Tangazo

Pages

Monday, May 16, 2016

MABONDIA WA TANZANIA WALIVYOWAADHIBU WAGENI JANA TAIFA




Bondia wa Tanzania, Francis Miyeyusho (kushoto) akimchapa konde bondia wa Uganda, Ben Sajjabi katika pambano lisilo la ubingwa uzito wa Super Bantam usiku wa jana Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam. Miyeyusho 'Chichi Mawe' alishinda kwa Knockout (KO) raundi ya raundi ya pili
Ben Sajjabi akiwa amelala chini baada ya kuchapwa ngumi ya uzito wa juu na Chichi Mawe
Bondia Thomas Mashali (kulia) wa Tanzania akimchapa konde Sajad Mehrabi wa Iran katika pambano la uzito wa Super Middle usiku wa jana kuwania ubingwa wa dunia wa UBU. Mashali alishinda kwa pointi
Mashali na Mehrabi wakionyesha ujuzi wa mchezo wa ngumi usiku wa jana Uwanja wa Taifa
Mashali na Mehrabi walipigaa kwa taundi 12 katika pambano kali na la kusisimua
Bondia Allan Kamote wa Tanzania (kushoto) akiwa amemchapa konde Salim Chazama wa Malawi katika pambano la uzito wa Light jana. Mabondia hao walitoka sare
Bondia Ramadhani wa Tanzania (kulia) akimchapa konde Osgood Kayuni wa Malawi (kushoto) katika pambano la uzito wa Welter. Shauri alishinda kwa pointi
Bondia Saleh Mkalekwa wa Tanzania (kushoto) akikwepa ngumi ya Mkenya, James Onyango (kulia) katika pambano la uzito wa Welter jana kuwania ubingwa wa UBO. Mkalekwa alishinda kwa pointi
Bondia Shaaban Kaoneka (kulia) akiwa amemchapa konde Mtanzania mwenzake, Hassan Mwakinyo (kushoto) katia pambano la Super Welter kuwania ubingwa wa PST. Kaoneka alishinda kwa Knockout (KO) raundi ya tano
Bondia Nassib Ramadhani wa Tanzania (kulia), akimuadhibu Remmy Iga wa Uganda usiku wa jana Uwanja wa Taifa katika pambano la uzito wa Super Bantam

No comments:

Post a Comment