Tangazo

Pages

Thursday, February 2, 2012

Rashidi MATUMLA VS MANENO OSWARD KUPAMBANA TENA Februar 25 UKUMBI WA PTA SABASABA DAR



BONDIA wa ngumi za kulipwa Rashid Matumla 'Snek man' amesema kukutana ulingoni mara kwa mara na bondia Maneno Osward 'Mtambo wa gongo' hawachezei njaa isipokuwa ni mapenzi ya ngumi aliyokuwa nayo.

Matumla na Maneno wanakutana ulingoni kwa mara ya tano sasa ambapo baadhi ya wadau wamekuwa wakihisi labda mabondia hao hupigana kwa sababu ya kutafuta fedha.

Akizungumza kwa njia ya simu Dar es Salaam jana, Matumla alisema yeye binafsi bado anauwezo wa kupigana katika mchezo huo na kama angetaka kustaafu angeweza kufanya hivyo ila bado anayo nafasi ya kufanya vizuri katika mapambano yake.

Alisema pambano lake dhidi ya Maneno litakalopigwa Februari 25 mwaka huu katika ukumbi wa PTA Sabasaba litakuwa ni pambano lake la tano kukutana na bondia huyo.

"Mimi na Maneno tumeshakutana mara nne ulingoni hadi sasa na hili litakuwa ni pambano letu la tano kupigana,"alisema Matumla na kuongeza kuwa.

"Katika mapambano hayo nimemshinda Maneno mapambano mawili, amenipiga pambano moja na tumetoka sare pambano moja lakini kama itawezekana nitamtwanga katika pambano lijalo,"alisema Matumla.

Alisema kwa sasa anajifua chini ya kocha wake Habibu Kinyogoli ambaye ameingia naye mkataba wa kumnoa na anainami atafanikiwa kumtwanga Maneno katika mchezo huo.

Pambano hilo la Februari 25 litakuwa ni pambano la marudiano kwa mabondia hao baada ya kutoka sare katika pambano la kwanza lililofanyika katika ukumbi wa Henken Mtoni Desemba 25 mwaka jana.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila ‘Super ‘D’.


“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’.

Wednesday, February 1, 2012

bdallah Mohamed 'Prince Nassime' kugombania ubingwa wa PST na Swaleh Mkalwekwa feb.24

 Bondia Abdallah Mohamed 'Prince Nassime' kulia akifuliwa na kocha wake msaidizi Rajabu
 Bondia Abdallah Mohamed 'Prince Nassime' kulia akifuliwa na kocha wake msaidizi Rajabu
Bondia Abdallah Mohamed 'Prince Nassime' (kulia) akioneshana ufundi wa kutupa makonde na Jofray Sadiq wakati wa mazoezi ya kujiandaa kugombania ubingwa wa taifa Kg.67 unaotambuliwa na shilikisho la kumi za kulipwa PST na Swaleh Mkalwekwa feb.24

FRANCIS CHEKA MADA MAUGO KUGOMBEA UBINGWA WA IBF RAUNDI 12 APRIL 28 PTA SABASABA


Bondia Fransic Cheka akizungumza na waandishi wa habari leo kupigania ubingwa  IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprilo 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Bondia Mada Maugo akiongea na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba uho leokupigania ubingwa  IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprilo 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Makamu mwenyekiti wa Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Nchini, Madaraka Nyerere (Kushoto) akiwaelekeza mabondia Fransc Cheka kulia na Mada Maugo jinsi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba April 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Sunday, January 29, 2012

FRANCIS CHEKA AMDUNDA KALAMA NYILAWILA KWA POINTI


Bondia Francis Cheka akinyoshwa mkono juu na refarii Nemesi Kavishe wakati wa mpambano wake na Kalama Nyilawila ambaye mpaka sasa aamini matokeo hayo
Askali wa usalama wakiendeleza ulinzi wakati wa mpambano huoo jana
Bondia Kalama Nyilawila Kushoto akioneshana ufundi na Frenisic Cheka
Fransic Cheka akinyosha mikono juu baada ya kuibuka mshindi
Francis Cheka kushoto na Kalama Nyilawila wakioneshana umwamba wa kutupa masumbwi jana
Baadhi ya mashabiki waliojitokeza wakati wa mpambano huu
Mawe ngumi makonde Boxing kushoto ni Francis Cheka na Kalama Nyilawila
Bondia Francis Cheka (kushoto) akioneshana umwamba wa kutupa masumbwi na Kalama Nyilawila wakati wa mpambano wao uliofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro mwishoni mwa wiki cheka alishinda kwa pointi.picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Madaraka Nyerere kushoto akifatilia mpambano huo jana
Baadhi ya wadau wakubwa wa mchezo wa ngumi wariofunga safari kutoka Dar kwenda Moro kuangalia mpambano kushoto ni kocha wa masumbwi nchini, Habibu Kinyogoli, Issa Malanga,Rashidi Mtulumla na Hssani Matumla
Bondia Ibrahimu Class (kushoto) akipambana na Venasi Mponji wakati wa mpambano wUtangulizi walitoka droooo
Bondia Ibrahimu Class akisikiliza maelezo toka kwa kocha wake habibu kinyogoli
Bondia Ibrahimu Class (kushoto) akipambana na Venasi Mponji wakati wa mpambano wUtangulizi walitoka droooo

Saturday, January 28, 2012

SUPER D BOXING C OACH KUSAMBAZA DVD ZA MAFUNZO LEO KATIKA UWANJA WA JAMHURI WAKATI CHEKA NA KALAMA WAKIPAMBANA


KALAMA NYILAWILA FRANSIC CHEKA USO KWA USO leo JANUAR 28

MIAMBA ya masumbwi nchini, bingwa wa Mabara Francis Cheka [SMG] na bingwa wa Dunia Karama Nyilawila [Kapten] wanatarajia kupanda ulingoni Januari 28 mwaka huu kuoneshana umwamba.
Cheka na Nyilawila hawajawahi kutwangana mpambano ambalo limewafanya mashabiki kuhisi kuwa mabondia hao wanaogopana.

Akizungumza Dar es Salaam jana, promota wa pambano hilo Philemon Kyando 'Don King' alisema pambano hilo litapigwa katika uwanja wa Jamhuri Morogoro nyumbani kwa Cheka.
Alisema pambano hilo litakuwa la raundi 10 uzito wa kg 72

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.

Alisema kutakuwa na pambano kati ya Maneno Osward [mtambo wa gongo] na Pasco Ndomba raundi nane uziti wa kg 75, Chaulembo Palasa na Deo Njiku kg 68, Venance Mpoji na Ibrahim Clases kg 63, Anthon Mathias na Juma Afande kg 54 na pambano la mwisho kati ya Hassan Kidebe na Arbert Mbena kg 54 ambapo mapambano hayo yatakuwa ya raundi sita kila moja.

Promota huyo alisema lengo la kumuandalia pambano Nyilawila na Cheka ni kuondoa uvumi kuwa mabondia hao wanaogopana lakini pia ni kuurudisha mchezo wa ngumi katika chati

Friday, January 27, 2012

FRANCIS CHEKA KALAMA NYILAWILA WAPIMA UZITO KWA AJIRI YA MPAMBANO WAO KESHO

FRANCIS CHEKA KALAMA NYILAWILA WAPIMA UZITO KWA AJIRI YA MPAMBANO WAO KESHO




Bondia Kalama Nyilawila (kushoto) akitunishiana misuri na Francis Cheka baada ya kupimauzito leo kwa ajiri ya mpambano wao utakaofanyika katika uwanja wa Jamhuri Morogoro kesho.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)