Ndugu waandishi ,na wadau wakuu wa mchezo wa ngumi za kulipwa tanzania.
hivi karibuni mbunge wa kinonondoni ndg iddi azani aliwakabidhi vifaa vya mchezo wa ngumi mabondia wa ngumi za kulipwa nchini ,
ni jambo la kupongezwa sana hasa inapotokea wabunge kuanza kuona umuhimu
wa kusaidia wanamichezo bila ubaguzi wa aina ya michezo.
imekuwa ni jambo la kawaida sana ktk nchi yetu ya tanzania kuona wabunge
na makampuni mbalimbali yakitowa misaada ya vifaa vya michezo kwa
upande wa mpira wa miguu tu ,na si jambo la kawaida kwa wabunge hata
makampuni kuona wakitowa misaada ya vifaa kwa wanamasumbwi ,IDD AZAN
umefunguwa ukurasa mpya na TPBO inaamini kabisa kwamba mfano wako
utaigwa na wabunge wanzako.
TPBO inakutuma rasmi mara uingiapo bungeni uishawishi serikali ya
jamhuri ya tanzania ibadil sera zake za michezo ,kwa KUTAMBUWA RASMI
MICHEZO ya kulipwa ili watanzania wapate ajira zaidi kupitia michezo.
mpaka sasa hakuna taasisi yoyote ya ngumi za kulipwa inayoweza kujinadi
na kujigamba eti wao ndiyo wamepewa mamlaka na serikali ya kusimamia
ngumi za kulipwa nchini tanzania ,
kwa sababu hata ktk orodha ya vyama vya michezo vinavyotambuliwa na
baraz la michezo la taifa ,ni BFT tu ndiyo inayotambuliwa kwa ngumi za
ridhaa tu.
na ngumi za kulipwa hazimo ktk orodha hiyo, hivyo hata hizi taasisi
tulizonazo zimetokana na ubunifu wa watu tu kuziunda ili kuwasaidia
vijana kuishi kwa nguvu kazi michezo.
TUNAHITAJI IDDI AZAN AWE MWAKILISHI WETU BUNGENI KWA KUISHIONIKIZA
SERIKALI ITAMBUWE MICHEZO YA KULIPWA NA HATIMAYE SERIKALI IUNDE BOXING
BOARD OF CONTROL AMBAKO TAASISI ZOTE ZA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TANZANIA
ZIWAJIBIKE KWA BOARD OF CONTROL itokeapo kutokuelewana miongoni mwa
taasisi hizi.
NA NI BUDI WAANDISHI MJUWE WAZI KATIKA TAASISI HIZI ZA NGUMI ZA KULIPWA MPAKA SASA ZINATAMBULIWA KWA MSAJILI ALIYEZISAJILI TU ,
HIVYO IELEWEKE WAZI HAKUNA TAASISI YEYOTE ILIYO NA MAMLAKA JUU YA
TAASISI NYINGINE ,WALA HAKUNA SERA YA SERIKALI YA MICHEZO ILIYOIPATIA
NGUVU TAASISI NYINGINE ETI NDIYO ISIMAMIE NGUMI ZA KULIPWA , KWANI SERA
YA SERIKALI YA MICHEZO BADO HAIJABADILISHWA ,NA INATAMBUWA MICHEZO YA
RIDHAA TU.
IMELETWA KWENU NA
YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA--- USTAADH
RAIS -- TANZANIA PROFESSIONAL BOXING ORGANISATION -TPBO
WPBF -USBC -world professional boxing federation -representative to TANZANIA
No comments:
Post a Comment