Tangazo

Pages

Tuesday, February 18, 2014

NGUMI KUAMIA KISARAWE APRIL 26

Bondia Mbaruku Heri kushoto akimkabidhi barua ya maombi ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi katika Wilaya ya Kisarawe Mwenyekiti wa halimashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adam Ng'imba
ambapo imepagwa April 26 kutakuwa na ngumi za wazi kwa ajili ya kuhamasisha mchezo huo uliopotea wilayani humo wengine wa pili kushoto ni Masudi Bakari na Saidi Chaku picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mwenyekiti wa halimashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adam Ng'imba kushoto akitaniana na Masudi Bakari mara baada ya kuletewa barua kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa ngumi Wilayani humo Jana ambapo imepagwa April 26 kutakuwa na ngumi za wazi kwa ajili ya kuhamasisha mchezo huo uliopotea wilayani humo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mwenyekiti wa halimashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adam Ng'imba
Bondia Mbaruku Heri kushoto akimvisha gloves Mwenyekiti wa halimashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adam Ng'imba wengine kulia ni Masudi Bakari na Said Chaku
mara baada ya kuletewa barua kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa ngumi Wilayani humo Jana ambapo imepagwa April 26 kutakuwa na ngumi za wazi kwa ajili ya kuhamasisha mchezo huo uliopotea wilayani humo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI  wa halimashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adam Ng'imba amepokea maombi ya kuhamasishwa mchezo wa masumbwi katika halimashahuri hiyo baada ya mchezo huo kufutuka kwa kipindi hiki

Maombi hayo yaliyopelekwa na kamati ya kufufua mchezo wa masumbwi Kisarawe ikiongozwa na Bondia Mbaruku heri, Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' pamoja na wadau wengine wa masumbwi nchini Saidi Chaku na Masudi Bakari ambao wamepereka barua hiyo kwa ajili ya kurudisha hamasa ya mchezo wa masumbwi

akizungumza mara baada ya kusoma maombi yaliyopo katika barua hiyo alijibu kwa kusema nimepokea kwa moyo mmoja maombi haya na ngumi zitapigwa kama zamani nakumbuka mabondia wengi akiwemo Habibu Kinyogoli 'Masta' ametokea hukuhuku Kisarawe na mkumbuke kuwa bondia wa ngumi za ridhaa anaetamba kwa sasa na aliyetuwakilisha katika mashindano ya Olimpic yaliyomalizika hivi karibuni Selemani Kidunda naye anatoka hapa hapa katika wilaya ya Kisarawe hivyo tunaweza  kuhakikisha ngumi zinarudia enzi zake

na naku aididi ngumi hizi zitapigwa katika viwanja vya wazi ili kila mtu ashudie mchezo wa ngumi unavyorudi upya katika wilaya hii naomba wapenzi mashabiki wa mchezo wa masumbwi wakae mkao wa kula siku ya April 26 ngumi zitapigwa katika uwanja wa bomani ili kila mtu ajionee mwenyewe

aliongeza kwa kusema ataendelea kutafuta wafadhili ili walete hamasa ya mchezo wa ngumi katika wilaya hiyo ambayo imejinyakulia umaarufu mkubwa mpaka sasa kupitia mchezo wa ngumi nita akikisha tunanunua vifaa vya mchezo ili vijana wapate kuendelea kushiriki mazoezi na atimae waje kurudia enzi za Kinyogoli

nae mkuu wa msafara wa kuhamasisha mchezo wa ngumi katika wilaya  hiyo, Mbaruku Heri amesema atakikisha siku hiyo analeta vijana wengi wakali wanaotamba katika ulimwengu wa masumbwi kwa sasa kama vile Ibrahimu Class 'King Class Mawe',Hamza Mchanjo,Thobias Adaut, Husein Pendeza,Said Uwezo,Adamu Ngange,Ambokile Chusa,Georgr Dimoso,Twalibu Mchanjo na wengine wengi wanaofanya vizuri katika ulimwengu wa masumbwi kwa sasa   


No comments:

Post a Comment