Tangazo

Pages

Friday, April 18, 2014

MABONDIA WAPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WA APRIL 19 PTA SABASABA JUMAMOSI



Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Mustafa Doto utakaofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mustafa Dotto kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'KIng class Mawe' kabla ya kuzipiga katika ukumbi wa PTA Sabasaba April 19 siku ya jumamosi  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mustafa Dotto kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'KIng class Mawe' kabla ya kuzipiga katika ukumbi wa PTA Sabasaba April 19 siku ya jumamosi  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mfaume Hamad kushoto akitunishiana misuli na Godfrey Sadiki kabla ya kuzipiga katika ukumbi wa PTA Sabasaba April 19 siku ya jumamosi  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' KUSHOTO ALIESIMAMA AKISHUDIA MPINZANI WAKE AKIPIMA AFYA
PROMOTA WA MPAMBANO MUSSA KOVA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MPAMBANO HUO
BONDIA FRANSIC MIYEYUSHO AKIZUNGUMZA
CHICHI MAWE AKIPIMA UZITO
MIYEYUSHO

Manny Pacquiao Ngumi zake nyepesi kama karatasi Wachambuzi watilia shaka uwezo wake Huenda asimvutie mbabe Mayweather


Manny Pacquiao

Ngumi zake nyepesi kama karatasi

 Wachambuzi watilia shaka uwezo wake

 Huenda asimvutie mbabe Mayweather


LAS VEGAS, Marekani

BONDIA Manny Pacquiao amerejea ulingoni na kupigana kwa kiwango bora, lakini alianza kurusha makonde taratibu mithili ya mtoto anayejifunza kutembea.
Hakuwa na kasi iliyozoeleka kama ya mwaka 2008/2009, wakati alipoonyesha umahiri ulingoni mara zote kiasi cha kulinganishwa na enzi za Mike Tyson.
Pacquiao huenda asirudi katika makali hayo tena, lakini ataendelea kuwa moja ya mabondia bora duniani kutokana na kile alichofanya Jumamosi iliyopita mbele ya mashabiki 15,601 kwenye ukumbi wa MGM Grand Garden.
Alimtandika makonde ya kutosha Timothy Bradley, na kushinda kwa pointi 119 dhidi ya 109 na kutwaa taji la WBO ambalo alipoteza kwa mpinzani wake huyo mwaka 2012.
Wengi waliamini bondia huyo raia wa Ufilipino alishinda pambano hilo, lakini majaji walimnyima ushindi.
Pacquiao mwenye sifa ya kutumia vizuri pembe za ulingo wa ngumi alimfumua Bradley na kuzima mbinu zake.
Bradley alimshambulia Pacquiao, kwa kumpiga ngumi kali, na kuelekea kumaliza pambano hilo.
Katika raundi ya nne, alimchanganya Pacquiao kwa kumpiga sumbwi zito kichwani na Pacquiao akainama, lakini Mfilipino huyo aliinuka haraka.
"Nafikiri alifanya vizuri kidogo, lakini hakutarajia ile staili," alisema kocha wa Pacquiao, Freddie Roach. "Ilituogopesha kidogo, kwa sababu tulidhani ameumizwa kwa ngumi. Hatukudhani angerudi nyumbani akiwa anashangilia."
Licha ya maelezo hayo ya Roach, Pacquiao alishindwa kupigana kwa kasi yake kabla ya kuzinduka na kumdunda konde zito la kushoto Bradley, ambalo ilidhaniwa lingemdondosha na kumaliza pambano.
Bradley alisema Pacquiao alimpiga ngumi nzito sana na kuongeza kuwa, makonde mengi ya mpinzani wake hayakuwa makali kama alivyokuwa zamani.
"Ngumi zake hazikuwa za haraka," alisema Bradley, japokuwa amekubali kuwa 'muziki' wa Pacquiao ulikuwa unatisha walipozipiga katika pambano la mwaka 2012.
Lakini matokeo hayaongopi. Tangu 2010 mwanzoni, Pacquiao katika mapambano sita aliyopigana hakuna ambalo ameshinda kwa 'KO'.
Ingawa kocha Roach amesema anachofikiri yeye, "Sumu ya Manny (Pacquiao) bado haijakwisha," lakini ukweli unabaki kama ulivyo ni kwamba madhara ya ngumi zake hayafanani na ilivyokuwa miaka michache iliyopita.
Mabondia hawaugulii maumivu kama alivyokuwa akiwatandika ngumi zake nzito.
"Bado ni bondia bora, dhahiri yupo imara, lakini kwa kawaida, inashangaza ngumi zake zenye nguvu zimeenda wapi," Makamu wa Rais wa Kampuni ya Top Rank, Carl Moretti alisema.
Kilichofanya Pacquiao kuwa miongoni mwa mabondia bora na maarufu duniani ni kuamini 'miguvu' aliyokuwa nayo kipindi alipokuwa anawaangusha wababe wengi wa ngumi.
Alikuwa kamili, anapiga ngumi nzito za kudondosha mpinzani mara moja na pambano kumalizika punde.
Hakuwa bondia mwenye sifa hizo, japokuwa ni miongoni mwa wapiganaji wanaoongoza kwa ubora.
"Pacquiao alipigana vizuri usiku huu na alionyesha alivyojiandaa," alisema Bradley, ambaye aliumia kiwiko cha kulia katika raundi ya kwanza lakini baadaye aligoma kuzungumzia jeraha hilo.
"Jamaa bado anatisha. Moja ya sababu ya kumpenda sana Pacquiao hadharau mpinzani.
"Siku zote anataka kukabiliana na mabondia bora, ambaye mmoja wao amepambana naye usiku huu. Amekuwa bora na ndiyo maana mahiri sana."
Mpaka katika raundi ya sita mabondia hao walikuwa wanakaribiana pointi, Pacquiao alikuwa na 58, mpinzani wake 56. Lakini Pacquiao alicharuka na kuibuka kidedea.
Alitumia vyema raundi ya saba, nane na tisa, 10 hadi ya 12. Licha ya kuongoza, ngumi za Pacquiao hazikuwa kama zile ambazo mashabiki wake walizoea kuziona.
Alifanya kazi yake vizuri, lakini hakuwa na kitu cha pekee kulinganisha na wakati alipopewa hadhi ya kuwa Bondia wa Muongo.
Jambo lingine alikuwa muoga kuingia kwenye mikono ya mpinzani wake kwa kuwa hakutaka kuumizwa, hasa wakati Bradley alipokuwa anarusha makonde, ameshinda lakini si kwa ngumu zenye ladha.
"Sikutaka kuwa mzembe," alisema Pacquiao, ambaye alipigwa kwa 'KO' mwaka 2012 na Juan Manuel Marquez na alipoteza fahamu kwa muda kutokana na kupigwa konde la kulia kichwani.
Kulingana na orodha ya mabondia bora, ni wazi Pacquiao yumo, lakini hamfikii hata chembe hasimu wake, Floyd Mayweather.
Kiwango kimeporomoka, japo, Pacquiao kuna wengine wanasema ni 'nusu Tyson'. Amebakisha miezi michache kufanya sherehe ya kutimiza miaka 36 na mpaka akipanda ulingoni tena inapita miaka tangu aliposhinda kwa 'knockout'.
Kwa umri wake bado ana nafasi ya kujirekebisha kwa kufanya 'tizi' gumu na kurudisha mvuto kwa mashabiki wake hata kulipa viiingilio vikubwa kwa ajili ya kuona mapambano yake.
Floyd Mayweather bondia anayetajwa kuwa ni bora wakati wote ulimwenguni katika uzani anaocheza, huenda asipigane na Pacquiao kutokana na kiwango cha kawaida kilichoonyeshwa na Mfilipino huyo.
Japokuwa Pacquiao amekaribisha ombi la bondia yeyote mwenye nia ya kupigana naye, huku akimlaumu Mayweather kwa kupiga chenga miaka mingi kuhusu pambano lao, hakupigana kiasi cha kumshawishi Mmarekani huyo atamani wazipige.
Mayweather hakuwepo ukumbini wakati wa pambano hilo hali inayotia wasiwasi kama atakubali kucheza na Pacquiao. Nafasi nyingine ipo kwa Marquez, ambaye kama atakubali kudundana na Pacquiao, itakuwa mara ya tano.
Mfilipino huyo katika pambano lake la wiki iliyopita alichanika nyama ya juu ya jicho na kushonwa nyuzi kadhaa.
HISTORIA YAKE
Pacquiao alizaliwa Desemba 17, 1978, huko Kibawe, Bukidnon, Ufilipino.
Ni mtoto wa Rosalio Pacquiao na Dionesia Dapidran-Pacquiao. Wazazi wake waliachana wakati bondia huyo alikuwa darasa la sita, baada ya mama yake kubaini mumewe alikuwa anaishi na kimada.
Mtoto wa nne kati ya sita kutoka tumboni kwa mama yake: Liza Silvestre-Onding na Domingo Silvestre (ndugu zake waliozaliwa kwa mume wa kwanza wa mama yake) na Isidra Pacquiao-Paglinawan, Alberto "Bobby" Pacquiao na Rogelio Pacquiao.
Pacquiao ni mume wa Maria Geraldine "Jinkee" Jamora, na wamezaa watoto wanne: Emmanuel Jr. "Jimuel", Michael, P

rincess, na Queen Elizabeth "Queenie."
Anaishi kwenye mjengo wake huko General Santos City, Kusini mwa Cotabato, Ufilipino.
Baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Sarangani, kwa sababu za kiofisi amehamia Kiamba, Sarangani, nyumbani kwa mke wake.
Ni muumini wa dhehebu la Kanisa Katoliki, Pacquiao ingawa katika siku za karibuni anasali katika kanisa la Waprotestant.

MAKALA HII KWA HISANI YA BURUDANI.
NA BAADHI YA DVD ZAKE ZA BONDIA HUYO PACQUAIO

Wednesday, April 16, 2014

CHICHI MAWE KUCHEZA MICHEZO MIWILI NDANI YA MWEZI MMOJA


MPAMBANO wa masumbwi wa bondia Fransic Miyeyusho na mohamed Matumla sasa utafanyika Mei 10 katika ukumbi wa PTA Sabasaba mpambano huo uliokuwa ufanyike April 26 sasa umesogezwa mbele
kumpisha bondia Miyeyusho ili acheze vizuri mpambano wake wa kimataifa unao mkabili dhidi ya Bondia Sukkasem Kietyongyuth  kutoka Thailand mpambano utakaofanyika April 19 katika ukumbi wa Pta sabasaba
mpambano uhoutakaosindikizwa na ngumi za wanawake ambapo bondia Lulu Kayake atavaana na Halima Ramadhani katika kuhakikisha mchezo wa masyumbwi kwa wanawake unahamasishwa vizuri
mshindi katima mpambano wa matumla na miyeyusho atapata nafasi ya kupata meneja kutoa katika kampuni ya Mwazoa  Promosheni kutoka Tanga
akizungumzia maandalizi ya mpambano huo promota amesema kua mpambano huo utachezwa mei 10 katika ukumbi huo wakatik huohuo aliongeza kwa kusema
mpambano mwingine mkali utawakutanisha mabondia Kalama Nyilawila na Thomas Mashali siku ya mei mosi mwaka huo katika ukumbi wa PTA sabasaba aliongeza kuwa katika michezo hiyo kingilio ni 7000, na 10,000 kwa viti maalumu na mchezo huo utachezwa kivyovyote iwe mvua iwe jua kwani akuna kitu kitakachoweza kuzuia mpambano usifanyike kwa kuwa tunatumia uwanja mkubwa na uwanja wa ndani hivyo mashabiki wasisite kuja katika mechi hizo ambazo zina upinzani wa ali ya juu
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha


--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

CHICHI MAWE AJIFUA KUMKABILI MTHAILAND APRIL 19 NA MOHAMED MATUMLA MEI 10 PTA SABASABA



 Kiongozi wa Lazima Ukae GYM Gulamu Kassim kushoto akipambana na bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' wakati wa mazoezi yake yanayoendelea katika kambi hiyo iliyopi Kinondoni Dar es salaam Miyeyusho anajiandaa na mpambano wake na  Bondia Sukkasem Kietyongyuth  kutoka Thailand April 19 na Mohamed Matumla Mei 10 mipambano yote itafanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe'  kulia akipangua konde la Gulamu Kassim
wakati wa mazoezi yake yanayoendelea katika kambi ya lazuima ukae GYM iliyopo Kinondoni Dar es salaam Miyeyusho anajiandaa na mpambano wake na  Bondia Sukkasem Kietyongyuth  kutoka Thailand April 19 na Mohamed Matumla Mei 10 mipambano yote itafanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Kiongozi wa Lazima Ukae GYM Gulamu Kassim kushoto akimwelekeza bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' jinsi ya kutupa makonde wakati wa mazoezi yake yanayoendelea katika kambi hiyo iliyopi Kinondoni Dar es salaam Miyeyusho anajiandaa na mpambano wake na  Bondia Sukkasem Kietyongyuth  kutoka Thailand April 19 na Mohamed Matumla Mei 10 mipambano yote itafanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Tuesday, April 15, 2014

DVD MYA ZA NGUMI ZAINGIA NCHINI SASA ZINAPATIKANA

 DVD INAYOPENDWA NA WADAU WENGI WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI IKISHILIKISHA BONDIA MANNY PAQUAIO  SASA ZINAPATIKANA KWA WINGI MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI KAriakoo dar es salaam zaidi piga simu 0713406938,0787406938 au unaweza kutembelea www.superdboxingcoach.blogspot.com

DVD KUTOKA SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION

DVD INAYOPENDWA NA WADAU WENGI WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI IKISHILIKISHA MABONDIA MANNY PAQUAIO NA JUAN EMANUEL MARQUEZ 4 SASA ZINAPATIKANA KWA WINGI MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI KAriakoo dar es salaam zaidi piga simu 0713406938,0787406938 au unaweza kutembelea www.superdboxingcoach.blogspot.com

DVD YA BONDIA ROGERS MTAGWA BONDIA MTANZANIA ANAEFANYA SHUGHULI ZAKE NCHINI MAREKANI AMBAPO KATIKA DVD HII KUNA MECHI ZAKE TOFAUTI TOFAUTI PAMOJA NA MATUKIO MBALIMBALI AKIWA USA SASA ZINAPATIKANA

dvd mpya kutoka super d boxing coach and promotion

DVD MPYA INAYO MUHUSISHA CHICHI MAWE VS JOSHUA AMOKULU WA KENYA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE VS MUSTAFA DOTO  NA SIMBA WATUNDULU LINGINE FADHILI MAJIA VS ANTONY MATHIAS NA JUMA SELEMANI MAPAMBANO YOTE YAKIWA KATIKA DVD MOJA SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI ULIZA SUPER D AU PIGA SIMU 0713406938

DVD MPYA INAYO MUHUSISHA CHICHI MAWE VS JOSHUA AMOKULU WA KENYA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE VS MUSTAFA DOTO  NA SIMBA WATUNDULU LINGINE FADHILI MAJIA VS ANTONY MATHIAS NA JUMA SELEMANI MAPAMBANO YOTE YAKIWA KATIKA DVD MOJA SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI ULIZA SUPER D AU PIGA SIMU 0713406938
DVD YENYE MAPAMBANO MENGI YA FLOYD MAYWEATHER JR HII HAPA

DVD YENYE MAPAMBANO MBALIMBALI

Sunday, April 13, 2014

NGUMI KUPIGWA CHALINZE MJINI APRIL 15 NDELEMA INN


ERICK MAGANA
 MCHEZO wa ngumi utachezwa Chalinze mkoa wa Pwani katika ukumbi wa Ndelema Inn ukiwakutanisha mabondia Erick Magana kutoka Dar es salaam atakae oneshana umwamba wa kutupiana makonde na Mwaite Juma siku ya April 15  katika ukumbi wa Ndelema Inn Chalinze Mjini


mpambano huo wenye upinzani mkubwa wa ali ya juu unaosubiliwa na wapenzi wa ngumi Chalinze Mkoa  wa pwani pamoja na vitongoji vya jirani utakuwa chachu ya kuhamasisha mchezo uho kwa ajili ya kuibua vipaji vipya vya mchezo wa ngumi katika mkoa mzima wa pwani
mbali ya mpambano huo kutakuwa na mipambano mingine ya utangulizi ambayo watapata wapinzani wao baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano huo utakaowakutanisha mabondia wa chalinze na Dar es salaam

mabondia ambao watatoka Dar kwenda kupambana na wenzao wa chalinze ni Erick Magana,Godfrey Sadiki 'Pacho Mawe',Juma Biglee,Husein Pendeza,Hamisi Kavirondo ambao wata ongozana na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' 

kwa ajili ya kwenda kushiriki mashindano hayo ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi nchini mchezo ambao unapendwa na wengi duniani
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha


JUMA BIGLEE


Saturday, April 12, 2014

MANNY PAQUAIO AMSHINDA TIMOTHY BRADLEY KWA POINT

 Bondia Manny Paquaio kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Timothy Bradley wakati wa mpambano wao uliofanyika leo alfajili manny pac alishinda kwa point
Bondia Timothy Bradley kushoto akipambana na Manny Pacquiao wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa WBO welterweight champion uliofanyika alfajili ya leo katika ukumbi wa MGM Grand in Las Vegas, Nevada. USA  Paquaio alishinda kwa pointi katika mchezo uho wa marudiano
Bondia Manny Paquaio kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Timothy Bradley wakati wa mpambano wao uliofanyika leo alfajili manny pac alishinda kwa point
Bondia Timothy Bradley kushoto akipambana na Manny Pacquiao wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa WBO welterweight champion uliofanyika alfajili ya leo katika ukumbi wa MGM Grand in Las Vegas, Nevada. USA  Paquaio alishinda kwa pointi katika mchezo uho wa marudiano