Tangazo

Pages

Wednesday, June 24, 2015

ALLY BAKARI CHAMPION ACHUKUWA JIKO


Refarii wa mchezo wa masumbwi nchni kushoto akiwa na mke wake Aisha Chilumba  baada ya kuowa hivi karibuni maendeo ya Vingunguti Dar es salaam


Refarii wa mchezo wa masumbwi nchni kushoto akiwa na mke wake Aisha Chilumba  baada ya kuowa hivi karibuni maendeo ya Vingunguti Dar es salaam

Tuesday, June 23, 2015

BONDIA WA KIKE MWANNE HAJI AWATAKA MABONDIA WA DAR




Na Mwandishi Wetu 

BONDIA wa kike Mwanne Haji ambaye amejitokez kupambana na mabondia kwa kike wa Dar es salaam baada ya kuwasumbuwa sana mabondia wenzake wanaotoka Chunya Mkoa wa Mbeya na sasa kujikita katija jiji lakitokea katika GYM ya Zugo iliyopo Gongolamboto

bondia uyo wa kike ambaye amesha panda uringoni kupambana na baadhi ya mabondiwa wa mkoani amesema amekuja kwa ajili ya mchezo wa msumbwi jijini hivyo mabondia wa kike wakae pembeni kwani sasa ata wasambalatisha mmoja baada ya mwingine 

alitolea mfano wa mabondia wanaotamba Dar es salaam kwa kupigana wenyewe kwa wenyewe kila wakati ni Lulu Kayage,Halima Ramadhani, Fatuma Yazidu

sasa wakae foleni kwani atawapa vipigo mmoja baada ya mwingine bondia uyo mpaka sasa amecheza michezo mitatu ambapo mchezo wake wa kwanza alicheza na Vailet Modest na kufanikiwa kumtwanga kwa point mchezo wake wa pili alicheza na Telesia Kiwale na mchezo wake wa tatu alicheza na Jennifer Pius na kumsambalatisha kwa pointi

hivyo amewaomba mapromota wajitokeza kumsaidi kupambanishwa na mambondia aliowataja hapo juu kwa uzito wa kg 49

mbali na hivyo ametowa wito kwa tasisi mbalimbali pamoja na kmpuni kujitokeza kudhamini mchezo wa masumbwi kwani unapendwa na mashabiki lukuki nchini

Saturday, June 20, 2015

BONDIA WA MOROGORO AOMBA PAMBANO LA NGUMI KWA MAPROMOTA

Na Mwandishi Wetu 

PIUS KAZAULA
BONDIA Pius Kazaula wa Morogoro KG 66 amejitokeza hadharani na kuwaomba wadau wa mchezo wa masumbwi pamoja na mapromota kumwandalia mpambano kwa ajili ya kupima kiwango chake kwa kuwa mapromota wengi wapo Dar es salaam wao wa mikoani wanasahaulika

akizungumza na mwandishi wa habari kwa njia ya simu amesema mabondia wa uzito wake wapo wengi ingawa kila siku wanapangiwa wao kwa wao mana unaweza kukuta bondia mmoja kacheza na mtu mmoja mara nne wakati mabondia wengine tupo mokoani tunafanya mazoezi tu bili kujipima viwango vyetu

hivyo napenda kutoa wito kwa mapromota kujitokeza kutusapoti sisi mabondia wa mkoani ili nasi tujipime na mabondia mnao waamini

najiamini kuwa naweza kazi hivyo nami wasinikwepe kwa kuwa nawataka mabondia wao nasikia Bagamoyo Mkoa wa Pwani nao wanandaa ngumi mara kwa mara wajaribu kutuita na sisi si Dar peke yake mabondia wapo nchi nzima hivyo mapromota kama wana nia kweli ya kukuza mchezo na kuendeleza ngumi chini wawe wanachanganya mikoa mbalimbali 

bondia huyo mwenye makazi yake Morogoro akusita kumpongeza kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa sapoti anayotoa kwa mabondia mbalimbali na kuwapatia vifaa vya masumbwi  kwa galama nafuu na DVD zenye mbinu mbalimbali za mafunzo ya ngumi anazotoa kuelekeza mabondia chipkiz ambao wana kiu ya kuwa mabingwa wa Dunia kupitia mchezo wa masumbwi nchini




Friday, June 12, 2015

NGUMI ZA VUNJA JUNGU KUPIGWA BAGAMOYO JUMAPILI UKUMBI WA TASUBA



DVD ZA SUPER D BOXING COACH ZILIZOPO SOKONI
Na Mwandishi Wetu
 Bondia Shabani Kaoneka sasa atapanda ulingoni juni 14 jumapili hii kukabiliana na Cosmas Kibuga  uzito wa kg 72 baada ya mpinzani wake wa mwanzo Said Mbelwa kuingia mitini akizungumzia mpambano uho mwandaji Muhsin Shaliff amesema kuwa maandalizi ya mpambano uho yamekamilika kwa asilimia 98 kufikia 100

mbali na mpambano uho wenye upinzani mkali kutakuwa na michezo mingine itakayo wakutanisha Adam Ngange wa Chanika na Mfaume Mfaume wa Manzese mpambano wa kg 61 mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa TASUBA uliopo Bagamoyo mjini

siku hiyo pia kutakuwa na bondia Abdallah Pazi 'Mfalme wa wazalamu' atakaepambana na Mrisho Rajabu 'Dame' wakati bondia kutoka Kiwangwa Bagamoyo Iddi Pialali 'Simba aliyejeruiwa' atakumbana na Sweet Kalulu mpambano wa kg 63 raund sita

ngumi zingine zitawakutanisha Raymond Mbwago atapambana na Halidi Honga

siku hiyo pia kutapambwa nja burudani kutoka kwa Jumanne Iddi pamoja na Sam wa Ukweli watakaopamba jukwaa hilo kwa ajili ya burudani za muziki wa kizazi kipyaa 

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Monday, June 8, 2015

NGUMI KUFANYIKA TENA BAGAMOYO JUMAPILI JUNI 14

Na Mwandishi Wetu

MPAMBANO mkali wa masumbwi unatarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii juni 144 katika ukumbi wa TASUBA Bagamoyo mjini mpambano uho utakaowakutanisha mabondia Iddi Pialali wa Kiwangwa Bagamoyo na Sweet Kalulu wa Dar es salaam

akizungumzia mpambano uho mratibu Muhsini Sharif amesema pambano hili litakuwa la raundi sita uzito wa kg 63 mbali na mpambano uho kutakuwa na mipambano mingine ya kumaliza ubisha kati ya Adam Ngange wa Chanika na Mfaume Mfaume kg 61 pamoja na Abdallah Pazi 'Mfalme wa wazalamu' na Mrisho Rajabu 'Dame' kg 74 wa kawe mpambano mwingine ni kati ya Raymond Mbwago na Halidi Hongo kg 63

aliongeza kwa kusema kuwa pia siku hiyo kutakuwa na burudani za nguvu kutoka kwa wasanii Sam Wa Ukweli na Jumanne Iddi ndio watakaotoa burudani kwa siku hiyo

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

MPAMBANO WA VICENT MBILINYI NA SAID MUNDI ULIVYOPIGWA UWANJA WA NDANI WA TAIFA

Bondia Said Mundi kulia akimtupia konde Vicent Mbilinyi wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliopita Mundi alishinda kwa point mpmbano uho wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Vicent Mbilinyi kushoto na Said Mundi wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika wishoni mwa wiki iliyopita katika uwanja wa ndani wa taifa Mundi alishinda kwa point  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Vicent Mbilinyi kushoto na Said Mundi wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika wishoni mwa wiki iliyopita katika uwanja wa ndani wa taifa Mundi alishinda kwa point  Picha na SUPER D BOXING NEWS

MBILINYI KUSHOTO NA MUNDI KULIA WAKISUBILI MATOKEO

Bondia Abdallah Pazi kushoto akipambana na Ibrahimu Tamba wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita  SUPER D BOXING NEWS

Friday, June 5, 2015

MABONDIA VICENT MBILINYI NA SAID MUNDI WA TANGA KUPIGANA KESHO UWANJA WA NDANI WA TAIFA



Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akitunishiana misuli na Said Mundi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpaqmbano wao wa kesho jumamosi utakaofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akipozi kigagwe na Said Mundi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumamosi ya juni 6 katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
 Bondia Vicent Mbilinyi akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Said Mundi wa Tanga kushoto ni mratibu wa mpambano uho Antony Rutta Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Said Mundi wa Tanga akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Vicent Mbilinyi kushoto ni Anton Rutta Picha na SUPER D BOXING NEWS