Rais wa TPBC, Onesmo Ngowi |
Shirikisho
la Ngumi Tanzania (BFT) na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC}
zimekubaliana kuunda Kamati ya watu kumi (lO) ili kufufua na kuundeleza
mchezo wa ngumi Tanzania.
Kamati
hiyo ambayo itajumuisha wajumbe watano (5) kutoka BFT na watano (5)
kutoka TPBC itakuwa chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais wa TPBC,
Godfrey Madaraka Nyerere, ambayo itajulikana kwa jina la 'Kamati ya Nyerere ya Kufufua na Kuendeleza Ngumi Nchini'
'Kamati ya Nyerere ya Kufufua na Kuendeleza Ngumi Nchini' itafanya kazi ya kuandika hadidu rejea za rasimu ya makubaliano ya pande zote mbili ili ziweze kutumika kama mwongozo wa makubaliano hayo.
Ushirikiano kati ya BFT na TPBC utaratibiwa na Katibu Mkuu wa BFT Makore Mashaga pamoja na Katibu Mkuu wa TPBC Nemes Kavishe.
Wawili
hawa watakuwa ndio wakuu wa Sekretariet ya 'Kamati ya Nyerere ya
Kufufua na Kuendeleza Ngumi Nchini', ambacho ndicho chombo cha kusimamia
na kuratibu makubaliano haya.
Ushirikiano
kati ya vyama hivi viwili ambavyo kimoja kipo kwenye ngumi za ridhaa na
kingine kipo kwenye ngumi za kulipwa ni ushirikiano unaolenga kubadili
mwelekeo wa mchezo wa ngumi Tanzania.
Kwa
muda mrefu sasa mchezo wa ngumi umekuwa ukikumbwa na matatizo
mbalimbali ambayo yamepelekea kutokuwepo na maendeleo yanayotegemewa na
wadau wa ngumi Tanzania.
Ushirikiano
wa vyombo vyote vinavyoratibu ngumi nchini Tanzania utakuwa ni msingi
imara wa kujenga ari ya maendeleo ya ngumi kwa Tanzania.
Tanzania
imekuwa ikivurunda kwenye mashindano ya kimataifa karibu kila michezo
ya kimataifa na hivyo ushirikiano wa vyombo hivi viwili vya ngumi
utakuwa ndio msingi imara wa kuendeleza na kuondoa aibu hiyo ya muda
mrefu ya mchezo huo Tanzania .
No comments:
Post a Comment