Tangazo

Pages

Friday, November 13, 2015

MABONDIA HAMISI MWAKINYO NA MESHACK MWANKEMWA KUPIGANA KESHO JUMAMOSI

Bondia Hamisi Mwakinyo kushoto akitunishiana misuli na Meshach Mwankemwa baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa taifa unaotambuliwa na  Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBC  katikati ni promomota kutoka katika kampuni ya Golden boy Afrika Shomari Kimbau Picha na SUPER D BOXING NESW

Bondia Hamisi Mwakinyo kushoto akitunishiana misuli na Meshach Mwankemwa baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa taifa unaotambuliwa na  Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBC utakaofanyika kesho katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala katikati ni promomota kutoka katika kampuni ya Golden boy Afrika Shomari Kimbau akiwa na mkanda utakaogombaniwa Picha na SUPER D BOXING NESW

Mabondia Hamis Mwakinyo na Meshack Mwankemwa wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa KG 66 utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Mwijuma mwananyamala Dar es salaam jumamosi Picha na SUPER D BOXING NESW

Bondia Joyce Awino akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Asha Nzoa kushoto mpambano utakaofanyika kesho katika ukumbi wa CCM Mwijuma Dar es salaam kulia ni Rais wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa Picha na SUPER D BOXING NESW

Bondia Asha Nzowa kushoto akitunishiana misuli na Joyce Awino baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa kesho utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala Picha na SUPER D BOXING NESW

Promota Shomari Kimbau akiwainua mikono juu mabondia Asha Nzowa kushoto na Joyce Awino baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho

Rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa akiwakumbusha baadhi ya sheria zitakazo tumika katika mchezo wa ngumi utakaofanyika kesho katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala Dar es salaam

NA Mwandishi Wetu

MABONDIA Meshack Mwankemwa na Hamisi Mwakinyo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa kg 66 unaotambuliwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchi mkanda uho uliokuwa umeachwa wazi na bondia Selemani Zogo kwa kuto utetea kwa wakati sasa utapiganiwa na mabondia hawo kesho

akizungumza wakati wa upimaji wa uzito promota wa mpambano uho Shomari Kimbau amesema mkanda uho utapiganiwa na mabondia hawo ili apatikane bingwa mpya wa uzito wa kg 66

mpambano uho utasimamiwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini chini ya rais wake Chauremba Palasa aliongeza kwa kusema mbali na mpambano uho siku hiyo pia kutakuwa na ngumi za utangulizi za mabondia mbalimbali

Said Mayanga atamenyana na Gido Selemani wakati Mohamed Amir atapambana na Hemed Hemed

na mpambano mwingine wa kusisimua utakuwa ni wa akina mama ambapo bondia mnaschachali Asha Nzowa 'Asha Ngedere' atapambana na Joyce Awino ambambao ambao unasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wanawake wa mchezo wa masumbwi  

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment