Tangazo

Pages

Saturday, December 31, 2016

CHEKA AFUNGIWA MIAKA MIWILI NA TPBC KWA KUMKIMBIA DULLA MBABE

Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam,  kuhusu bondia Francis Cheka ambaye amefungiwa miaka miwili pamoja na kulipa faini ya Shilingi 500,000. Kulia ni Mwenyekiti Kamati ya Ufundi TPBC, Ally Bakari na katikati Katibu Msaidizi wa TPBC, Mchatta Michael

KAMISHENI ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), imemfungia bondia Francis Cheka kujihusisha na ngumi kwa miaka miwili pamoja na faini ya Sh 500,000 ikiwa ni siku moja tangu bondia huyo  atangaze kustaafu.

Juzi Cheka alitangaza kustaafu kucheza ngumi akidai kwa muda mrefu amekuwa akipigana bila mafanikio kutokana na kudhulumiwa na waandaaji wa mapambano au kulipwa tofauti na makubaliano pamoja na misukosuko anayofanyiwa na wapinzani wake.

Cheka ilikuwa apande ulingoni Desemba 25 mwaka huu kupigana na Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ lakini hakufanya hivyo akidai kumaliziwa kwanza fedha zake.

Pambano hilo liliandaliwa na bondia Siraji Kaike. Mwanzoni mwa wiki hii bondia huyo alikamatwa na Polisi Morogoro kwa kosa hilo la kuchukua nusu ya fedha na kutopanda ulingoni ambapo alishikiliwa kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa.

Akizungumza na wandishi wa habari jana, Rais wa TPBC Chaurembo Palasa, alisema Cheka amefungiwa kutokana na  kutofika ulingoni kwenye pambano hilo la siku ya Krismasi.

“Cheka aliingia makubaliano na promota Siraji Kaike ya kupigana na Dulla Mbabe, lakini hakufika kwenye pambano jambo ambalo halileti picha nzuri kwenye ngumi za kulipwa hivyo tumemfungia pamoja na faini juu,” alisema Palasa.

Katika mkutano wake huo na waandishi wa habari, Palasa aliongozana na Mwenyekiti Kamati ya Ufundi wa TPBC, Ally Bakari na Katibu Msaidizi wa kamisheni hiyo Mchatta Michael ambao walilaani kitendo cha Cheka kutopanda ulingoni kwani kilisababisha promota Kaike kupata hasara na pia kinarudisha nyuma ngumi kwani wanaonekana wababaishaji.

Kwa mujibu wa Cheka, alipaswa kulipwa Sh milioni tisa, lakini hadi wakati wa kupima uzito alikuwa amepewa Sh milioni tatu pekee ndio maana hakupima uzito kwani kisheria ukipima uzito umekubali kucheza.

Baada ya kutangaza kustaafu Cheka amesema anajielekeza kufanya biashara zake na ameahidi ushirikiano kwenye mchezo wa ngumi ili kukuza na kuendeleza mchezo.

Akizungumzia kufungiwa kwake Cheka alisema hatambui maana yeye si mwanachama wa TPBC.

“Bondia wa kulipwa hana chama wala mwanachama, kuna mkataba walifoji (kughushi) saini yangu waliuona? au wanahukumu upande mmoja, kwa nini wasinitafute wakanisikiliza na mimi? Mimi nadhani sasa viongozi waende wakosomee uongozi, serikali itusaidie hili,” alisema.

BONDIA VICENT MBILINYI

BONDIA VICENT MBILINYI KG 63

 BONDIA VICENT MBILINYI KG 63

BONDIA VICENT MBILINYI KG 63

BONDIA VICENT MBILINYI KG 63

MABONDIA VICENT MBILINYI NA MRISHO ADAM KUONESHANA UMWAMA LEO MANZESE

Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akitunishiana misuli na Mrisho Adam baada ya kupima uzito jana kwa ajili ya mpambano wao leo katika ukumbi wa manyara park manzese Picha na SUPER D BOXING NEWS
bondia Mrisho Adam akipima uzito kushoto ni Vicent Mbilinyi
Bondia Vicent Mbilinyi akipima Uzito

Tuesday, December 20, 2016

BONDIA OMARI KIMWERI AWAMWAGIA VIFAA MABONDIA WATANZANIA

Mwakilishi wa Kimweri Promotion Nchini Tanzania Yuyuph Mnyeto kushoto akimkabidhi vifaa vya ndondi kwa kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kupokelewa na kukabidhiwa kwa wadau mbalimbali nchini vifaa hivyo vimetolewa na Bondia Mtanzania anaefanya shughuli zake Victoria, Australia, Omari Kimweri picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Selemani Kidunda kushoto kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' na Mwakilishi wa Kimweri Promotion Nchini Tanzania Yuyuph Mnyeto kushoto wakiwa katika picha wa pamoja baada ya kukabidhi vifaa vilivyotoka kwa bondia Omari Kimweri anaefanya shughuli zake Australia
 picha na SUPER D BOXING NEWS

Mwakilishi wa Kimweri Promotion Nchini Tanzania Yuyuph Mnyeto kushoto akimkabidhi vifaa vya ndondi kwa kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kupokelewa na kukabidhiwa kwa wadau mbalimbali nchini vifaa hivyo vimetolewa na Bondia Mtanzania anaefanya shughuli zake Victoria, Australia, Omari Kimweri picha na SUPER D BOXING NEWS

Monday, December 19, 2016

MABONDIA VICENT MBILINYI NA IDD MKWELA WAENDELEA KUJIFUA CHINI YA USIMAMIZI WA SUPER D COACH

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimnowa bondia Vicent Mbilinyi kwa ajili ya mpambano wake na Mrisho Adamu utakaofanyika katika ukumbi wa Manyara Park desemba 31 mpambano wa raundi kumi Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Iddi Mkwela wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM Kariakoo Mbilinyi anajiandaa na mpambano wake na Mrisho Adamu utakaofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Iddi Mkwela kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Vicent Mbilinyi Mbilinyi anajiandaa na mpambano wake Desemba 31 kupambana na Mrisho Adamu Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Iddi Mkwela kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Vicent Mbilinyi Mbilinyi anajiandaa na mpambano wake Desemba 31 kupambana na Mrisho Adamu Picha na SUPER D BOXING NEWS
KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KATIKATI AKIWA NA MABONDIA IDDI MKWELA KUSHOTO NA VICENT MBILINYI BAADA YA MAZOEZI KATIKA KAMBI YA SUPER D COACH UHURU GYM
KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KATIKATI AKIWA NA MABONDIA IDDI MKWELA KUSHOTO NA VICENT MBILINYI BAADA YA MAZOEZI KATIKA KAMBI YA SUPER D COACH UHURU GYM
SUPER D COACH KULIA AKIWA NA MABONDIA VICENT MBILINYI KULIA NA IDDI MKWELA KATIKATI

Friday, November 25, 2016

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' APAA Huxleys,Berlin

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere kwa ajili ya safari yake ya kwenda Huxleys, Kreuzberg, Berlin kupambana novemba 29 mpambano wa marudio na bondia Zapir Rasulov baada ya  lile la kwanza kushinda kwa point kule nchini Panama City,  Panama na kurudi na ubingwa kulia ni msaidizi wa bondia huyo Joe Anena  Picha na SUPER D BOXING NEWS
Msaidizi wa  Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' JoeAnena kushoto wakiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere kwa ajili ya safari yao ya kwenda Huxleys, Kreuzberg, Berlin kupambana novemba 29 mpambano wa marudio na bondia Zapir Rasulov baada ya  lile la kwanza kushinda kwa point kule nchini Panama City,  Panama na kurudi na ubingwa  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akiwa na bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati alipo msindikiza bondia huyu uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere kwa ajiri ya safari yake ya kwenda Huxleys, Kreuzberg, Berlin kupambana novemba 29 mpambano wa marudio na bondia Zapir Rasulov baada ya  lile la kwanza kushinda kwa point kule nchini Panama City,  Panama na kurudi na ubingwa  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Msaidizi wa  Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' Joe Anena kushoto akizungumza na bondia huyo kabla awajapanda pipa kwenda Berlin
Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na bondia Ibrahimu Class kushoto na Joe Anena katika uwanja wa ndege wa kimataifa kwa ajili ya safari ya Berlin ya bondia huyo anaenda kuzipiga mpambano wa marudiano na na bondia Zapir Rasulov baada ya  lile la kwanza kushinda kwa point kule nchini Panama City,  Panama na kurudi na ubingwa  Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na bondia Ibrahimu Class kushoto na Joe Anena katika uwanja wa ndege wa kimataifa kwa ajili ya safari ya Berlin ya bondia huyo anaenda kuzipiga mpambano wa marudiano na na bondia Zapir Rasulov baada ya  lile la kwanza kushinda kwa point kule nchini Panama City,  Panama na kurudi na ubingwa  Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akiwa na bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati alipo msindikiza bondia huyu uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere kwa ajiri ya safari yake ya kwenda Huxleys, Kreuzberg, Berlin kupambana novemba 29 mpambano wa marudio na bondia Zapir Rasulov baada ya  lile la kwanza kushinda kwa point kule nchini Panama City,  Panama na kurudi na ubingwa  Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na bondia Ibrahimu Class kushoto na Joe Anena katika uwanja wa ndege wa kimataifa kwa ajili ya safari ya Berlin ya bondia huyo anaenda kuzipiga mpambano wa marudiano na na bondia Zapir Rasulov baada ya  lile la kwanza kushinda kwa point kule nchini Panama City,  Panama na kurudi na ubingwa  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Saturday, October 22, 2016

IDDI MKWELA NA ISSA NAMPEPECHE WAPIMA UZITO KUZIPIGA KESHO OCTOBER 23 CCM MWIJIMA MWANANYAMALA

Kocha wa wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D ' katikati akiwa na mabondia Iddi Mkwela kushoto na Issa Nampepeche baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa  raundi kumi utakaofanyika siku ya jumapili ya October 23 katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Iddi Mkwela kushoto akitunishiana misuli na Issa Nampepeche baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya Ocober 23 katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini katikati Rajabu Mhamila 'Super D ' akimtia gumi la kolomelo kocha wa ISSA Nampepeche  Ibrahimu Kamwe wakati wa upimaji uzito baada ya kokosana kauli kila mmoja akidai bondia wake zaidi Super D anamnowa Iddi Mkwela na Kamwe anamfundisha Nampepeche 

Kocha wa wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D ' katikati akiwa na mabondia Iddi Mkwela kushoto na Issa Nampepeche baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa  raundi kumi utakaofanyika siku ya jumapili ya October 23 katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Iddi Mkwela akihojiwa na wana habari nyuma ni kocha wake Rajabu Mhamila 'Super D' 
Bondia Mohamed Kisua akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake kesho jumapili

mohamedi kisua
bondia Pius Kazaula akipima uzito
PIus Kazaula
Pius Kazaula
Bondia Iddi Mkwela akipima uzito kushoto ni mpinzani wake Issa Nampepeche
Bondia Rojas Masamu akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Haidal Raju
Rojas Masamu