PRETORIA, Afrika Kusini
BINGWA wa zamani wa dunia wa uzani wa ‘heavyweight’ Corrie
Sanders amefariki dunia baada ya kupigwa risasi katika tukio la ujambazi
lililohusisha matumizi ya risasi za moto jijini hapa.
Mkali huyo mwenye miaka 46, aliripotiwa kuhudhuria sherehe
ya kifamilia kwenye mgahawa mmoja jirani na hapa Pretoria katika nchi yake ya
asili ya Afrika Kusini, ambapo shambulio hilo lilichukua uhai wake akiwa
hospitalini kwa matibabu.
Sanders anakumbukwa zama zake ulingoni, alikotisha kiasi cha
kutwaa mataji makubwa ya dunia, likiwamo la WBO ‘heavyweight’ alilotwaa kwa
kumchapa Wladimir Klitschko mwaka 2003.
Miaka mitano baada ya ubingwa huo, Sanders akatundika glovu
zake mwaka 2008, akiwa na rekodi ya kushinda mapambano yake 42 kati ya 46
aliyopanda ulingoni kupigana.
Sanders akiwa na mkanda wake huo wa WBO Desemba mwaka huo
huo wa 2003 apanda ulingoni dhidi ya ndugu yake na Wladimir, Vitali kuwania
ubingwa wa WBC aliokuwa akiushikilia
Vitali raia wa Ukraine.
Lakini katika pambano hilo, Sanders alishindwa kurejea kile
alichomfanyia Wladimir, baada ya kukubali kichapo cha raundi ya nane ya kwenye
Ukumbi wa Staples Center jijini Los Angeles.
Sanders akastaafu masumbwi Desemba 2004 baada ya kumchapa
Alexei Varakin katika raubndi ya pili ya pambano lao nchini Austria, lakini
akarejea tena ulingoni miaka miwili baadaye.
Februari 2008, Sanders akapoteza pambano lake la mwisho
alilotangaza kustaafia, dhidi ya Osbourne Machimana, kuwania ubingwa wa Afrika
Kusini ‘heavyweight’ na kumfanya astaafu kwa kichapo.
You might also like:
No comments:
Post a Comment