANI TANGA

Pambano la masumbwi kutetea makanda wa mabara wa WBF(world boxing forum) wategemea kufanyika katika uwanja wa mkwakwani jijini  Tanga kwa  kuwakutanisha  Alan Kamote, ambae ni bingwa mtetezi wa  mkanda huo aliouchukua  nchini Malawi  kwa  kuzipiga na  Jumanne Mohamed  wa tanga  ambae anavyo vigezo  na sifa zote  za kuugombania ubingwa huo.
Jumanne Mohamed ambae alipata nafasi  ya kugombania  ubingwa  wa  dunia  nchini Namibia na kuipoteza kwa kupigwa na mnamibia  nafasi hiyo imejirudia tena,safari hii katika ubingwa wa mabara na kuugombania katika ardhi ya nchini mwake.
Muandaaji wa pambano hilo Ally Mwanzoa  akizungumza  na viongozi wa ngumi nchini pamoja na katibu mkuu wa ngumi za kulipwa  Ibrahim  kamwe  amesema ameamua kuandaa pambano hilo ili Alan kamote autetee  mkanda wake alioupata  Blantaya nchini Malawi usije ukapoteza kwa kutokuutetea ubingwa wake huo, na kukaa na uongozi wa ngumi  kwa kuangalia bondia gani  anafaa  na ikaamuliwa  jumanne Mohamed anafaa kutokana na sifa alizonazo na upinzani walionao  mabondia hao utaleta mshawasha na msisimko mkoani Tanga, kwa hiyo haina haja ya kumleta mtu kutoka nje ya nchi.mwanzoa aliendelea  kwa kusema pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi  kati jj ngotiko  na  haji juma wa Tanga katika pambano la raund kumi, na kutakuwepo na mapambno mengine mengi y a utangulizi.

Friday, March 1, 2013

KASEBA VS MANENO, MCHUMIATUMBO VS MARWA WAPIMA UZITO MPAMBANO JUMAMOSI MARCH 2 DDC KONDOA


Bondia Aliphonce Mchumiatumbo (kushoto) akioneshana umwamba na Josephe Marwa, Dar es salaam , baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa uzito wa juu utakaofanyika katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa  march 2 jumamosi PICHA NA www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Aliphonce Mchumiatumbo akipima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa uzito wa juu na Josephe Marwa utakaofanyika jumamosi ya  March 2 katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa
Josephe Marwa katikati akiwa na baadhi ya mabondia

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na mabondia Japhert Kaseba kulia,Josepher Marwa na Aliphonce Mchumiatumbo wa pili kushoto baada ya kupama uzito kwa ajili ya mpambano wa March 2
Bondia Maneno Osward akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa na Japhert Kaseba utakaofanyika March 2 katika kumbi wa DDC Magomeni Kondoa kulia ni Katibu wa PST Antony Luta ambaye alikua anasimamia zoezi la upimaji uzito Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na mabondia Japhert Kaseba kulia,Josepher Marwa na Aliphonce Mchumiatumbo wa pili kushoto baada ya kupama uzito kwa ajili ya mpambano wa March 2

Mabondia Japhert Kaseba kushoto akitunishiana misuri na Maneno Osward baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa utakaofanyika DDC Magomeni Kondoa Dar es salaam March 2 Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.comNa Mwandishi Wetu

BONDIA Maneno Osward ametamba kumchakaza mpinzani wake Japhert Kaseba kunako raundi za awali akizungumza na mwandishi wa habari hizi maneno maarufu kwa jina la Mtambo wa Gongo amesema yeye yupo fiti na anasubili hiyo March 2 katika ukumbi wa DDC Magomeni kondoa apate kumshikisha adabu 

Kaseba ni bondia mchanga sana kwangu nilimkaribisha katika masumbwi na sasa nitamstafisha masumbwi mimi mwenyewe kwa kipigo nitakacho mpa na atajua kwa nini nimepewa jina la mtambo wa Gongo

Katika mpambano huo kutakuwa na mpambano wa uzito wa juu kati ya Josefu Marwa na Alphonce Mchumiatumbo mpambano unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wa ngumi za uzito wa juu nchini 

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D
.

--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
  

BONDIA AMIR KHAN AMPANIA JULIO DIAZ APRILI 27



LONDON, England

“Diaz ni bingwa wa zamani wa Dunia na ni mpinzani hatari mno ulingoni. Najua atakuja ulingoni akiwa na silaha kamili za maangamizi nami nakuhakikishia niko tayari kwa lolote. Kasi yangu na ujuzi nilionao ulingoni, nguvu zake na uzoefu alionao, vinalifanya hilo liwe moja ya mapambano makali unayopaswa kuyashuhudia"

BONDIA Amir Khan amekiri kuisubiri kwa hamu Aprili 27, siku ambayo atarejea ulingoni kumvaa Julio Diaz kwenye ukumbi wa Motorpoint Arena.

Hilo litakuwa ni pambano la kwanza kwa Khan katika ardhi ya Uingereza, tangu alipokubali kichapo kutoka kwa Paul McCloskey jijini Manchester mwaka 2011.

Na Khan, 26 amethibitisha alivyoupania mpambano huo kurejesha heshima yake iliyotoweka ulingoni – huku akisema: “Aprili 27 unaelekea utakuwa usiku maalum.

“Imeshapita miaka miwili sasa tangu pambano langu la mwisho katika ardhi ya nyumbani na sitasubiri kupanda tena ulingoni na kufanya vitu adimu mbele ya mashabiki wangu.

“Diaz ni bingwa wa zamani wa Dunia na ni mpinzani hatari mno ulingoni. Najua atakuja ulingoni akiwa na silaha kamili za maangamizi nami nakuhakikishia niko tayari kwa lolote.

“Kasi yangu na ujuzi nilionao ulingoni, nguvu zake na uzoefu alionao, vinalifanya hilo liwe moja ya mapambano makali unayopaswa kuyashuhudia.

“Yeye anaweza kuwa na amawazo kama waliyonayo wengine, nina imani kuwa marejeo yangu katika ardhi ya Uingereza yatakuwa ya mafanikio makubwa ulingoni.”

Diaz, 33, hajawahi kupigana kwa raundi 12 tangu alipopokwa mkanda wa IBF – uzani wa  ‘light’ alipoumana na Juan Diaz mwaka 2007.

The Sun

Thursday, February 28, 2013

MNAMIBIA KUUMANA NA MGHANA UBINGWA WA IBF.


  Albinus (kushoto) akifanya vitu vyake
 Thursday, February 28, 2013 - Dar-Es-Salaam, TANZANIA- Siku kubwa na yenye matumaini mapya katika maisha ya bondia wa Namibai Albinus Felesianu (9(4)-2(1)-0) itawadia hivi karibuni wakati atakapokutana na bodia Herbert Quartey (10(7)-8(6)-0) wa Ghana kugombea ubingwa wa IBF wa dunai uzito wa Unyoya (Featherweight). Albinus alipata mshtuko mkubwa sana na kushangzwa na habari za hivi karubunI kuwa IBF imempa nafasi ya kugombea ubingwa wa dunia wa vijana jambo lililomfanya apate furaha ya ajabu. Albinus Felesianu Albinus (kushoto) akifanya vitu vyake Mtu pekee atakayeweza kuzima furaha yake na kumfanya asiweze kufikia malengo yake katika ngumi ni bondia Herbert Quartey kutoka Ghana ambaye ni moja kati ya mabondia wenye ujuzi mubwa wa kupigana ulingonI. Kama inavyosemwa kuwa "mtoto mtukutu aliyepotea kwenye ngumi anapoomba kurudi kundini na kukaa kufuata kanuni na shaeia za ngumi mchezo wa ngumi humpokea kwa shangwe na nderemo na kumpa mawaidha na ushauri wa kumwendeleza" ndivyo hivyo hivyo Albinus Felesianu na Herbert Quartey watakavyopokelewa na ngumi baada ya pambano lao la tarehe 29 Machi jijini Windhoek, Namibia. Bondia Albinus Felesianu yuko chini ya promosheni ya Kinda Nangolo ambaye anamiliki kampuni tanzu ya Kinda Boxing Promotion na ni promota anayeinukia kwa kasi sana katika tasnia ya ngumi nchini Namibia na barani Afrika