Monday, October 29, 2012
MCHEZO WA MASUMBWI, TAA INAYOZIZIMA – SEHEMU YA KUMI NA TISA
■UNAPENDWA
NA KUOGOPWA NA WATU WENGI DUNIANI
■UKO
HATARINI KUPOTEZA ASILI YAKE KABISA
Na Onesmo Ngowi
Masumbwi au kwa majina mwengine ndondi au ngumi na kwa
majina ya mitaani ndogwa, mawe n.k. ni mchezo unapoendwa sana na watu wengi.
Aidha mchezo huu ni kati ya michezo inayoogopwa sana duniani. Mchezo wa ngumi
uko hatarini kupoteza maana yake ya asili yaani kucheza kama burudani,
kuwakilisha nchi na kujenga ushupavu wa mchezaji. Mamilioni ya watu wanaojazana
kuutazama wasingependa kabisa kujiingiza kuucheza mchezo wa ngumi. Sasa
endelea………………………………….!
Ari ya kucheza gumi ya Duran na kiu chake cha kupata
fedha nyingi zilimfanya apande uzito kwenda Welter. Miaka ya sabini
ilimshuhudia Roberto akipata ushindi wa uhakika kwa kuwanyuka vilivyo mabondia
kama Carlos Palomino ambaye alikuwa bingwa wa zamani wa dunia wa welterweight
aliyetambuliwa na WBC) na Zeferino“Speedy” Gonzales. Ikumbukwe kwamba mabondia
hawa wawili walikuwa kati ya kundi lililokuwa tishio kwenye uzito wa Welter!
Kuingia kwa Duran kwenye uzito huu hasa ikikumbukwa
kuwa alikuwa anamfuata mbabe mwenzake Sugar Ray Leonard ambaye tayari
alishajijengea sifa kibao kwenye daraja hilo kulitafsiriwa kuwa ni kiama kwa
mabondia wengine. Wachezeshaji kamati wengi (Betting Houses) walingojea kwa
hamu habari za kutangazwa kwa mpambano utakaowakutanisha miamba hiyo miwili!
Ilifiki siku ya siku ambayo kila mpenzi wa masumbwi
duniani alikuwa anaingojea kwa hamu. Tarehe na mahali pa mpambano wa mwaka
ilipangwa nayo ilikuwa si pengine ila Uwanja wa Olimpiki jijini Montreal mahali
ambapo Sugar Ray Leonard alijipatia medali ya dhababu ya Olimpiki mwaka 1976.
Mpambano huu kama walivyoelezea wanazuoni wa maaswala
ya ngumi uliwakutanisha mbabe wa ngumi wa miaka ya sabini na bingwa wa miaka ya
baadaye, miaka ya themanini pamoja nao alikuwepo pia bondia machachari toka
Mexico Julio Cesar Chavez.
Sugar Ray
Leonard ambaye ndiye aliyekuwa bingawa wa dunia wakati huo baada ya kumshushia
kipigo kisichokuwa na wasiwasi mbabe toka Puerto Rico, Wilfred Benitez. Hakika
Ray Leonard alikuwa ndiye kipenzi cha vyombo vingi ya habari na hakuna
aliyeamini kama mbabe huyu angepoteza ubingwa wake kwa “mikono ya mawe” (Hands
of Stone) toka Panama City!
Kupendwa kwake Ray Leonard na vyombo vya habari pamoja
na wachezesha kamari (Betting Houses) zilimpa shinda Duran na alijiona kama
anapamana na mataifa yote ya American ya Kaskazini ambayo ni Marekani na
Kanada.
Mgao wa fedha za mpambano nazo zliichemsha harisa ya
Duran na akajiona kwamba kumbe kweli kulikuwa hamna haki kwake. Ray Leonard
alikuwa ndiye achukue zaidi ya robo tatu ya kitita cha mpambano ukilinganisha
na cha Duran ambacho kilikuwa ni robo tu. Haya yote yalimchukiza sana Duran na
aliapa kwamba angemuulia Ray Leonard ulingoni!
Hasira za Duran kwa Ray Leonard hazikuwa ndogo, kwani
wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari alimtukana na kumkebehi kama kweli
alikuwa mwanamme. Alienda mbali hata kumtukana mkewe Juanita!
Haya yote yaliongeza msisimko wa mpambano na mashabki
wengi wa ngumi walingojea kuuona moto utakaowashwa kwa mikono ya miamba hiyo
miwili! Lengo la Duran kumshambuliwa Ray Leonard lilikuwa kumtibulia ili
asiweze kufikiria vyema na baadaye kumtoa nishai ulingoni.
Mshikemshike wa Montreal “Brawl in Montreal” wa tarehe
20th, Juni 1980
ndivyo mpambano huu ulivyopewa jina na vyombo vingi vya habari na ulingojewa na
kila mtu anayependa ngumi.
Ilikuwa ni siku ya mvua nzito na japokuwa kulikuwa na
baridi kwani kipindi cha baridi ndio kilikuwa kinaishia maelfu kwa maelfu ya
wapenzi wa ngumi waliohudhuria bila manunguniko kwani walijikuta wakisisimka
kutokana na mpambano huo mkali wa aina yake.
Kama kawaida yake Ray Leonard ambaye kwa maumbile
ndiye aliyekuwa mkubwa alianza kwa kuutumia vilivyo ukumbwa wa ulingo kwa
staili yake ya kurukaruka na kuchezacheza. Mashabiki waliufuatilia mwendo wake
wa madaha kwa kelele za muue, muue huyo Mpanama Ray!
Naye Duran alikuwa anamfuata Ray Leonard kwa usongo wa
kummaliza kama mtu aliyepagawa na akitaka kuugeuza mpambano wenyewe uwe vita ya
msituni.
Hakika hii ndiyo iliyokuwa staili Duran aliyoizoea
kwani mapambano yake mengi yalikuwa hayana tofauti na mapigano ya kwenye vita
vya msituni. Kwake mpambano wowote ulikuwa ni vita kwelikweli!
Usongo wa kurusha makonde kwa kinyongo na ushambuliaji
mkali wa Duran uliweza kumpatia raundi ya kwanza bila shida. Hii ilimpa nafasi
ya kujipongeza na kujipa moyo kwamba kumbe kelele za Ray Leonard hazikuwa kitu
chochote. Lakini kwa maelfu ya mashabiki waliojazana kwenye ukumbi huo wa
Olimpiki mjini Montreal kwao raundi hiyo ilikuwa ni kama asusa tu ya mpambano
huo wa mwaka!
Kwa usemi usemeo kwamba “siku njema huonekana asubuhi”
ilidhihirisha na ushindi wa raundi ya mwanzo uliompa joto Duran akaingia raundi
ya pili kama mnyama aliyetaka kukitafuna kitoweo chake sawasawa. Kwa uhakika
raundi ya pili ilikuwa ni kipigo kikali kwa Ray Leonard kwani mwishioni mwa
raundi Duran alimpambikizia Ray Leonard konde zito linaloiwa “right-left combo”
likifuatliwa na ngumi aina ya hook ya mkono wa kushoto iliyoingia barabara
usoni mwa Ray Leonard.
Uzito wa konde hilo la Duran kwenye uso wa Leonard
ulileta wasiwasi kwenye kona yake na japokuwa Ray Leonard alitingisha kichwa na
kuchezacheza lakini ukweli ni kwamba kila mtu alijua kuwa amepewa kibano cha
uhakika. Watu wengi hususan mashabiki wa ngumi waliojazana kwenye ukumbi huo
walianza kushuku kama kweli Ray Lenaord angeweza kumaliza mpambano huo!
Baada ya kupewa kibano kwenye raundi hiyo Ray Leonard
aliamua kutumia sehemu ya ndani ya ulingo ambayo asingeweza kuangushwa kirahisi
na makonde ya mbabe wa Panama City kwa kweli hiyo ilimpa nafasi ya kuuonyesha
ulimwengu uwezo aliokuwa nao kwenye ngumi!
Baada ya raundi kumi na nne za kuadhibiana vikali watu
wengi walioona wazi kuwa Duran angeshinda mpambano huo na kwa kweli hata yeye
mwenyewe aliona uwezekano huo! Mikono ya mbabe huyo toka Panama City
yalirindima kwa ushuhuda wa kusukuma makonde ya mfululizo yaliyokuwa yanaingia
barabara kwenye uso wa Ray Leonard. Ilikuwa ni muda tu ulimwengu utambue kweli
nami mbabe kati yao!
Mwanzoni mwa raundi ya kumi na tano na ya mwisho Duran
alikataa kugusana glovu na Ray. Ni kawaida ya mabondai wanapofikia kucheza raundi
ya mwisho kugusanisha glovu kuonyesha kuwa wao ni wanamichezo na sio maadui.
Lakini kwa Roberto Carlos Duran hii kwake ilikuwa ni vita na mtu aliyesimama
mbele yake Sugar Ray Leonard alikuwa adui namba moja! Alilazimishwa na refarii
wa mpambano huo Carlos Padilla kugusanisha glovu!
Raundi hii
ilimshuhudia Duran akimkebehi Ray Leonard kwa makonde ya mpapatiko (telling
punches) na ulizi uliomnyina nafasi kabisa ya kufikisha ngumi zake kwa Duran.
Ikumbukwe kwamba kwa sababu ya tofauti ya lugha Duran alishikwa sana na hasira
kuwaona mashabiki wengi wakipiga kelele.
Duran
alikuwa anazungumza kugha ya Kihispania wakati sehemu yenyewe Montreal
alikopigania kunazungumzwa lugha za Kiingereza na Kifaransa. Kelele za
mashabiki zilimzidishia hasira Duran kwani hakuelewa kama walikuwa wanamtukana
au kumshangilia.
Inaendlea…..!
Mwandishi wa makala haya
ni; Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Shirkisho la Ngumi
za Kulipwa Afrika Mashariki na Kati (ECAPBF), Shirikisho la Ngumi la Kimataifa
bara la Afrika, Masharilki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi (IBF/AFRICA) na
Mkurugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) E-mail: ibfafrica@yahoo.com
Saturday, October 27, 2012
RASHID MATUMLA NA PATRICK AMOT WA MKENYA KUZICHAPA KESHO MTWARA, WAPIMA UZITO LEO
Bondia Rashid Matumla na Patrik Amot wa kenya wanategemea kupanda ulingoni kesho katika ukumbi wa makonde mkoani mtwara.
Mabondia wote wamepima na kuwa na afya njema na wote kuwa katika uzani sawa wa kilo 73 kila mmoja.zoezi zima la upimaji liloendeshwa na katibu mkuu wa TPBO Ibrahim Kamwe na Dkt. Madono lilienda vema.
Pia katika pambano hilo kutakuwa na mapambano ya utangulii kati ya Bakari Mohamed wa Mtwara na Abdallah Mohamed wa Dar es Salaam, katika pambano la ubingwa kg57.
Aidha kutakuwa na mapambano mengine mengi ya utangulizi kati ya mabondia kutoka Black Mamba ya Mtwara na mabondia kutoka jijini Dar es Salaam, kama Haruna Mnyalukolo, ambaye atacheza na Ashraf Abdallah, Issa Matumla (mtoto wa Rashid Matumla) atacheza na Hamis Mtupeni, Hamis Ali Mkupa wa Mtwara atacheza na Ide Mnali katika pambano la raundi nane.
Mabondia wakiendelea na zoezi la kupima uzito, leo.
HABIBU KINYOGOLI AENDELEA KUMKUMBUKA MWALIMU NYERERE KATIKA MICHEZO
MWALIMU Julius Kambarage Nyerere kipindi yuko madarakani,
alipenda michezo kuanzia mashuleni hadi kwenye makampuni na mashirika
mbalimbali hapa nchini, ingawa alikuwa akipenda mchezo wa bao.
Aliweka sera bora ya michezo na kufanikisha
kuundwa kwa Baraza la Michezo la Taifa mwaka 1967 na kutoa fursa zaidi kwa wenye
vipaji kuvionyesha.
Kwa mujibu wa bondia mahiri wa Ngumi hapa
nchini, Habibu Ally Kinyogoli (64), Nyerere alifanikisha wachezaji wa Tanzania
kuitangaza zaidi nchi yetu na kufanya vizuri kutokana na mazingira bora
yaliyokuwako wakati huo.
Kinyogoli ni mwanachama wa Mabingwa wa Ligi Kuu
Tanzania bara, Simba lakini hahudhurii michezo ya timu hiyo, mapenzi yake
yanabaki kwenye ngumi.
Nyota yake ya michezo ilianzia shuleni,
Manerumango Wilayani Kisarawe mkoani Pwani, mwaka 1958, alicheza soka, ngumi na
riadha, aliendelea na mchezo wa ngumi kwa sababu ndio ulikuwa ndani ya damu
yake, michezo mingine ilimshinda kwa sababu ya hasira za baadhi ya wachezaji
pindi zinapotokea rafu.
Kinyongoli wakati alipokuwa akicheza, alikuwa
pia akitoa mafunzo kwa wenzake, mwaka 1966, katika klabu ya Magomeni Centre
yalipo makao Makuu ya Manispaa ya Kinondoni alimfunza Majuto Mahavu ambaye
baadae alikuwa tishio kwenye timu ya Taifa.
Mwaka 1970 alijitosa rasmi kwenye ngumi baada ya
kuvutiwa na Titus Simba aliyeiletea medali ya kwanza Tanzania ya Jumuiya ya
Madola iliyofanyika Scotland, ndipo na yeye akaongeza ufanisi zaidi katika
mchezo huo.
Mwaka 1971 aliajiriwa kiwanda cha Bora baada ya
kuonesha umahiri katika mchezo huo, akafanikiwa kumfudinsha ngumi, Zakaria
Yombayomba, mwaka 1973 aliasisi klabu ya ngumi ya Urafiki akawaibua akina
Charles Mhilu ‘Spinks’, Habibu Mzungu, Lazaro Makarious, Kwelu Msinjili na
wengineo.
Mwaka 1972 alishiriki mashindano ya Olimpiki,
Munich Ujerumani walikwenda na akina Titus Simba, Robert Mwakosye, Bakari
Suleimani ‘Match Maker’, Said Tambwe katika mashindano hayo, mwanariadha Clever
Kamanga aliipa Tanzania medali ya shaba kwa mbio za umbali za mita 400.
Katika mashindano hayo, Kinyogoli alifanya
vibaya baada ya kukatika kwa mshipa wa mkono wa kulia katika mazoezi nchini
humo, mchezo wa kwanza wa Olimpiki alishinda kwa pointi nyingi dhidi ya
Mcambodia, mchezo wa pili alipoteza pambano baada ya kujitonesha mkono wake na
damu zikatoka nyingi.
Maumivu hayo hakuyaona hadi, Profesa Philemon
Sarungi wakati huo alikuwa akisoma nchini humo, alijitolea kuisaidia timu hiyo.
Mwaka 1973 alishiriki All Africa Games jijini
Lagos Nigeria akarejea na medali ya fedha na kuchaguliwa kwenye timu ya Afrika
iliyoshiriki Inter-Continental
iliyofanyika Mexico , uteuzi huo pia uliwahusu pia akina Jacob Mussa,
Bakari Suleimani, Titus Simba na Mbaraka Mkanga wakati katika soka Tanzania
iliwakilishwa na akina Maulid Dilunga, Abdallah Kibadeni na Kitwana Manara.
Mwaka 1974 alisisi klabu ya Simba ambayo kipindi
hicho ilikuwa ikiongozwa na Mwenyekiti, Abubakar Mwilima baada ya kuchana
mkataba wa Bora, baada ya uongozi mpya wa kiwanda hicho kutokupenda michezo,
akaondoka na wenzake wote aliokuwa nao kiwandani hapo kama Bakari Suleiman
‘Match Maker’, YombaYomba na wengineo.
1976 akiwa
kwenye kambi ya maandalizi ya
Olimpiki alitangaza kujiuzulu kuchezea timu ya Taifa, mwaka 1978
akaanzisha
klabu za watoto wadogo ya Relwe na kuendelea na Simba, Simba
wakachipukia akina
Rashid Matumla, Iraq Hudu Mkumwena,Rajabu Mhamila 'Super D' Shabani
Mhamila 'Star Boy, Remmy Ngabo, Joseph Marwa,mohamedi Chipota na
wengineo.
Hivi sasa,
Kinyogoli anafundisha klabu ya
Amana ya Ilala akisaidiwa na Kocha wa kimataifa wa mchezo huo Rajabu
Mhamila 'Super D' kocha Mohamedi Chipota, Kondo Nassoro na Sako Mtulya
na akiendelea na Simba pia akiwa na changamoto nyingi ambazo
ni uwezeshwaji wake kutoka kwa wadau mbalimbali kwa sababu ameutengeneza
mchezo
huo tangu alipokuwa akifanya kazi na alitumia gharama zake lakini sasa,
kazi
hafanyi. Ametoa wito kwa mashirika na watu binafsi waliokuwa na nia ya kumsaidiakuendeleza mchezo wa masumbwi nchini kuja katika kambi ya Ilala Iliyopo
Amana CCM ambapo ana endesha darasa la vijana kujifunza na kujiendeleza kwa
mchezo uho au anaweza kuwasiliana moja kwa moja na habibu Kinyogoli kwa
simu namba 0655928298
Friday, October 26, 2012
BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' APANIA KUWA BINGWA WA TAIFA
Hali hiyo inadhihirika kwa kijana Ibrahim Class 'king Class
Mawe' ambaye anafanya vizuri katika medani za ngumi ambazo zinamsaidia
kuinua kiwango chake.
Tangu aingie katika mchezo huo ameshiriki katika mashindano mengi
na kufanya vizuri na kusababisha wadau mbalimbali wa masumbwi kumtabilia
kufika mbali mbali ikiwa atazingatia mazoezi.
King Class anasema alishawishika kuingia katika mchezo huo kutokana
na mapenzi aliyokuwa nayo tangu utotoni ambapo alikuwa na ndoto za kuwa
mwanamasumbwi.
Anasema kuwa ndoto yake ilianza kutimia baada ya kaka yake naye
anaeitwa Chaku Master kuwa mwanamasumbwi alikuwa akifanya vyema miaka
kadhaa iliyopita.
Chaku nilikuwa nikiishin naye hivyo wakati anakwenda kufanya
mazoezi nilimuomba kuongozana na hali iliyonifanya kuanza kucheza licha
ya kuwa ni ndoto yangu ya siku nyingi, anasema King Class.
Kocha wake wa kwanza kufundisha kucheza ngumi alikuwa ni mzee Babu
Tule ambaye alimpa misingi ambayo inamfanya hadi kuwa bondia mzuri
anaeshimu nidhamu na sheria za mchezo huo.
Mwaka mmoja baada ya kuwa na kocha huyo alimuamishia kwa
kocha Mkongwa Habibu Kinyogoli ambapo hapo alikutana na makocha wengi
akiwemo kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila
'Super D' ili kumpa mbinu zaidi za mchezo huo na kumjenga katika
misingi thabiti ya kufikia ndoto za kifikia mafanikio.
Anasema mwaka 2006 baada ya kuwa chini ya kocha wa siku nyingi
katika mchezo huo Kinyogoli kiwango chake kinakuwa kikiongezeka kila
siku na kuwa tishio katika ngumi za amacha.
Class anasema tangu wakati huo amepambana mapambano mengi ambao
alifanya vizuri na kumbukumbu yake inaonesha alifanikiwa kuwatwanga
wapinzani kwa KO katika mapambano zaidi ya 10, ndicho kitu anachojivunia
kwa sasa.
"Huwa najisikia faraja ninampompiga mtu kwa KO kwani inazidi
kunijengea heshima katika ngazi ya amacha ambayo ndiyo niliyopo kwa sasa
ambayo nahisi sina mpinzani," anasema Class.
Anasema siri kubwa ya kufanikiwa kufanya vizuri katika mapambano
yake ni kutokana na kuzingatia mazoezi, miiko, sheria na kanuni za
mchezo huo ambazo kila siku huwa anaelekezwa na kocha wa Kinyogoli.
Chipkizi huyo katika masumbwi anasema kila bondia anaweza
kufanya vizuri ikiwa atajihidi kusimama imara kuzingatia yanayokatazwa
katika mchezo huo.
"Moja ya vitu ambavyo avitakiwi ni uvutaji wa sigara na utumiaji wa
dawa kulevya ikiwemo Bangi na dawa nyingine ambazo ufanya kuwa na
uhamuzi usio sahihi," anasema Class.
Class anasema ikiwa bondia atatumia Sigara au akivuta bangi ufanisi
wake unakuwa mdogo kutokana na kifua kuwa kizito na kushindwa kumaliza
raundi za mchezo au anaweza kupigwa kwa KO.
Hivyo anawashauri mabondia ambao wanajihusisha utumiaji wa tumbaku
kuhachana na tabia hiyo ili kufikia malengo waliojiwekea katika
masumbwi.
Pia anasema unywaji wa pombe nayo ni sehemu inayonyong'onyesha
viungo, ikiwa bondia atahitaji kufanya vizuri ni vyema akaepiuka
utumiaji wa pombe.
Kingine anasema kuwa suala la uzinzi nalo ni tatizo kwa baadhi ya
wanasumbwi na ndiyo sababu kubwa inayowafanya kushindwa kufanya vyema
ulingoni na kuambulia kupigo kikali.
Hivyo anawaomba wanamasumbwi chipukizi na wakongwe kujiepusha na
hanasa hizo ambayo zinarudisha nyuma harakati za maendeleo ya mchezo huo
nchini.
Kijana huyo aliyemaliza taehe 10/10/1990 na kupata elimu yake ya msingi katika Shule ya msingi Mafinga mwaka 2000, mkoani
Iringa anasema licha ya kujihusisha na masumbwi pia ni fundi wa vifaa
vya umeme ikiwemo pasi, TV, Friji,specer na vifaa vyote vinavyotumia umeme.
Anasema ili kuundeleza mchezo ni bora vifaa
vikatolewa kwenye klabu mbalimbali zinazoinua mchezo huu kwa vijana
wadogo ambao mara wamekuwa wakitatizwa na nyenzo za kufanyia mazoezi.
King
Class Mawe kwa sasa aliemia katika ngumi za kulipwa na kufanya vizuri
katika mapambano yake ya awali ikiwemo kumtwaga bondia Sako Mwaisege kwa
K,O ya raundi ya tatu na kufanikiwa kumdunda bondia mkongwe wa mchezo
huo Jonas Segu kwa point na kufanikiwa kuweka rekodi yake ya masumbwi
kuwa nzuriBondia huyo kwa sasa yupo kambini kwa ajili ya mpambano wake na bondia kutoka Tanga Said Mundi utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam
King Class Mawe kwa sasa yupo chini ya kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuakikisha kipaji chake kinakuwa na anapata michezo mbalimbali hapa nchini na matarajio yake ni kuwa bingwa wa Taifa na bingwa wa Dunia kupitia mchezo wa Masumbwi
--
Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Mob;+255787 406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
shabani kilumbelumbe vs imanuel naidjala
bondia chipukizi mtanzania shabani kilumbelumbe tarehe 13-11-2012 anatarajiwa kupanda ulingoni jijini windhock- namibia kuzipiga na bondia immanuel naidjala -the prince- wa namibia katika pambano la raundi 12 kugombea ubingwa wa WBO-AFRICA .
Pambano hilo ni la uzito wa bantam-kgs 53.5 na litafanyika katika ukumbi wa windhock country club resort.
promota wa pambano hili ni NESTOR TOBIAS wa NESTOR SUNSHINE BOXING AYA NCHINI NAMIBIA.
TPBO tayari imeshapata barua ya mwaliko kutoka chama cha ngumi na mieleka cha namibia na mktaba wa bondia pia umeletwa kwa TPBOkupitia wakala wa pambano hili ndg julius odhiambo wa kenya .
tayari meneja wa bondia huyu kilumbelumbe mwalimu HATIBU ameshapewa taarifa kuhusu bondia wake kukabiliwa na pambano hili chini namibia.
TPBO INAMTAKA MENEJA WAAKE KUMUANDAA BONDIA WAKE VYEMA KWA AJILI YA PAMBANO HILO ILI AKAFANYE VYEMA.
TPBO IMECHOSHWA SANA NA MAJIGAMBO YA MABONDIA WA KITANZANIA AMBAO HUPATA MIALIKO YA KWENDA KUPAMBANA NJE YA TANZANIA
LAKINI KILA WAKIENDA HUKO HUDUNDWA NA WARUDIPO HUWAKIMBIA WAANDISHI WA HABARI ILI WASIHOJIWE JUU YA KUDUNDWA KWAO.
NAWATAKA MABONDIA WA KULIPWA WAACHE KUONGEA SANA NA BADALA YAKE WAJIANDAE VYEMA KWA MAPAMBANO YAO
BY -YASSIN ABDALLAH -USATAADH
RAIS-TPBO
MBABE WA RAJABU MAOJA KUTETEA MKANDA WAKE DECEMBA 1
Bondia kutoka nchini Namibia Gottlieb
Ndokosho ambaye alimsambaratisha Mtanzania Rajabu Maoja katika raundi ya
kwanza ya mpambano wao wa kugombea mkanda wa IBF Afrika katika uzito wa
unyoya, atapanda tena ulingoni jijini Windhoek, Namibia kutetea mkanda
wake kati ya mabondia watatu ambao walipendekezwa na IBF.
Pambano
hilo litakalofanyika katika jiji la Windhoek nchini Namibia utatoa
upinzani mkali sana kati ya mabondia hao wanaochipukia vyema.
Kati ya majina matatu yaliyopendekezwa na
IBF limo jina moja na Mtanzania Fredy Sayuni ambaye anaishi jijini
Dar-Es-Salaam. Wengine ni Patric Okine kutoka Ghana na David Kiilu
kutoka nchini Kenya.
Wakati huo huo IBF
imetoa kibali kwa bondia Helene Joseph wa Nigeria kutoka barani Afrika
kupigania ubingwa wake wa dunia. Mpambano huo utawakutanisha Helen
Joseph kutoka nchi ya Nigeria akikutana na bondia Dahianna Santana
kutoka Dominican Republic huko Latin America ambaye ndiye bingwa wa
dunia wa IBF katika uzito wa unyoya (featherweight) kwa upande wa
wanawake.
Helen Joseph
Mpambano
huo utafanyika Decemba 1 katika jiji la San Domingo na litasimamiwa na
Rais wa IBF kutoka bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba za Uarabu na
Uajemi, Mtanzania Onesmo Ngowi.
Picha ya (kulia) Bondia Santana kulia, akiwa ulingoni.
Bondia
Helen Joseph ameshapigana mapambano 13 na amepoteza moja wakati
mpinzani wake Dahianna Santana amepigana mara 37 na kupoteza mara 6.
*Uongozi*
*IBF Africa, Masharikim ya Kati, Ghuba za Uarabu na Uajemi*
*Dar-Es-Salaam*
Subscribe to:
Posts (Atom)



