Tangazo

Pages

Saturday, January 25, 2014

MABONDIA WAPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WAO WA JUMAPILI YA JANUAR 26 MANZESE


Bondia Muss Chitepete kushoto akitunishiana misuli na Ramadhani Shauli wakati wa upimaji wa uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumapili ya january 26 katika ukumbi wa Friends Corner Manzese Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Muss Chitepete kushotoakipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Ramadhani Shauli kulia
Mabondia Bakari Magona 'Beka Ostadhi' kushoto akitunishiana misuli na Juma Fundi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumapili ya january 26 katika ukumbi wa Friends Corner Manzese Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MJUE KWA UNDANI BONDIA AMIR KHAN





Amir Khan:
LEO katika safu hii ya maisha ya wenzetu tutakuwa tukiangazia maisha ya mwanamasumbwi, Amir Abdul Khan ambaye amepata kupendwa na kuwashika mashabiki wengi wa mchezo huo kutokana na umahiri, uwezo na mbwembwe anazokuwa anazifanya pindi  anapokuwa ulingoni.
Mbabe Khan ambaye ni raia wa Uingereza alikuwa bingwa wa dunia wa uzito wa WBA, WBA (Super) ikiwa ni pamoja na IBF, hivi sasa ameonesha nia ya kutaka kupambana na mbabe asiyepigika Floyd Mayweather Jr.
Zipo kila dalili zinazoashiria kwamba wawili hawa watachapana kutokana na kauli ambayo imewahi kutolewa na Mayweather Jr mwaka jana baada ya kumchapa Saul ‘Canelo’ Alvarez alisema kuwa anatarajia hadi kufikia Septemba mwakani awe amecheza mapambano manne na ya kwanza kuanza nayo ni mawili ambayo miongoni mwao yatakuwa kati yake na Amir Khan au bondia wa Argentina Marcos Maidana.
USICHOKIJUA
Ingawa watu wengi hufikiria kwamba Khan ni raia wa nchi za Asia lakini kijana huyo amezaliwa na kukulia Bolton, England, na wazazi wenye asili ya kipakistan wanaotokea katika jamii ya Punjab.
Khan ni muumini wa dini ya kiislam, na amekuwa akisaidia katika kuiwezesha tuzo inayotolewa na waislama wa nchini humo inayokwenda kwa jina la ‘Muslim Writers Awards’.
han anatoka katika familia yenye watoto wanne ambako ana dada wawili na kaka mmoja, Haroon ‘Harry’ Khan, mbabe asiyepigika.
Amir Khan ni mdogo wa mbabe na mshindi wa medali ya Olympic ya Uingereza, mshindi wa medali ya fedha ya olimpiki ya mwaka 2004 wakati akiwa na miaka  17.
Khan ana historia ya kukamata ubingwa wa dunia wa WBA akiwa na umri mdogo kuliko mwingireza mwingine wakati huo aliuchukua akiwa na miaka 22.
Ukiachilia ngumi ni mpenzi wa mchezo wa Kriketi, mpira wa kikapu na soka akiwa shabiki wa klabu ya Bolton Wanderers.
Mwaka 2012, alikuwa katika picha ya pamoja katika akaunti yake ya Twitter ikimuonesha akiwa na wachezaji wa Manchester United, Rio Ferdinand, Alex Buttner, Michael Carrick na David De Gea.
Lakini pamoja na kuonekana akiwa na nyopta hao huku akiwa amevaa jezi ya klabu hiyo lakini Khan alisema kuwa 'pamoja na kufanya hivyo lakini mimi bado ni shabiki wa klabu ya Bolton kwa njia yoyote.'



MSAADA WA KIJAMII
Khan amekuwa mtoaji mzuri wa misaada kwa watu wenye mahitaji kwa mfano mwaka 2004 alitoa msaada wa Euro milioni 1 kwa familia za wahindi waliokumbwa na tetemeko la Tsunami nchini India.
Katika mwaka huo alikwenda nchini Pakistan na kutoa vyakula katika kambi za watu waliokuwa wameathiriwa na tetemeko la Kashmir.[
Desemba 2013, Khan aliongoza harambee ya kuchangia Umoja wa waislam kutoka Ufilipino kwa ajili ya kutoa msaada wa waathirika wa tetemeko la Typhoon Haiyan na walikusanya kiasi cha Euro 83,400.
JINAI
Oktoba 23, 2007 Khan alitiwa mbaroni kwa kuendesha kwa kasi na alifikishwa katika mahakama ya Bolton kujibu shtaka lake ambako alifungiwa kuendesha gari kwa muda wa miezi sita ikiwamo na kupigwa faini ya euro 1000.
Mwaka 2006 aliwahi kupigwa faini ya Euro 40,000 kwa kosa la kuendesha kwa kasi.
Januari 7, 2008 Khan alipigwa faini ya Euro 1000 na kufungiwa kuendesha gari kwa siku 42.
Kama ilivyokawaida mwenye tabia yake hawezi kuacha Julai 12, 2009 Khan alijikuta akipata ajali ingawa hakufikishwa katika vyombo vya sheria.
 
MAHUSIANO
Januari 29, 2012 Khan alifunga ndoa na mwanamke wa Marekani mwenye asili ya Pakistani, Faryal Makhdoom katika harusi ya kifahari iliyohudhuriwa na ndugu na marafiki waliofikia 1000 akiwamo bondia Ricky Hatton.
Wawili hawa walifanya sherehe ya harusi yao Mei 31, 2013 huko Waldorf Astoria jijini New York, Marekani.
Baada ya kumalizika kwa sherehe hiyo ya kifahari wawili hawa walichukua ndege na kwenda nyumbani kwao na Khan huko Bolton kwa ajili ya kufanya sherehe nyingine ya kimila iliyofanyika Manchester na kuhudhuriwa na wageni 4,000.
FEDHA
Mbabe Amir Khan  anamiliki utajiri unaofikia dola milioni 23 (sawa na shilingi bil 36.8).
MAKAZI
Mbabe Amir Khan ana mjengo wa maana ambao hajaweka thamani yake lakini pia anamiliki gari mbalimbali ikiwamo Range Rovers, Bentley Continental, New Mercedes CLS63, Audi R8, Lamborghini Murcielago na Can-Am Spyder.
WASIFU
JINA: Amir Iqbal Khan ‘King’
KIMO: Futi 5 na inchi 9
UMRI: 27
Mapambano ya kucheza: 31
Ushindi: 28
KO:     20
Poteza:    3
Sare: 0

Thursday, January 23, 2014

MKUTANO MKUU WA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA KUFANYIKA FEB MOSI


TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
Siku ya terehe 1 ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni KUANZIA SAA TATU NA NUSU ,kutakuwepo na mkutano mkubwa wa wanamasumbwi wote ulioitishwa na orgnaizesheni ya ngumiza kulipwa Tanzania (TPBO) kwa lengo la kuwakutanisha mapromota wote,mabondia na makocha  wa ngumi wote kwa lengo la kujadili ngumi za kulipwa zinapoelekewa,kujuana na kuelimishana sheria za ngumi za kulipwa  zinavyotumika kinyume na sasa ,sheria nyingi zinafungiwa macho na kutumia uzoefu zaidi kuendesha mgumi nchini.  Mkutano huo ulioitishwa na Rais wa TPBO bw  Yasin Abdallah akishirikiana  na Ibrahim kamwe na Mapromota wa ngumi chini ya ufadhili wa kitwe Traders unatarajiwa  kuwa mkutano wa kwanza  kuwakutanisha mapromota wote pamoja na  mabondia wa ngumi  za kulipwa wa hapa nchini ili kuboresha ngumi na kuhamasisha wadhamini na makampuni wajitokeze kuudhamini mchezo huo ,ambao ndio mchezo unaoliletea mataji na  sifa Tanzania katika medani za kimataifa lakini hauna udhamini  wowote ,mpaka sasa ni mchezo  ambao unaojiendesha wenyewe kwa nguvu za  wadau wachache wachovu  na mabondia wenyewe ambao uwezo wao ni mdogo sana kukikidhi matakwa kamili ya mchezo wenyewekam ilivyo kwa wenzetu,ni mchezo  ambao una huduma nyingi zinazohitaji nguvu ya wadhamini ili  uendelee kuboreka zaidi.
Akizungumza na vyombo vya habari katibu wa ngumi za kulipwa nchini bw Ibrahim kamwe , amesema imewaalika viongozi wa baraza la michezo (BMT), na viongozi wengine wote wa ngumi za kulipwa watakuwepo kama vile Emmanuel mlundwa,names kavishe,  makaranga,Onesmo ngowi,kinyogoli,  matumla, Zuwena kibena(mama zugo) na viongozi wadau wa karibu na ngumi wamealikwa kuhudhulia mkutano huo ambao utafanyika Siku ya terehe moja ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni. hivyo kamwe alimaliza kwa kuwaomba kila anaejijua kuwa yeye ni bondia wa ngumi za kulipwa na promota wangumi  ahudhurie bila kukosa mkutano huu muhimu sana kwa wamasumbwi ya nchi  yetu

TUZO ZA TANZANIA BOXING AWARDS WAENDELEA KUHAMASISHA MASHABIKI MBAGALA

Bondia Abuu Abas kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Abdul Zugo wakati wa uhamasishaji wa tuzo za PSPF Boxing Award zilizofanyika katika viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es salaam tuzo hizo zinafika tamati january 25 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Zugo alishinda kwa K,o ya raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Hamisi Mpili kushoto akichuana na Khalfani Jumamane wakati waq mpambano wa uhamasishani wa tuzo za PSPF Tanzania Boxing Awards zinazofika tamati january 25 katika ukumbi wa PTA Sabasaba jumanne alishinda kwa point mpambano huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
MJUMBE WA BFT AISHA MZUNGU AKISALIMIA MASHABIKI WALIOJITOKEZA KATIKA KUANGALIA MIPAMBANO YA MASUMBWI YA KUHAMASISHA TUZO ZA BOXING AWARDS KATIKA VIWANJA VYA zakhem mbagala kushoto ni mjumbe mwingine Zuwena Kibena 'Mama Zugo'

wajumbe wa shilikisho la ngumi za ridhaa wakifatilia mpambano wa masumbwi kutoka kushoto ni Asisha Mzungu, Zuwena Kipingu 'Mama Zugo' na Antoni Mwangonda

Rais wa shirikisho la ngumi za ridhaa nchin Mutta Rwakatale akisalimiana na mjumbe wa shilikisho hilo Zuwena Kipingu

Rais wa shirikisho la ngumi za ridhaa nchin Mutta Rwakatale akisalimiana na mjumbe wa shilikisho Aisha Mzungu



WANDISHI WA HABARI WAKIFATILIA MPAMBANO WA MASUMBWI

BAADHI YA MASHABIKI WALIOJITOKEZA KWENYE VIWANJA VYA ZAKHEM MBAGALA KUANGALIA BURUDANI ZA MASUMBWI

Tuesday, January 21, 2014

TUZO ZA PSPF BOXING AWARDS ZAZIDI KUHAMASISHWA

Bondia Antony Edowa kushoto akipambana na Gervas Regasiano wakati wa mchezo wao kwa ajili ya kuhamasisha tuzo za PSPF Tanzania Boxing Awards zilizofanyika nje ya uwanja wa karume karibu na soko la mitumba mchikichini Regasiano alishinda kwa point mchezo huo Picha na www.superdboxingcoac.blogspot.com

BAADHI YA VIONGOZI WA TUZO ZA PSPF TANZANIA BOXING AWARDS WAKIFATILIA MCHEZO WA WAZI ULIOFANYIKA NJE YA UWANJA WA KARUME KARIBU NA SOKO LA MITUMBA MCHIKICHINI KWA AJILI YA KUHAMASISHA TUZO HIZO ZINAZOFIKIA KILELE CHAKE JANUARY 25 KATIKA UKUMBI WA PTA SABASABA

Bondia Antony Edowa kushoto akipambana na Gervas Regasiano wakati wa mchezo wao kwa ajili ya kuhamasisha tuzo za PSPF Tanzania Boxing Awards zilizofanyika nje ya uwanja wa karume karibu na soko la mitumba mchikichini Regasiano alishinda kwa point mchezo huo Picha na www.superdboxingcoac.blogspot.com

Bondia Gervas Regasiano akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wake baada ya kumtwanga Antony Edowa

Na Mwandishi Wetu

MCHEZO wa mwisho kwa ajili ya kuhamasisha ngumi unatarajia kufanyika siku ya alhamisi ya january 23 katika viwanja vya wazi vya Zakhem mbagala Dar es salaam mapambano hayo ya ngumi yenye lengo la kuhamasisha tuzo za PSPF Tanzania Boxing Awards ambazo zinafikia tamati january 25 kwa washindi kupatiwa tuzo hizo zitakazofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam

akizungumza na waandishi wa habari makamu wa rais wa shirikisho la ngumi za ridhaa nchini Lukelo-Willilo amesema utoaji wa tuzo hizo zitaongozwa na burudani mbali mbali na mapambano ya masumbwi ya mabondia wa ridhaa na kulipwa ambao wataoneshana uwezo siku hiyo alitaja burudani zitakazokuwepo siku hiyo kuwa na FM Academia, Malkia wa Mipasho Khadija Kopa, Excel one band,tom ongala, na kantona mgogo wa mazizi ndio burudani zitakazo tolewa kwa iku hiyo na mgeni rasmi

hatakuwa  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fennela Mukangara ambaye atakukuwa akishudia kwa mara ya kwanza kabisa tuzo hizo  zinazoshirikisha mabondia mbalimbali 

na namna ya kupiga kula kuchagua bondia bora wa mwaka 2013,2014 unandia NGUMI (ACHA NAFASI)  andika namba ya mshiriki iliyoorodheshwa kwenye jina lake,kisha tuma kwenda namba 15573 kwa mfano ngumi 49 kwenda 15573 itakugalimu T.sh 150 kwa kila SMS  na unakumbushwa kupiga kula zaidi kadri 
uwezavyo kufanikisha  mwakilishi wako ananyakuwa tuzo hiyo 

Monday, January 20, 2014

BONDIA WA UZITO WA JUU IDDI BONGE AJIANDAA KUMKABILI MWAKASANGA MARCH 23


Kocha wa mchezo wa ngumi Kwame Mkuluma kushoto akimwelikeza jinsi ya kupiga ngumi bondia Iddi Kipandu 'Iddy Bonge' wakati wa mazoezi yanayoenderea kwa ajili ya mpambano wake wa march 23 na David Mwakasanga utakaofanyika ukumbi wa frends corner Manzese mazoezi hayo  katika klabu ya biafra iliyopo kigogo mburahati Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa mchezo wa ngumi Kwame Mkuluma kulia akimwelikeza jinsi ya kupiga ngumi bondia Iddi Kipandu 'Iddy Bonge' wakati wa mazoezi yanayoenderea kwa ajili ya mpambano wake wa march 23 na David Mwakasanga utakaofanyika ukumbi wa frends corner Manzese mazoezi hayo 
 katika klabu ya biafra iliyopo kigogo mbulahati Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MABONDIA WATWANGANA DAME GYM MANZESE

Bondia Rashidi Palasa  kushoto akijitutumua kupiga  ngumi bila mafanikio wakato wa mpambano wake na Jumanne Saleh uliofanyika jana katika ukumbi wa Ndame GYM uliopo Manzese ilimahewa Dar es salaam Saleh alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

BONDIA RASHIDI PALASA AKITAMBA JUKWAANI KWA MWNDO WA MADAHA ATA HIVYO ALOAMBULIA KIPIGO KWA POINTI

BONDIA JUMANNE SWALEH AKITANGAZWA MSINDI NA REFARII KONDO NASSORO BAADA YA KUMGALAGAZA KWA POINT RASHIDI PALASA WAKATI WA MPAMBANO WAO

Bondia Ibrahimu Tamba kushoto akipiga makonde ya nguvu kwenda kwa mpinzani wake Tyson Kushi wakati wa mpambano wao uliofanyika jana katika ukumbi wa Ndame GYM manzese Kilimahewa Dar es salaam Tamba alishinda K,O ya raundi ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Julius Kisarawe kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Uwesu Mtulia wakati wa mpambano wao uliofanyika jana Kisarawe alishinda kwa K,o ya raundi ya pili Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com