Tangazo

Pages

Monday, April 8, 2019

HOMA YA MPAMBANO WA PASAKA DAY KATIKA UKUMBI WA CCM MWINYIMKUU WAPAMBA MOTTO

Na Mwandishi Wetu

zikiwa zimebakia siku chache kabla ya mpambano wa masumbwi wa kumaliza ubishi kati ya Hussein Pendeza na Juma Ramadhani Choki siku ya April 21  Pasaka Day mabondia hawo wamendelea na mazoezi yao kama kawaida kwa ajili ya siku hiyo ya
Mpambano uho ulioandaliwa na Promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa pambano hilo litafanyika siku ya sikukuu ya pasaka likiwa limepewa nguvu na 

Bondia Mtanzania Omari Kimweri 'Lion Boy 'anaefanya shughuli zake nchini Australia  bondia huyo ndie aliesababisha mabondia hawo wazipige siku hiyo kwa kuwa vijana wanatakiwa kuendeleza rekodi zao za masumbwi kila wakati ndio mana akaongeza nguvu ili mpambano uho ufanyike



Super D aliongeza kwa kusema kuwa mbali na pambano hilo siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali yatakayokuwa yanafanyika siku hiyo ambapo bondia  Idd Mkwera ataoneshana umwamba na Rojas Masamu na  Shomari Milundi ataoneshana umwamba na Bakari Mbede wakati ibrahimu Makubi atavaana na Haruna Ndalo na Ramadhani Mbegu 'Migwede' atakabiliana na Rashidi Mnyagatwa na Salum Tandu zidi ya Gerald Mkude na Sunday Kiwale 'Moro Best' atalindima na Luckman Ramadhani Vicent Mbilinyi na Shabani Mbogo Hussein Shemdoe na Shehe Azizi na Ahmadi Kombo atakumbana na Sandali Nyambala

Mapambano yote hayo yanaletwa kwenu na kampuni tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion ambayo ipo nchini Tanzania kwa ajili ya kuinuwa vipaji ya vijana mbalimbali ili kuendeleza vipaji vyao pendwa


na kupitia kampuni ya Super D Promotion imejizatiti kuweka angalau pambano moja kila baada ya miezi milili ili kuwasaidia vijana mbalimbali kukuza vipaji vyao na kujiendeleza kupitia mchezo uho wa masumbwi nchini

No comments:

Post a Comment