NDG WAANDISHI WA HABARI- MICHEZO
NI MASIKITIKO YANGU MAKUBWA SANA NINAPOONA JINSI BAADHI YA VIONGOZI
WENZANGU WA NGUMI ZA KULIPWA [ SIYO ONESMO NGOWI ] JINSI WANAVYO
WAPOTOSHA BAADHI YA MABONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA ,KIASI CHA KUWAFANYA
WAJENGE TABIA ZA KUDHARAU MABONDI WENZAO.
MNAMO MWEZI WA SABA MWAKA HUU 2012 WAPENZI WA NGUMI ZA KULIPWA
WALIINGIZWA KTK MGOGORO MKUBWA WA MAWAZO PALE LILIPOTANGAZWA PAMBANO
KATI YA BONDIA FRANCIS CHEKA NA JAPHET KASEBA,
KATIKA HALI YA KUUSHANGAZA ULIMWENGU WA MASUMBWI NA WAPENZI WAKE KUINGIA
KTK FADHAA KUBWA ,BAADA YA KUMUONA BONDIA FRANCIS CHEKA KUPITIA VYOMBO
VYA HABARI AKIPIMA UZITO NA AFYA KWA AJILI YA PAMBANO LAKE LA TAREHE
07-07-2012 PALE UWANJA WA TAIFA NA KISHA KUGOMEA KUPAMBANA KWA KIGEZO
AMBACHO HAKINA NAFASI KATIKA TARATIBU ZA NGUMI ZA KULIPWA.
KTK MAELEZO YAKE CHEKA ANADAI NA BADO ANAENDELEA KUMPONDA KASEBA KUPITIA
VYOMBO VYA HABARI[BAADHI]KWAMBA KASEBA NI KIBONDE NA ANA POINT 13 TU NA
YEYE AKIWA NA POINTS 90. KWA KWELI UTARATIBU WA KUDHARAULIANA WAKATI
HAKUNA PAMBANO LINALOWAHUSU ,HAUPO- NA INARUHUSIWA TU WAKATI WA
KUTANGAZA PAMBANO LINALOWAHUSU MABONDIA HUSIKA NA,BAADA YA PAMBANO
KWISHA UHUSIANO MWEMA UNADUMISHWA NA KUENDELEA KAMA KAWAIDA.
NDG WAANDISHI KWANZA NI LAZIMA MJUWE KWAMBA KUPANDA KTK UBORA WA VIWANGO
KWA BONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA ,NI BUDI BONDIA AMBAYE REKODI YAKE NI
NDOGO APATE NAFASI YA KUPAMBANA NA BONDIA MWENYE REKODI BORA.ILI
AONYESHE UWEZO WAKE
NA IWAPO BONDIA MWENYE REKODI NDOGO ATABAHATIKA KUMSHINDA BONDIA MWENYE
REKODI BORA ,BASI HUYU BONDIA MWENYE REKODI NDOGO ATAPANDISHWA KWENYE
VIWANGO ,NA POINTS ZAKE ZITAPANDA VILEVILE KUWA NYINGI, NA POINT ZA
HUYU BONDIA MWENYE REKODI BORA ATASHUSHWA KTK VIWANGO NA POINT PIA.
NA IWAPO BONDIA MWENYE REKODI BORA NA PONT NYINGI AKISHINDA YEYE
HAONGEZEWI KITU BALI ATABAKI NA POINT ZAKE ALIZOKUWA NAZO NA ATABAKIA
KTK NAMBA ILEILE ALIYONAYO KTK VIWANGO .
NDIYO MAANA HAPO JUU NIMESEMA KWAMBA SABABU ALIZOZITOWA BONDIA FRANCIS
CHEKA HAZINA NAFFASI KABISA KTK NGUMI ZA KULIPWA BALI ALIHOFIA KUWA
ENDAPO ANGEPOTEZA PAMBANO HILO BASI ANGEKUWA AMEMPANDISHA KATIKA VIWANGO
BONDIA JAPHET KASEBA .
MUHHAMAD ALI-THE GREATEST
BONDIA MAARUFU DUNIANI MOAHAMED ALI, ALIPOANZA KUPIGANA NGUMI ZA
KULIPWA HAPO TAREHE 29-10 -1960 KTK UKUMBI WA FREEDOM -HALL STATE FAIR
GROUND-USA ,PAMABNO LAKE LA WANZA ALILIPAMBANISHWA NA BONDIA TUNNY
HUNSURKER
RAIA WA MAREKANI ,NA MKAZI WA FAYELLEVILLLE, WEST VIRGINIA-USA
NA WAKATI HUO HUYO TUNNY HUNSAKER ALIKUWA TAYARI AMEPAMBANA MAPAMBANO
1SHIRIN NA TANO [25] AKIWA AMESHINDA MAPAMBANO 15 AMEPOTEZA 9 NA SARE 1 ,
[ingia boxrec.com -then search -andika tunny last name hunsaker] UTAONA REKODI YAKE YOTE NA ALIOPAMBANA NA MOHHAMD ALI UTAONA.
SASA KAMA TARATIBU HIZO ZA KUMKATAZA MABONDIA WENYE POINT NYINGI KUCHEZA
NA WENYE POINT CHACHE ZINGEKUWEPO BASI HATA HUYU MUHAMMAD ALI
TUJINGEMJUWA . NA ASINGEJULIKANA
JAPHET KASEBA
TAREHE 02 -10 -2009 FRANCIS CHEKA ALIKUBALI KUPAMBANA NA BONDIA JAPHET
KASEBA WAKATI HUO MLUNDWA/PST AKIJUA WAZI KWAMBA JAPHET KASEBA ALIKUWA
NJE YA ULINGO WA NGUMI ZA BILA MATEKE KWA KIPINDI CHA MIAKA 12, NA AKIWA
NA PAMBANO MOJA TU LA NGUMI BILA MATEKE ALILOPIGANA NA ERNEST BUJIKU
PALE -PTA HALL, NA HALI YA KUWA YEYE FRANCIS CHEKA ALIKUWA TAYARI
AMEPIGANA MAPAMBANO ISHIRINI NA TATU [23]
NDIYO MAANA HAPO KTK SOMO ,NIMESEMA MABONDIA WA KULIPWA WANAVYOPOTOSHWA NA VIONGOZI ,
PAMBANO LA CHEKA MWENYE REKODI YA 23 NA JAPHET KASEBA MWENYE REKODI YA
PAMBANO MOJA LA TAREHE 02-10-2009 LILIIDHINISHWA NA EMANUEL MLUNDWA /PST
NA PAMBANO AMBALO ALITAKIWA FRANCIS CHEKA ACHEZE NA KASEBA LILIKUWA
CHINI YA USIMAMIZI WA TPBC , TENA WAKATI HUU KASEBA AKIWA NI BINGWA WA
PST ,CHEKA AKAPOTOSHWA KWAMBA POINT ALIZONAZO NI NYINGI HIVYO HARUHUSIWI
KUCHEZA NA JAPHET KASEBA .NAYE KWA KUWA HAJUWI ALIKUBALIANA NA USHAURI
WA KIJINGA , ULIOMHARIBIA HESHIMA YAKE MBELE YA JAMII.
SASA TUJIULIZE HATA NAFASI YA JAPHET KASEBA KUPIGANIA UBINGWA WA PST
DHIDI YA MKONGWE MANENO OSAWLD MWENYE MAPAMBANO ZAIDI YA 60 ALIIPATAJE
HALI YA KUWA JAPHET KASEBA AKIWA NA MAPAMBANO MAWILI TU ? LA CHEKA NA
BUJIKU ?NA KISHA ETI KWA CHEKA AWE HANA SIFA ZINAZOSTAHILI? KWA PAMBANO
LINALOSIMAMIWA NA TPBC?
SISI ORGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA [TPBO] TUNAAMINI KABISA
KWANBA KUNA BAADHI YA VIONGOZI WA NGUMI ZA KULIPWA NI WAPOTOSHAJI WA
TARATIBU ZINAZOTAWALA NGUMI ZA KULIPWA NA TUTAENDELEA KUWAELIMISHA
WAANDISHI WETU MARA ZOTE ILI KUONDOWA DHANA NZIMA YA KUWA KUNA MIGOGORO
KTK NGUMI ZA KULIPWA. KUMBE NI UJINGA WA BAADHI YETU SISI VIONGOZI.
,NAPO BAADHI YA VIONGOZI WANAOJIFANYA WANAJUWA SAAANA NA KUWAPOTOSHA MABONDIA KWA MASLAHI YAO BINAFI.
KATIKA PAMBANO LILOANDALIWA NA KITWE GENERAL TRADERS KUGOMBEA UBINGWA WA
IBF-AFRIKA BAINA YA MTANZANIA RAMADHANI SHAURI NA MGANDA SANDE KIZITO
LILIPANGWA PAMBANO LA UTANGULIZI KATI YA BONDIA FRANCIS MIYEYUSHO ACHEZE NA BONDIA BORA WA TASWA NASIBU RAMADHANI ,
KUNA KIONGOZI MMOJA [SIYO NGOWI] ALIMKATAZA BONDIA FRANCIS MIYEYUSHO
ASIPIGANE PAMBANO LA UTANGULIZI ETI MIYEYUSHO ALISHAWAHI KUMPIGA
RAMADHANI SHAURI PALE TEXAS, KWA HIYO SHERIA INAMKATAZA KUCHEZA
UTANGULIZI KWA PAMBANO KUU ANALOCHEZA BONDIA ALIYEWAHI KUMSHINDA / NA
KWELI FRANCIS ALIKATAA HUKU AKIWA AMESHACHUKUWA MALIPO YA AWALI KUTOKA
KWA PROMOTA. NA KIONGOZI HUYO ALIJUWA KWAMBA BONDIA AMESHALIPWA
ADVANCE.---HUU NI UPOTOSHAJI MKUBWA SANA NA UNAFAA ULAANIWE.
KWA KIFUPI NDG WAANDISHI WA HABARI HAKUNA KIPENGELE KINACHOMPA RUHUSA
BONDIA KUKATAA KUCHEZA NA BONDIA MWINGINE ETI KWA KUWA ANA POINT CHACHE ,
ILA NI CHAMA NDIYO CHENYE MAMLAKA YA KUAMUWA KWA MAPAMBANO YA UBINGWA
TU. NDIPO HUTAFUTWA MABONDIA WENYE VIWANGO VINYOKARIBIANA ILI KULETA
USHINDANI MKUBWA KWENYE MAPAMBANO YA UBINGA ,NA SI KTK PAMBANO AMBALO
SIYO LA UBINGWA.
NA KIUTARATIBU BONDIA ANAPOKUWA BINGWA ANAYETAMBULIWA NA CHAMA CHOCHOTE
CHA NCHI AU CHA KIDUNIA ,NA ANATAKA KUCHEZA PAMBANO LISILO LA UBINGWA AU
LA UBINGWA WA CHAMA KINGINE NI LAZIMA AOMBE KIBALI KUTOKA KWENYE CHAMA
ANACHOSHIKILIA UBINGWA HUO . HASA KAMA CHAMA HICHO ANACHOSHIKILIA
UBINGWA WAKE HAKISIMAMII PAMBANO HILO.
NATOWA WITO KWA VIONGOZI WENZANGU KWAMBA HUU SIYO WAKATI WA KUWADANGANYA
WAANDISHI , KWA KUWAPA HABARI POTOFU , KWANI KUWA KIONGOZI WA CHAMA
HAKUKUPI WEWE NAFASI YA KUPOTOSHA WAANDISHI ,NA KAMA KUNA BAADHI YA
MAMBO HATUYAJUWI TUWE NA UTARATIBU WA KUULIZANA ,KWANI MAMBO HUBADILIKA
KILA MARA.
IMEANDIKWA NAMI[-
YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
RAIS -TPBO & WPBF-USBC [WORLD PROFESSIONSL BOXING FEDERATION -REPRESENTATIVE -TO TANZANIA
+255-713-644974 -752-335584
No comments:
Post a Comment