Tangazo

Pages

Wednesday, September 19, 2012

ELIMU YA MCHEZO WA MASUMBWI


WAANDISHI NA WADAU WAKUU WA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA.

KAMA NILIVYOWAHI KUWAAHIDI KWAMBA KILA  KILA NITAKAPOKUWA NIMEPATA NAFASI NZURI NITAKUWA NIKIWAPATIA ELIMU YA BURE KTK MASUALA MAZIMA YAHUSUYO NGUMI ZA KULIPWA ILI KUONDOWA MIKANGANYIKO AMBAYO HUJITOKEZA KWA BAADHI YA WATU WASIOJUWA VYEMA TARATIBU NZIMA NA MTIRIRIKO WA MAMLAKA ZA KUSIMAMIA NGUMI ZA KULIPWA KOTE DUNIANI.

NINAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWAMBA NIMEPATA NAFASI HIYO.

NA KATIKA MAELEZO HAYA NITAJIKITA ZAIDI NA UTARATIBU MZIMA WA UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA DUNIANI KOTE;-

UTARATIBU NA MTIRIRIKO WA MAMLAKA ZA KUSIMAMIA NA KUENDESHA NGUMI ZA KULIPWA KATIKA NCHI NYINGI DUNIANI YANAKUWA CHINI YA MAKAMPUNI AU VYAMA VYA HIYARI.

MFANO HALISI NI BARAZA LA NGUMI ZA KULIPWA LA JUMUIYA YA MADOLA AMBALO LILISAJILIWA MWAKA 1967 KAMA KAMPUNI [COMMON WEARTH BOXING COUNCIL -LIMITED] [GOOGLE THEN- COMMON WEARTH BOXING COUNCIL LTD] UTAIONA KAMPUNI HII YA NGUMI YA JUMUIYA YA MADOLA NA UNDANI WAKE

NA PIA WANACHAMA WA BARAZA HILO AMBALO NI KAMPUNI, NI VYAMA VYA VYA NGUMI ZA KULIPWA KUTOKA NCHI AMBAZO NI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA.KWA HAPA TANZANIA TPBC  ILYOSAJILIWA WIZARA YA MAMBO YA NDANI NI MWANACHAMA WAKE .


NA NDIYO MAANA HAPA TANZANIA TUNAZO TAASISI ZAIDI YA 5 ZA NGUMI ZA KULIPWA
AMBAZO NYINGI KATI YA HIZO ZIMESAJILIWA KWA MSAJILI WA MAKAMPUNI ,ISIPOOKUWA TPBC PEKEE AMBAYO IMESAJILIWA KAMA -NONE GOVERNMENT ORGANIZATION [NGO] WIZARA YA MAMBO YA NDANI.

KATIKA NCHI YETU YA TANZANIA NGUMI ZA KULIPWA HAZIKO CHINI YA WIZARA YA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO,KWA SHERIA NAMBA 12 YA MWAKA 1967 ILIYOFANYIWA MAREKEBISHO 1971 ,SHERIA IKO WAZI KABISA KWAMBA NGUMI ZA KULIPWA HAZISIMAMIWI NA WIZARA ,NA HATA KATIKA ORODHA YA VYAMA VYA MICHEZO VINAVYOTAMBULIWA NA BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA [BMT], NGUMI ZA KULIPWA HAZIMO KTK ORODHA  YA VYAMA HIVYO.BALI  NGUMI ZA RIDHAA TU KUPITIA -BOXING FEDERATION OF TANZANIA [BFT] NDIZO ZINATAMBULIWA.NA ZIKO CHINI YA WIZARA.


NA HUU NI UTARATIBU WA KAWAIDA KWA NCHI KARIBU ZOTE DUNIANI ISIPOKUWA TU KAMA SERIKALI YA NCHI HUSIKA ITAAMUWA KUANZISHA MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUTOA MIONGOZO PALE PANAPOKUWA NA MATATIZO KUHUSU NGUMI ZA KULIPWA [BOXING BOARD OF CONTROL ]

NCHINI UINGEREZA KUNA VYAMA VYA NGUMI ZA KULIPWA ZAIDI YA KIMOJA  LAKINI VYOTE VINAWAJIBIKA KWA -BRITISH BOXING BARD OF CONTROL [BBBC]

NA VYAMA HIVYO VINAVYOENDESHA NGUMI ZA KULIPWA AIDHA NI MASHIRIKA YA HIYARI AU MAKAMPUNI  [LIMITED ]


NIMEAMUWA KUTOWA ELIMU HII KUTOKANA NA UELEWA MDOGO SANA KWA BAADHI YA WATANZANIA NA HATA WANAOJIITA NI WADAU WAKUBWA WA NGUMI ZA KULIPWA , NA WAPO HATA BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO, WANAOAMINI KABISA KWAMBA NGUMI ZA KULIPWA  HUSAJILIWA NA BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA[BMT] NA ZINASIMAMIWA NA WIZARA HUSIKA NA MICHEZO.


 NA HATA KWA VIPINDI TOFAUTI  WABUNGE PIA WAMEKUWA WAKIHOJI BUNGENI JUU YA KUWA NA TAASISI ZAIDI YA MOJA KATIKA NGUMI ZA KULIPWA.



NAPENDA SANA NA NINAFURAHIA SANA MAONI YANAYOTOLEWA NA WABUNGE WAWAPO KTK VIKAO VYA BUNGE KUHUSU MICHEZO KWA UJUMLA WAKE .


LAKINI NI VYEMA WAHESHIMIWA WABUNGE NAO WAKAJULISHWA  KWAMBA KUWA NA TAASISI ZAIDI YA MOJA INAYOONGOZA NA KUSIMAMIA NGUMI ZA KULIPWA SI KOSA LA JINAI, NA SI TANZANIA PEKEE YENYE MFUMO HUU ,WA KUWA NA MASHIRIKISHO ZAIDI YA MOJA,NA HATA KUWA NA MARAIS ZAIDI YA 600 KTK NGUMI ZA KULIPWA KOTE DUNIANI ,LAKINI INGESHANGAZA SANA KAMA TAASISI MOJA TU YA NGUMI ZA KULIPWA HAPA IKAWA NA MARAIS 10.


NA TPBO TUPO TAYARI KUTOWA USHIRIKIANO  KWA WAHESHIMIWA WABUNGE IWAPO WATAHITAJI KUJUWA LOLOTE KUHUSU NGUMI ZA KULIPWA KWA MANUFAA YA WATANZANIA WANAOWAWAKILISHA.BUNGENI

JAMBO KUBWA LINALOHITAJIKA HAPA TANZANIA NA AMBALO NI LA MUHIMU,  NI UWAJIBIKAJI NA UMAKINI KATIKA KAZI ZA KUHAKIKISHA  MABONDIA WANACHEZA NA KUPATA HAKI ZAO BILA UBABAISHAJI ,PIA KUJENGA DHANA NZIMA YA KUHESHIMIANA MIONGONI MWA VIONGOZI WA TASISI  HIZO ZINAZOSIMAMIA NGUMI ZA KULIPWA.HAPA TANZANIA.

KATIKA HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE ,WAKATI AKIHUTUBIA MIKUTANO YAKE YA KAMPENI MWAKA 2005 ALISISITIZA KWAMBA ANATAKA KUBUNI AJIRA ZA SEKTA BINAFSI MILIONI MOJA NA LAKI TANO [1,500,000] ILI VIJANA WA TANZANIA WAWEZE KUJIAJIRI.


TUNAJIPONGEZA KUWA KATIKA NGUMI ZA KULIPWA TUMEFANIKIWA KUWATENGENEZEA AJIRA VIJANA WENGI AMBAO WANAPATA MALIPO KUTOKANA NA MCHEZO WA NGUMI KTK KILA PEEMBE YA TANZANIA ,JAPO KUWA TUNAKABILIWA NA CHANGAMOTO KUBWA SANA YA KUKATALIWA NA WADHAMINI ,MPAKA SASA TUNAJIULIZA NI KWA NINI HAWATAKI KUUDHAMINI MCHEZO WA NGUMI KWA UJUMLA WAKE NA KWA NINI WANAUWEKEA UBAGUZI ?


SASA TPBO TUNADHANI IKO HAJA HATUA ZA MAKUSUDI ZICHUKULIWE NA VIONGOZI WALIOKO MAARAKANI NA HATA  WALE WA VYAMA VYA SIASA VYA UPINZANI AMBAO WANATAKA KUINGIA MADARAKANI ,KUONA KWAMBA UMEFIKIA WAKATI WA KUWASAIDIA  VIJANA WACHEZAO NGUMI ILI NAO WAJIHISI KWAMBA NI WAPIGA KURA WAO HALALI AMBAO WAMEWAWEZESHA AU WATAWAWEZESHA KUINGIA MADARAKANI KUIONGOZA NCHI YAO -TANZANIA.

PIA KWA KUWA NA TAASISI ZAIDI YA MOJA YA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TANZANIA TUMEFAIDIKA NA KUTAMBULISHA TANZANIA KATIKA DUNIA NA RAMANI YA NGUMI ZA KULIPWA ,KWANI VIONGOZI WAKUU WOTE WA TAASISI HIZO WAPEPATA NAFASI YA KUWA WAWAKILISHI WA MASHIRIKISHO YA NGUMI ZA KULIPWA YA KIMATAIFA.

 [1]MIFANO HAI-; MKURUGENZI WA PST NDG EMANUEL MLUNDWA YEYE NI MWAKILISHI WA -   UNVERSAL BOXING ORGANISATION [UBO ] BARANI AFRKA ,NA MABONDIA WA     KITANZANIA WANAPAMBANA  MARA KWA MARA ILI KUIGOMBEA MIKANDA INAYOTAMBULIWA NA UBO ,KWA MALIPO MAZURI KABISA .


[2]ONESMO NGOWI ;-RAIS WA TPBC YEYE NI MWAKILISHI WA SHIRIKISHO LA NGUMI LA KIMATAIFA --INTERNATIONAL BOXING FEDERATION[[IBF ] BARA LA AFRIKA.NA MABONDIA WA TANZANIA WAMESHAPIGANIA UBINGWA UNAOTAMBULIWA NA IBF -AFRICA NA WAMEJIPATIA KIPATO KIZURI , NA HIVI KARIBUNI BONDIA CHIPUKIZI RAMADHANI SHAURI WA TANZANIA ALIFANIKIWA KUMTWANGA MGANDA SANDE KIZITO KWA KNOCK OUT YA RAUNDI YA 8 NA KUUTWAA UBNGWA KTK UZITO WA FEATHER.



[3]YASSIN ABDALLAH USTAADH - RAIS WA TPBO YEYE ANAWAKILISHA SHIRIKISHO LA NGUMI ZA KULIPWA LA DUNIA[world professional boxing federation-WPBF-USBC] LENYE MAKAO MAKUU NCHINI MAREKANI,  ,NA HIVI KARIBUNI MTAONA MIKANDA YA UBINGWA YA SHIRIKISHO HILI IKIPIGANIWA NCHINI TANZANIA,BAINA YA MABONDIA WA TANZANIA NA WA NJE YA TANZANIA ,TARATIBU ZOTE ZA AWALI ZIMEKAMILISHWA.


 PIA IPO MIFANO YA NCHI ZA JIRANI KUWA NA ZAIDI YA TAASISI MOJA YA NGUMI ZA KULIPWA--

 KENYA IPO KAMISHENI YA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI KENYA [KPBC]  ,IPO  FPBK, NA KBB NA ZOTE ZINAFANYA KAZI KWA KUHESHIMIANA KWA LENGO LA KUWASAIDIA MABONDIA WA NCHI A KENYA


,NA HIVI KARIBUNI NCHINI UGANDA IMESAJILIWA TAASISI MPYA IJULIKANA KAMA [UPBU ] UGANDA PROFESSIONAL BOXING UNION PAMOJA, NA ILE KONGWE -UGANDA PROFESSIONL BOXING COMMISION INAYOONGOZWA NA NDG SELESTINO MINDRA KAMA RAIS WAKE.KWA MALENGO YA KUWASAIDIA MABONDIA WA UGANDA.



TANZANIA PROFESSIONAL BOXING ORGANISATION [TPBO] INAWAOMBA WANANCHI WOTE NA HASA WAPENDA MICHEZO WA TANZANIA KUITIKIA WITO WA SERIKALI YA JAMHURI YA TANZANIA  YA KUATAKA WAJITOKEZE KWA WINGI ILI WAWEZE KUTOWA MAONI JUU YA MAREKEBISHO YA KATIBA ,NA WAITAKE KATIBA MPYA IBADILISHE SERA ZA MICHEZO NA ITAMBUWE RASMI  MICHEZO YA KULIPWA ILI VIJANA WENGI WAPATE AJIRA KUPITIA MICHEZO MBALI MBALI UKIWEMO NGUMI ZA KULIPWA.


KWA KIFUPI KABISA SOMO LETU LA LEO , NADAHANI LIMEELEWEKA NA NATARAJIA HAKUTAKUWA NA MSHANGAO TENA WA KWA NINI NGUMI ZA KULIPWA  ZINASIMAMIWA NA MAKAMPUNI AU VYAMA VYA HIYARI


TPBO DAIMA ITAENDELEA KUTOWA USHIRIKIANO MKUBWA KWA VYOMBO VYA HABARI WAKATI WOWOTE NA MAHALI POPOTE TUKIHITAJIWA KUFANYA HIVYO , KWANI TUNAAMINI KWAMBA VYOMBO VYA HABARI NI NYENZO MUHIMU SANA KWENYE TASNIA YETU YA NGUMI ZA KULIPWA ,MUSIOGOPE KUTUITA POPOTE PALE

        NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU ZA AWLI KWENU NYOTE


                        IMELETWA KWENU NAMI


                     YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
        RAIS - TANZANIA PROFESSIOHAL BOXING ORGANISATION -TPBO
        WPBF-USBC-world professional boxing organisation -representative to-TANZANIA

               +255-713-644974  - 752-335584

No comments:

Post a Comment