Gottlieb Ndokosho akinyanyua mkanda wake
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BONDIA Gottlieb Ndokosho kutoka nchini Namibia aliyemchapa kwa
KO bondia Rajabu Maoja wa Tanzania, atapanda tena uliongoni Februari 2 mwaka
huu katika jiji la Windhoek, nchini Namibia kupambana na bondia Prosper Ankrah
kutoka nchini Ghana.
Wawili hao watapambana katika mpambano wa mwaka wakati
Ndokosho wakati atakapotetea mkanda wa IBF wa bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi
na Mashariki ya Kati katika uzito wa unyoya. Ndokosho aliupata mkanda huo
tarehe 29 Septemba 2012 wakati alipomshinda Mtanzania Rajabu Maoja katika
mpambano uliofanyika katika ukumbi wa SPK jijini Windhoek, nchini Namibia.
Akizungumzia mpambano huo, Rais wa Shirikisho la Ngumi za
Kimataifa Afrika (IBF) na Ghuba ya Uajemi,
Onesmo Ngowi, alisema pambano lingine Namibia litawakutanisha mabondia
Albinus Felesianu wa Namibia atakapopambana na bondia Asamoah Wilson kutoka
nchini Ghana katika uzito wa Super Featherweight.
Wakati huo huo bondia mkali wa Tunisia Ayoub Nefzi mwenye
makao yake nchini Belgium atapambana na bondia Ishmael Tetteh wa Ghana kugombea
mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati (IBF
AMEPG)
Bondia anayekuja juu kwa kasi wa Ghana Richard Commey
atachuana na Mgahana mwenzake Bilal Mohammed kugombea mkanda wa IBF katika bara
la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.
Mpambano huu utafanyika sambamba na ule utakaowakutanisha
Mtanzania Fadhili Majia na Isaac Quaye wa Ghana. Mtanzania mwingine Allen
Kamote atapimana nguvu na bondia machachari na bingwa wa WBA wa mabara Emmanuel
Tagoe wa Ghana siku hiyo hiyo tarehe 22 Februari.
Naye bondia mwana dada Helen Joseph wa Nigeria atapambana na
bondia Mariana Gulyas wa Hungary kugombea mkanda wa IBF wa mabara katika uzito
wa Unyoya. Mpambano wa wanadada hao utafanyika katika jiji la Accra, nchini
Ghana tarehe 30 mwezi wa March, 2013.
Hili litakuwa pambano la kwanza kwa bondia Helen Joseph
tangu apoteze pambano la IBF la ubingwa wa dunia nchini Dominican Republic
alipokutana na bondia Dahianna Santana wa Domoinican Republic.
Mapambano hayo yote yatasimamiwa na Rais wa IBF katika bara
la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi.
No comments:
Post a Comment