Tangazo

Pages

Wednesday, September 18, 2013

DVD MPYA KUTOKA KWA SUPER D BOXING COACH HIZI HAPA

MPAMBANO AMBAO ULIWAKESHESHA WATU MACHO MIMI NIKIWA NI MMOJA WAO
Saul 'canelo' alverez bondia mkari kwenye dvd hii unapata gem zake nne pamoja na historia yake ya ngumi na ndie bondia anaekubalika zaidi mexico



CHAMPIONI LATOA MSAADA, MATUMLA AANZISHE SHULE YA MCHEZO WA NGUMI





Mhariri wa Championi Ijumaa, John Joseph akimkabidhi glovu mbili, bondia mkongwe nchini Rashid Matumla. Vifaa hivyo vimetolewa na gazeti la Championi ukiwa ni msaada kwa Matumla kwa ajili ya kusaidia ndoto yake ya kuanzisha shule ya ngumi.

Wengine katika picha hiyo ni Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally (wa pili kulia) aliyeratibu zoezi hilo.  Wanaoshuhudia ni waandishi wa gazeti hilo, Wilbert Molandi na Martha Mboma.
 
AKIWA NA SALEHJEMBE
Matumla amekuwa na ndoto ya kuanzisha shule ya ngumi lakini hana mtaji, hata Championi halijatoa vifaa vya kutosha, lakini uongozi wa gazeti hili umekuwa ukisisitiza wadau wajitokeze zaidi kumsaidia Matumla kutimiza ndoto yake.
 
AKIWA NA JOHN JOSEPH
Bingwa huyo wa zamani wa dunia mara mbili, amekuwa akiandamwa na ugonjwa wa ganzi na maumivu makali kwenye uti wa mgongo na daktari amemshauri kutoendelea kupigana ili kuokoa maisha yake.
Matumla amesema anaweza kuendeleza maisha yake kwa kufungua shule ambayo anaamini itazalisha wachezaji wengi nyota wa mchezo wa ngumi.
Championi limeamua kumsaidia katika hilo na kuendelea kuhimiza wadau kujitokeza zaidi kumsaidia ili atimize ndoto hiyo kwa kupata vifaa na kulipa pango angalau la mwaka, angalau aanzishe Matumla Boxing School.
PICHA NA KHATIM NAHEKA

Tuesday, September 17, 2013

BFT: TUNASUBIRI BARUA KUTOKA AIBA KWAAJILI YA MASHINDANO YA KLABU BINGWA YA KIMATAIFA



Na Elizabeth John


SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), linasubiri barua kutoka Shirikisho la Ngumi Duniani (AIBA) kwaajili ya kujulishwa tarehe mpya ya mashindano ya ubingwa wa Afrika ambayo yanatarajiwa kufanyika huko Mauritius.
Awali mashindano hayo yalipangwa kufanyika Septemba mosi hadi 7 nchini humo kabla AIBA hawajahairisha kutokana na sababu ambazo zimeelezwa kwamba zipo nje ya uwezo wao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema timu ya taifa inaendelea na mazoezi ya kujifua kwaajili ya mashinndano hayo katika uwanja wa ndani wa taifa.
“Timu ipo vizuri kwaajili ya mashindano hayo, bado inaendelea na mazoezi kama kawaida bado hatujajua ni lini mashindano hayo yataanza tunasubiri barua kutoka AIBA tukipata taarifa tutatangaza,” alisema.

Mashaga aliwaomba watanzania wajitokeze zaidi kusaidia timu yetu ya taifa ili uwakilishi katika mashindano ya kimatifa uwe wenye tija kwa kuzingatia kuwa watanzania wote ndio wanachohitaji na ili kitimie mabondia lazima waandaliwe vema.

FLOYD MAYWEATHER SASA KUZIPIGA NA AMIR KHAN



BAADA ya kumchakaza Canelo Alvarez, bondia Floyd Mayweather ‘Cash Money’ anamtaka bondia wa England, Amir Khan katika mpambano unaofuata.
Kituo kinachoonyesha mapambano ya ngumi ya Mayweather cha Showtime Sports kimetoa taarifa kuwa kuna uwezekano wa bondia huyo kupambana na Khan ambaye anayatajia kutetea taji lake la IBF uzito wa welter na Devon Alexander mwezi Desemba mwaka huu jijini New York.
Mapambano mawili kati ya sita ya Mayweather yataonyeshwa moja kwa moja kupitia kituo hicho na Mkurugenzi wa Showtime Sports, Stephen Espinoza alisema kuwa wanapenda kuona mpambano huo unafanyika.
Mkurugenzi huyo amepoendekeza mpambano huo unaweza kufanyika Uingereza. "Amir Khan ni mpinzani mzuri wa Floyd Mayweather, kwa sababu ana kasi ulingoni," alisema Espinoza.
"Mpambano huo wa kuvutia unaweza kufanyika Uingereza au New York. Floyd amezungumzia uwezekano wa kufanyika kwa mpambano huo sehemu moja kati ya hizo mbili.
Kama Khan akikubali kupambana na Mayweather, analipwa fedha nyingi sana ambazo anaweza kuwa hajawahi kupata katika maisha yake ya ngumi.
Alvarez alipata pauni 7.9 milioni poamoja na kupoteza mpambano huo. Espinoza alisema kwamba Khan anaweza kuwaongezea soko kubwa katika mpambano huo kuliko ilivyokuwa kwa Alvarez.

Monday, September 16, 2013

MABONDIA TUNAPONZWA NA NJAA ZETU ZA MAISHA

Asili ya mabondia wengi  duniani wanatoka katika familia duni kwa mfano hapa kwetu ni aghalabu kumkuta bondia ametoka upanga,oysterbay, au masaki ushuwani.nikiwa na maana  mabondia wengi wanatoka uswahilini ni watu wa hali duni wengi wetu hatujakalia madawati ya shule wengine tuliojitahidi tumefika darasa la tano au sita kama wazazi walikomaa ndio tunamaliza la saba. Baadhi yetu tukiwa na umri wa kuanzia miaka sita nyumbani huwa tunaanza kupewa uzowefu wa kuuza visheti,maandazi,vitumbua,karanga nk na vikibaki nyumbani hauli chakula mpaka viishe, shuleni mwalimu mkali, darasani afundishi mpaka usome tuisheni ndio unapata kufundishwa kidogo na ukishindwa maswali yake viboko vya ghazabu ,hapo ndipo tunapoamua kuachana na shule na kutinga mitaani.  michezo yetu ni katika madampo na vichochoroni na tukifikia umri wa kuanzia miaka 12 na kuendelea tunajua jinsi ya kutafuta pesa kwa kuuza njiwa,kucheza kamari,malani,kuiba kuku na bata , na kwa wale walio watukutu zaidi kuuza na kuvuta bangi ni sehemu ya maisha ya kawaida tu huku mitaani kwetu. mara nyingi mlo kwetu ni mmoja tu kiubishoo au kuwa wageni ndio tunakula milo miwili. Katika maisha yetu muda mwingi tupo huru na michezo kuliko kusoma hasa kolokolo,ngoma,mpira na ngumi, mpira tunacheza mabarabarani ,vichochoroni na madampo wakati ngumi tunajifundisha katika makamali vichochoroni au uwani kwa kina masta, begi au tairi limefungwa juu ya  mti tizi linaendelea bila vifanyio vya mazoezi vilivyo rasmi mwendo mdundo tunasonga na tunashinda au kufanya vizuri  katika mashindano yetu tunayoshiriki na hali yetu duni hihi hii ya kimaisha, na majina yetu kutangazwa sana katika vyombo vya habari na kupata umaarufu mkubwa nchini,nchi jirani  na hata nchi za ulaya.lakini ukibahatika kututembelea na kuangalia tunapoishi na familia zetu na umaarufu tulionao maisha yetu mabovu yanasikitisha .
siku za hivi karibuni kuna vimaendeleo kidogo baadhi ya mabondia tunafanya mazoezi katika vilabu vya pombe kwa kuwalipa kodi ya mazoezi wenye bar .naweza sema Tanzania hakuna sehemu rasmi  za kufanyia mazoezi ya ndani zilizotengwa na serikali kwa ajili ya raia wake wapenda michezo na kama zipo ni chache katika makambi ya jeshi kwa masharti magumu kwa raia wa kwawaida. Siku za nyuma wakazi wa mjini kama vile kisutu,gerezani na kariakoo walikuwa wanafanya mazoezi pale anatoglu,siku hizi huwezi kusikia kuna mwanamichezo katokea gerezani au kariakoo,iliyobaki kwao ni kuuza na kutumia madawa ya kulevya na kukimbizana na wafanyabiashara wa maeneo hayo, naweza ilaumu serikali kwa kutoendeleza michezo bali ilishiriki kuuwa kabisa michezo maeneo hayo na mengineyo zaidi.
Kwa sisi tulionza kukuwa kimchezo Pambano la ngumi likiandaliwa huwa tunalipwa kuanzia shilingi alfu 5 mpaka 20 kwa mapambano haya madogomadogo na iwapo kutakuwa na pambano kubwa na kupata bahati ya kucheza unaweza lipwa shilingi alfu 40 mpaka laki moja.mapambano makubwa yanaweza kuwa moja,mawili au matatu kwa mwaka hayazidi hapo, haya mapambano madogo tunaweza pata mawili mpaka sita kwa mwaka. Msiwaone mabondia wakicheza mkadhani wana kipato kikubwa la hasha, ni wale tu wachache waliobahatika kupata wadhamini au waratibu wenye uwezo wa kipesa ndio kidogo hutoka.
Kwa sisi wengine ukiangalia elimu ya kusoma hatuna kazi hakuna na mchezo wa ngumi tunaupenda na pengine tuna vipaji na kwa kufanya vizuri katika mapambano yetu,hivyo mchezo ndio huwa kama ajira zetu kwa sababu tunapata chochote kidogo kupitia mchezo huo kuliko kuiba au kukimbizana na mapolisi katika kamari na kuishia jela.
Kwetu sisi mabondia huona ni jambo la kifahari na hufurahi mno pale tu tunapopata pambano la nje ya nchi na hufurahia kupanda ndege na vile vimisosimisosi tunavyopata tukiwa mahotelini ugenini, tukihadisiana mambo ya safari uswahilini kwetu tunahisi tunakosa mambo mengi ya raha,
Hapo ndipo mawakala wa ngumi hutupata na mabondia huwa wanadiriki kukubali kwenda kucheza popote tukijua tutapanda ndege tunakula raha bila kujali  na wala kuhoji tuendako tutalipwa kiasi gani cha pambano nitakalocheza wala kujua usalama wangu.
Ukiangalia umbumbumbu na maskini tulionao mabondia,hapo wajanja wenye pesa zao,wafanyabiashara na baadhi ya viongozi wanatumia udhaifu tulionao mabondia kutuhadaa kwa kutupatia safari za nje za kimichezo au matembezi ya kwenda kufanya mazoezi ughaibuni na  hatimae kutubebesha mihadarati(madawa ya kulevya)  bila kujua kwa kutuwekea katika mizigo tunayosafiri nayo. Pindi kuna baadhi ya wafanya biashara hao wenye pesa zao hutuweka wazi wakati unaenda pigana umbebee mzigo wake na atakulipa pesa nyingi ,hapo ndipo tunapobanwa ukiangalia nyumbani tunalalia telemka tukaze tunashindia tembele mlo mmoja  msosi wa kengele tena kwa masimango,mfukoni sina kitu na wala sina kazi itakayonipatia pesa ya kula kwa sasa (hapo sijaingiza mambo ya kodi),demu wangu namlinda vipi.
Hii njaa na umaskini tulio nao mabondia,hapo ndio vigogo wanapoamua kututumia kwa  kutubebesha madawa ya kulevya kusafirisha nje wakijua wazi hatuwezi kataa kutokana na dhiki tuliyo nayo, tutakubali tu kwani hakuna apendae kulala njaa , kulala pachafu  au kuvaa midabwada.
’siwezi acha dili la pesa kama hili wakati jina langu kubwa kila kona linatajwa mitaani na vyombo vya habari lakini mimi binafsi nauli ya daladala sina,siku ya tatu leo nakula mlo mmoja kwa siku,watoto hawapo katika hali nzuri, mazoezi yenyewe sifanyi kwa raha nafikiria nitapata wapi mshiko,leo unaniletea ishu ya pesa niikatae si nitakuwa kichaa’wadau wenzangu wa ngumi ,wapambe wao,na walio karibu na sisi mabondia wana nguo za bei kubwa wanapendeza , wana magari, ukiangalia mimi bondia ndie mtendaji wao mkuu nipo ovyo sina kitu mfukoni wala tumboni madeni kibao yaani majanga matupu
Ushauri wangu kwa serikali au taasisi zinazohusika na wanaolichukia jambo hili kiukweli maana wengine hujifanya kulichukia mdomoni pembeni ndio watendaji wakuu wa kuwatumia wanamichezo au wasanii kwa faida zao. Mabondia au wanamichezo tuboreshewe maeneo yetu ya michezo ikiwemo katika vilabu vyetu na maeneo ya mazoezi, vifaa viongezwe ikiwezekana kodi ya vifaa vya michezo ipunguzwe ili viwe vingi nchini mabondia wasibabaike na vya kuazima au kuangalia katika tv vifaa nya wenzetu. Serikali iwajali mabondia, isaidie kudhamini semina za walimu wa ngumi ili wawaongoze vema vijana wao.magym ya makusudi yajengwe na maeneo ya wazi wasigawane wenye pesa na viongozi kwa faida zao  wajenge sehemu za michezo ya ndani(indoor), na kama pia itatumika njia ya kutoa madarasa matupu katika mashule yetu kwa ajili ya kutuachia sehemu ya mazoezi ya jioni itasaidia sana kukuza mchezo na walimu wenye taaluma kufundisha vizuri kuliko mabondia kufundishana vichochoroni na kutokuwa na nidhamu ya mchezo wala maisha
Na
 IBRAHIM ABBAS KAMWE
manager and boxing trainer of  Bigright boxing
Local Promoter via Bigright Promotion
Mwananyamala
Dar es salaam
+255 767 / 754 /  501991

SERIKALI YAMPA CHEKA VIWANJA VIWILI

Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda wanne kushoto akiwa na bingwa wa dunia wa mchezo wa masumbwi nchini Fransic Cheka baada ya kukaribishwa bungeni mjini Dodoma wengine kushoto Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  na bingwa wa mabara Fransic Miyeyusho kulia ni promota wa mchezo wa masumbwi nchini Mohamed Bawaziri,  na promota wa mpambano wa ubingwa wa Dunia ambao cheka anao kwa sasa Catherini Matili .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.comBingwa wa Dunia Mkanda wa WBF uzito wa super-middle, Francis Cheka, amezawadiwa viwanja viwili na serikali ya Mkoa wa Morogoro ikiwa ni zawadi na pongezi baada ya kufanikiwa kutwaa mkanda huo mkubwa duniani, hivi karibuni.


Cheka alifanikiwa kutwaa ubingwa huo wa dunia baada ya kumchakaza kwa pointi aliyekuwa akiushikilia ubingwa huo, Mmarekani Phil Williams katika pambano lililopigwa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga jijini Dar, Agosti 30, mwaka huu.

Cheka alipewa viwanja hivyo kwa nyakati tofauti mkoani Morogoro ambapo kimoja kipo Segera, Mvomero na kingine kipo Morogoro mjini.
Joel Bendera ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, alimkabidhi Cheka kiwanja kilichopo Morogoro mjini chenye thamani ya shilingi milioni sita kwa niaba ya manispaa ya mkoa huo huku wananchi wa mkoani humo wakiahidi kumjengea nyumba kwenye kiwanja hicho.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Cheka alisema amefurahia zawadi hiyo na amejisikia faraja kuona serikali inatambua umuhimu wake.

 “Nashukuru sana kwa kweli kwa viwanja hivi, kimoja kipo Segera, Mvomero, bado sijakiona ila hiki kingine cha mjini tayari nimeshakabidhiwa hati na kila kitu,” alisema Cheka.

Sunday, September 15, 2013

PICHA ZAIDI YA MPAMBANO WA FLOYD MAYWETHER NA CANELO ALVAREZ

Bondia floyd mayweather kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na  canelo alvarez wakati wa mpambano wao mayweather alishinda kwa point
MATOKEO KAMILI YA MPAMBANO WA floyd mayweather vs canelo alvarez Judges Dave Moretti (116-112) and Craig Metcalfe (117-111) scored the fight in favor of Mayweather, while C.J. Ross scored it a 114-114 draw.