Kamisheni ya Ngumi
za Kulipwa Nchini (TPBC) imelipiga jeki Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Nchini
(BFT) katika mashindano yaliyomalizika jana katika uwanja wa ndani wa Taifa.
Rais wa TPBC, Onesmo Ngowi (pichani) alimkabidhi Katibu Mkuu wa BFT bwana Makore Mashaga zawadi za
washindi wa kwanza na wa pili katika mashindano ya ngumi za ridhaa za taifa
yaliyoshirikisha mabondia kutoka katika mikoa zaidi ya 19 ya Tanzania
bara.
Ngowi
alimweleza Katibu Mkuu wa BFT kuwa TPBC inaungana na BFT katika kuendeleza ngumi
nchini wakijua wazi kuwa ni katika mashindano kama haya Tanzania inawapata
wawakilishi wake katika mashindano ya kimataifa.
Ushirikiano huu wa
TPBC ulianza tangu wakati wa Katibu Mkuu wa zamani wa iliyokuwa TABA marehemu
Narcis Tarimo.
Akimwelezea zaidi
msaada wa TPBC katika mashindano ya taifa, Rais wa TPBC bwana Onesmo Ngowi
alisema kuwa ni ngumi za ridhaa pekee ambazo zinaweza kuleta mwelekeo wa
maendeleo ya ngumi nchini.
Ngowi alisema kuwa
kama hakuna msingi mzuri wa ngumi za ridhaa ni wazi kuwa hakutakuwa na ngumi
nzuri za kulipwa kwani msingi wa ngumi unaanzia kwenye ngumi za
ridhaa.
Rais huyo
aliyekuwa bondia maarufu wakati wa ngumi za ridhaa na kulipwa miaka ya 80 na 90
kiasi cha lupewa jina la “Piston Mover”(mwendo wa piston ya gari) kwa ajili ya
kasi ya mikono na miguu yake alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kufundisha
ufundi kwa mabondia ili waweze kucheza ngumi za ufundi.
“Kuna tofauti
kubwa sana kati ya ngumi za ridhaa na ngumi za kulipwa” aliendelea kusisitiza
Rais huyo.
“Wakati mabondia
wa ridhaa wanapewa points wakati wanapopiga ngumi za ufundi za kichwani, bondia
wa ngumi za kulipwa anatakiwa aweze kumzidi mpinzania wake kwa kila kitu”
aliendelea kusisitiza Rais huyo.
Mabondia wetu wa
ridhaa wanatakiwa wafundishwe namna ya kupiga ngumi za ufundi kichwani na ziwe
nyingi ndipo wanaweza kushinda kwenye mashindano ya kimataifa” alimalizia
kusisitiza Ngowi.
Ushirikiano wa
TPBC na BFT unaleta sura mpya kwenye tasnia ya ngumi nchini na inaonyesha mwanga
mzuri mbele ta safari.
Imetolewa na
Uongozi
Kamisheni ya Ngumi
za Kulipwa Nchini (TPBC)
No comments:
Post a Comment