Tangazo

Pages

Thursday, June 4, 2015

BONDIA MRISHO RAJABU 'DAME' ATAMBA KUMCHAKAZA ABDALLAH PAZI JUNE 14 BAGAMOYO

Na Mwandishi wetu
Bondia Mrisho Rajabu 'Dame' amempania kumchakaza katika raundi za awali bondia Abdalla Pazi 'Mfalme wa Wazalamu' katika mpambano wao wa raundi sita utakaofanyika katika ukumbi wa TASUBA uliopo Bagamoyo mjini juni 14

Rajabu amesema atahakikisha awapi tabu majaji kwa kumsambalatisha kwa K,O ya raundi za awali wakati wa mpambano wao ambao umevuta isia za watu wengi wa Dar es salaam na mkoa wa Pwani

siku hiyo pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambapo Iddi Pialali 'Simba aliyejeruiwa' atapambana na Sweet Kalulu

wakati Raymond Mbwago atavaana na Halidi Honga na mchezo mwingine mkali zaidi utawakutanisha Mfaume Mfaume wa Manzese na Adam Ngane wa Chanika  pamoja na mipambano mingine mbalimbali 

siku hiyo pia kutapambwa nja burudani kutoka kwa Jumanne Iddi pamoja na Sam wa Ukweli watakaopamba jukwaa hilo kwa ajili ya burudani za muziki wa kizazi kipyaa 

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment