mashali ambye mwezi wa sita alifanikiwa kumtwanga bondia kutoka kyela maisha samson na kufanikiwa kutetea ubingwa wake kwa kumtwanga bondia huyo kutoka kyela kwa knock-out ya raundi ya sita.
pambano hili linaandaliwa kwa pamoja kati ya tpbo na media intertainment and arts promotion ni mahsusi kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa.
tpbo imeonelea imuenzi baba wa taifa kwa pambano la ngumi kama njia pekee ya kumuenzi ,kwa jinsi wakati wa utawala wake alivyoisaidia michezo yote bila kubaguwa ,na hatimaye tanzania kuwapata mabondia bora na wazuri kama akina rashid matumla ,kinyume na sasa mchezo wa ngumi haupati aina yoyote ya udhamini kiasi kuwakatisha tamaa hata mabondia wenyewe na mapromota.
tuna imani kubwa sana kwamba kwa kumkumbuka baba wa taifa tutapata mafanikio makubwa sana na matumani mapya.
imeletwa kwenu
nami yassin abdallah -ustaadh
rais -tpbo
No comments:
Post a Comment