Tangazo

Pages

Wednesday, September 12, 2012

BFT YAUNDA KAMATI YA KUFANIKISHA MASHINDANO YA NGUMI

SHIRIKISHO LA NGUMI TANZANIA (BFT)
                                                                                                      S.L.P 15558
                                                                                                                     DAR ES SALAAM.
                                                                                                              September 11, 2012,
                                                                                Email:-bft.tanzania 2009@gmail.com.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
     Yah:- BFT YAUNDA KAMATI YA KUFANIKISHA MASHINDANO YA NGUMI YA
                TAIFA 2012.TAREHE 17-22/09/2012.UWANJA WA NDANI WA TAIFA.
Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) limeunda kamati ya mashindano kwa lengo la kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kiwango cha taifa. Kamati hiyo imeundwa kwa kuwajumuisha wataalamu wa ufundi kutoka  kamati za BFT,mabondia wa zamani na wataalam wa mipango na fedha kutoka katika taasisi na mashirika ambayo yamekuwa mtari wa mbele kusaidia kwa vitendo shughuri na matukio mbalimbali ya BFT na kupelekea kusaidia kufuzu kwa bondia Selemani Kidunda  kushiriki katika michezo ya Olimpiki iliyomalizika hivi karibuni London, Uingereza.
Wajumbe walioteuliwa kuunda kamati hiyo ya mashindano ni Andrew kweyeyana ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati,Willy Issangura,Juma Suleiman,Remy Ngabo na Mohamed kasilamatwi.
Wengine ni Said Omari,Antony Mwang’onda,Joel Magori,Charles Jilaba na Undule Mwampulo.
Jukumu walilopewa ni kuhakikisha mashindano yanafanyika kwa kufata taratibu zote za chama cha ngumi cha dnia AIBA na kuhakikisha fedha za kuendesha mashindano zina patikana.
Majukumu ya kamati hiyo yatamalizika baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.
Nawatakia kazi njema kwa nia ya kutangaza mashindano haya .
Habari hizi zinaletwa kwenu na
Makore Mashaga
Katibu Mkuu (BFT)         Mob:-0713/0784/0763/0773- 588818
                                          Email:- mashagam@yahoo.com.

No comments:

Post a Comment