NA MWANDISHI WETU
KUNA kitu wengi hawakielewi kuhusu Floyd Mayweather Jr. Tangu aanze kucheza ngumi za kulipwa hajawahi kupoteza, lakini tangu aanze kupanda ulingoni amepigwa mara moja tu na aliyeifanya hii kazi anapatikana katika mji wa Pazardzhik, Bulgaria. Unamjua ni nani?
Anaitwa Serafim Rorodov. Kwa kumtazama usoni hivi sasa inaweza ikawa ngumu kwako kuamini ulichokisoma hapo juu, lakini ukiyapitia vizuri mashindano ya Olympic mwaka 1996 yaliyofanyika Atlanta, Marekani utatikisa kichwa chako na kutoa heshima kwake.
Kwa sasa Todorov anaishi pamoja na
mke, mtoto wake wa kiume na binti wake wa kike ambaye ni mjamzito. Maisha yake ni ya chini mno na hakuna kilichobora kwenye maisha yake zaidi ya rekodi ya kumchapa kisiki Floyd Mayweather japo mwenyewe amekuwa akichukizwa mara kwa mara kila anapokumbushiwa suala hili. Kwanini? Ilikuwa akampiga Mayweather? Makala haya yamekusanya majibu yote ya maswali hayo.
Ushindi wa Todorov alioupata enzi hizo akiwa na umri wa miaka 27 mbele ya Mayweather aliyekuwa na miaka 19 kwenye pambano la uzito mwepesi katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Olympic mwaka 1996, ndio pigano la mwisho Mayweather kupoteza ulingoni.
Miezi michache baadae baada ya kichapo hiko, Mayweather aliachana na ngumi za ridhaa na kuingia kwenye mapambano ya ngumi za kulipwa alipotengeneza rekodi ya kucheza michezo 47 bila kupoteza mpaka sasa na kutengeneza mamilioni ya pesa.
Kwa Todorov mwenye miaka 45 sasa, kuna tofauti kubwa ya kimaisha baina yake na Mayweather tangu mara ya mwisho wawili hawa walipopambana.
Mayweather aliyepoteza pambano anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola milioni 280 wakati Todarov aliyeibuka kidedea hamiliki hata ‘flat screen’ sebuleni kwake. Hali hii ndio inayomtia simanzi Todorov kila siku.
Kwa kipindi kirefu mashabiki wa masumbwi hususani Wamerakani wamekuwa wakiuponda ushindi wa Todorov wakidai kuwa majaji wa pambano lao walimpendelea.
Lakini hili ni kama halimuumizi kichwa sana Todorov, kinachoonekana kumtatiza ni namna maisha yake yalivyobadilika tangu alipotoa kichapo hiko cha Kihistoria miaka 19 iliyopita.
Mikosi ilianza kumuandama baada ya pambano lile ambapo Todorov alitemwa na shirikisho la masumbwi hali iliyomfanya ashindwe kuliwakilisha taifa lake katika mapambano ya kimataifa.
Wakati leo hii Mayweather akijiandaa kupokea dola milioni 180 kwa pambano lake dhidi ya Pacquiao, Todorov anaishi kwa kutegemea pensheni ya dola 435 kwa mwezi.
Hali hii inamfanya Todorov, binadamu pekee aliyemchapa Mayweather ulingoni kuamka kila siku asubuhi na kujuta kwanini alishinda pambano hilo.
“Alikuwa na miaka 19 kumbuka, uzoefu wangu ulingoni ulikuwa mkubwa zaidi yake. Nilishawachapa mabondia mbalimbali kutoka Urusi, Cuba, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza” alisema Todorov
“ Lilikuwa pambano zuri na la kuvutia, unahitaji kuwa vizuri zaidi ya mwenzako ili kupata ushindi. Mimi nilikuwa vizuri kwa siku ile”aliongeza bondia huyo.
Todorov bingwa mara mbili wa Ulaya katika ngumi za ridhaa alianza kujifunza ngumi akiwa na miaka 8 akipata mafunzo kutoka kwa mjomba wake katika kitongoji cha Peshtera, kusini mwa jiji la Pazardzhik, Bulgaria.
Udhaifu pekee wa Todorov ambao kocha wake Georgi Stoimenov, aliueleza ni kuwa, mbali na uhodari wa bondia huyo ulingoni ni mbovu sana kwa wanawake.
“ Tukiwa kwenye mashindano, kocha unatakiwa kulala chumba tofauti na kijana wako. Lakini kwangu ilikuwa lazima nilale nje ya mlango wa Todorov kwa ajili ya kumlinda” alisema kocha huyo.
Stoimenov aliongeza kuwa kuna kipindi alilazimika kumfungia Todorov kwa nje, lakini alipoamka asubuhi alimkuta ametoroka chumbani kwa kupitia dirishani.
Unajua Stoimenov alimpatia wapi Todorov? “ alimkuta mklai huyo akiwa amejifungia kwenye kambi ya wanawake waliokuwa wakishiriki riadha.
Hatahivyo Todorov anakubali kuwa Mayweather ni bondia mkali lakini kwa upande wake hakutumia muda mwingi kumchunguza kabla ya kupanda nae ulingoni.
“ Nilikuwa bondia niliyekamilika sana. Sikuwa na muda kumsoma. Nilipomtazama ulingoni kwenye pambano lake la robo fainali, ilitosha sana kwangu kuona udhaifu wake na kumchapa” alisema Todorov.
“ Lakini ukweli halikuwa pambano la kawaida, nilimpiga mmoja kati ya mabondia bora kabisa ulimwenguni.” Aliongeza Todorov.
Kuhusu hali ya maisha yake ilivyo hivi sasa, Todorov amekiri kuvurugika na akichukua zaidi kuwa na rekodi hiyo ambayo kwa sasa dunia inamtazama kwa sana.
“ Kwenye maisha, ni kawaida kushinda vitu vichache na kushindwa na vitu vingi. Nachukia na ninajutia kuwa na rekodi ya aina hii kwenye maisha yangu” alisema Todorov.
Sababu kubwa inayodaiwa kusababisha mapromota kumkumbia Todorov na kuanza kuweka pesa kwa Mayweather, ni kitendo cha mkali huyo kudengua mara kwa mara katika kusaini mikataba.
Lakini mmoja wa watu waliokuwa wakifanya kazi na bondia huyu, Angel Angelov, anasema kuwa maisha ya Todorov yalibalika tangu alipopokea kichapo kutoka kwa Kamsing.
Angel anaamini kuwa Todorov bado ana mawazo ya pambano lile ambalo aliamini ni wazi kuwa majaji walimkandamiza ili apoteze pambano lile.
“ Nakumbuka Todorov alikuwa karibu ya kuchanganyikiwa baada ya raundi ya kwanza ya pambano lile. Alifoka kwa hasira kwa kocha wake akimwambia kuwa majaji hawahesabu ngumi zake” alisema Angel ambapo mwisho wa siku Todorov alipoteza pambano hilo kwa pointi 8-5.
Baada ya kichapo hiko, Todorov alitumia siku mbili akiwa hotelini akisubiri ndege ya kumrudisha kwako.
“ Sitaacha kunywa pombe kwa maisha yangu yote, na ninataka kifo change kinikute nikiwa na pombe” alisema Todorov anayehisi maisha yake yametawaliwa na usaliti.
Kwa sasa Todorov anaishi katika kibanda kilichozungukwa na mashamba ya ya ndizi eneo linalofahamika zaidi kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya nchini Bulgaria.
“ Kuna mambo ya ajabu zaidi mahala hapa, mambo mengi mabaya yanaendelea mahala hapa. Sipendezwi na maisha haya. Hakuna sehemu za mafunzo ya ngumi za kutosha, siongei na watu wengi wa hapa na kwa sasa sihitaji zaidi marafiki. Nahitaji kupumzika tu” alisema Todorov.
Todorov anaamini kama angepoteza pambano lile la Mayweather, angeendelea vyema na mchezo huo kama alivyofanya kwenye michuano ya Olympic.
Pia anaamini kabisa asingepata nafasi ya kuishi Marekani alikokutana na fedheha ya kichapo cha uonevu mbele ya Kamsing. “ Yameshatokea, na nimeshasahau. Kwa sasa nahitaji kuishi na kusahau yaliopita. Kuna mambo ya kipuuzi niliyafanya na nilipokuja kugundua tayari nilishadumbukia shimoni”
Kuhusu rekodi yake ya kumchapa Mayweather kama bado watu wanaikumbuka, Todorov alisema “ Wanakumbuka, lakini huwa sipendi kusikia ninapopota mtaani watu wakisema, Yule ndiye mtu aliyewahi kumpiga Mayweather”.
No comments:
Post a Comment